Jeshi la Nigeria linasema kuwa limewaua zaidi
ya wanamgambo 100 wa kundi la Boko Haram kufuatia shambulizi la
wapiganaji hao siku ya ijumaa kazkazini mashariki mwa jimbo la Borno.
Vikosi
vya serikali vimeripotiwa kuyakamata magari na risasi wakati vilipokuwa
vikiimarisha usalama katika mji wa Konduga,yapata kilomita 35 kutoka
mji mkuu wa jimbo hilo, Maiduguri.Wapiganaji wa Boko Haram wameiteka miji kadhaa na vijiji katika majuma ya hivi karibuni wakikaribia kuelekea Maiduguri.
0 comments:
Chapisha Maoni