Jumamosi, 13 Septemba 2014

MFUNGWA AKUTWA NA SIMU MWILINI


 Tatizo la kuingiza bidhaa kimagendo ndani ya magereza ya Kenya imekuwa kero kubwa kwa maafisa wa magereza.
Kwa baadhi ya watu simu ya mkononi ni kifaa tu cha mawasIliano ilihali kwa wengine ni kifa ambacho kinaweza kukuweka katika hali ya kufa kupona.
Mfungwa mmoja nchini Kenya amewaacha wengi vinywa wazi, baada ya simu tatu za mkononi kutolewa mwilini mwake. Inaarifia aliziingiza simu hizo mwilini mwake kupitia sehemu yake nyeti ya nyuma.
 
 Mfungwa ambaye alitolewa simu mwilini kwa kufanyiwa upasuaji.
Tatizo la kuingiza bidhaa kimagendo ndani ya magereza ni kero kubwa kwa maafisa wakuu wa magereza.
Wamekuwa kwa miaka mingi wakijaribu kulikomesha tatizo hilo bila mafanikio.Kwa njia yoyote ile wafungwa huingiza bidhaa kama simu katika magereza nchini Kenya kinyume na sheria za magereza.
Maafisa wa magereza wanakiri kwamba wafungwa hawa wakati mwingine hushirikiana na walinzi wa magereza kuingiza bidhaa katika magereza kimagendo.

0 comments:

Chapisha Maoni