Home »
» Alichojibu Guardiola baada ya kuulizwa kama ataifundisha tena Barcelona
Miaka takribani mitatu baada kuacha kuifundisha klabu ya FC Barcelona, kocha Pep Guardiola amezungumzia kama ikitokea nafasi ya kurudi Nou Camp – atakubali kuifundisha timu hiyo.
Akizungumza na gazeti la Mundo Deportivo Guardiola ambaye alijiunga
na Bayern Munich mwaka 2013 baada ya mapumziko ya mwaka mmoja baada ya
kuondoka Barca – amesisitiza haoni namna anaweza kurudi kuifundisha
klabu hiyo, kwa sababu alishamaliza kazi yake.
Boss huyo wa Bayern Munich alitumia miaka minne Nou Camp –
akitengeneza timu ambayo inatajwa kuwa bora kuliko zote katika historia
ya soka wakishinda makombe mawili ya ulaya na La Liga mara 3 kuanzia
mwaka 2008 mpaka 2012.
Baada ya miezi 12 ya mapumziko, Guardiola aliteuliwa kuwa kocha wa
Bayern Munich mwaka jana, japokuwa mara kwa mara imekuwa ikiripotiwa
kwamba anaweza kurejea kuifundisha Barca kwa muhula wa pili.
Lakini wakati kocha huyo mwenye miaka 43 akiwa anakiri kwamba atarudi
Catalonia kwenda kuishi na mkewe, anasema sio kwenda kuifundisha Barca
tena.
“Kwa haraka haraka tu naweza kukwambia kwamba sitoifundisha tena
Barca. Naamini kuna maduara kwenye maisha – langu mie na Barca
lilishaisha,” aliiambia Mundo Deportivo.
“Mke wangu anafanya kazi jijini Barcelona na wazo ni kurejea tena
hapa na kuishi na familia yangu, lakini sijui lini hiyo itakuwa.”
Related Posts:
Mdahalo Wa Tahliso Kujadili Hotuba ya Magufuli Waingia Dosari Baada Ya Wanafunzi wa UDSM Kuupinga
WAZIRI
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye jana alinusuru
kuvunjika kwa mdahalo ulioandaliwa na Jumuiya ya Taasisi za Elimu ya Juu
(TAHLISO), baada ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Sa… Read More
Asipofunga Zipu…Nay wa Mitego Atakufa Kwa Ngoma
Staa
wa Bongo Fleva, Emmanuel Eribaliki ‘Nay wa Mitego’ akijiachia na
mrembo mpya mwenye umbo dogo kwenye bwawa la kuogelea katika Hoteli ya
White Sands iliyopo Mbezi Beach jijini Dar.
KIWEMBE!
Ndivyo… Read More
Chadema Bado Hawajakubali Yaishe...Waapa Kumshughulikia Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo Bungeni
Chama
Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimeahidi kumshughulikia Bungeni,
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo kikidai kuwa bado
hajasafishwa kwenye kashfa ya akaunti ya Escrow.
Ahadi
hiyo il… Read More
Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Disemba 17, Siri Kung'oka Hoseah wa Takururu Hii Hapa
Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Disemba 17, Siri Kung'oka Hoseah wa Takururu Hii Hapa
… Read More
Waziri Atoa Mkwara Jeshi la Polisi Atoa Siku Mbili Aletewe Taarifa Kuhusu Udhibiti wa Madawa ya Kulevya na Watu Kubambikiwa Kesi
Waziri wa mambo ya ndani Charles Kitwanga amefanya ziara ya ghafla leo
Dec 16 2015 katika makambi mbalimbali ya Jeshi la Polisi Dar es salaam
na kutoa amri kwa viongozi wa jeshi hilo siku mbili za kuhakikisha
amepata ta… Read More
0 comments:
Chapisha Maoni