Kupitia youngluvega.blogspot.com siku ya juzi ulipata taarifa kuhusu msanii wa Bongo Fleva Diamond Platnumz kuachia nyimbo yake mpya ambapo kwa mara ya kwanza ilionyeshwa kupitia kituo cha MTV, na jana ikawa siku rasmi ambayo Diamond aliachia nyimbo hiyo.
Leo Novemba 21, Diamond amesikika kwenye show ya XXL
 ambapo amezungumzia mambo mengi, baadhi ya yale aliyoyazungumzia ni 
pamoja na story zilizoenea mitandaoni kwamba mahusiano ya msanii huyo na
 Wema yameisha pamoja na story ambayo imetokana na kuenea kwa picha 
mitandaoni za msanii huyo na Zari the Boss Lady kutoka Uganda.
Hii ni sehemu ya mahojiano aliyofanya Diamond kwenye XXL:
Adam Mchomvu :”…Nataka
 kujua ile vibe ya Fiesta that day, story zilikuja ooh Diamond 
kazomewa.. kazomewa kazomewa..na vitu kama vile, sijapata chance ya 
kukusikia wewe una kipi cha kuzungumzia kuhusiana na that situation..?“
Diamond :- “…
 Siku zile kwangu ilikuwa kama mchezo, unajua muziki ushakuwa kama sio 
fani tena, ushakuwa kama siasa.. So, lazima uichukulie hivyo wewe 
mwenyewe kama msanii ujue una control vipi kwa sababu sio mara ya kwanza
 vitu kama hivyo vishatokea Maisha.. Maisha yalitupwa mpaka na mayai 
viza kabisa.. Ni vitu ambavyo vikitokea naonaga kama ni kawaida…“
B 12  :-“…Kwa hiyo ukweli uko wapi kati yako wewe na Wema Sepetu?...”
Diamond  :- “…Kuna
 vitu vitu fulani nadhani kuvizungumza sio vizuri… Lakini ikifikia 
kuvizungumzia vinazungumziwa… Uzuri wa mahusiano yetu ni kwamba kila mtu
 anafahamu… Haijafikia kuweka wazi ndio maana ninapoulizwa inakuwa ni 
swali gumu kulijibu.. “
B 12 :- “.. Ni gumu kwa upande wako lakini yeye yuko tayari kuzungumza kwamba it’s over kati yangu mi’ na Diamond…“
Diamond  :- “… Sijui…“
B 12  :- “...Hii
 ngoma kama umemzungumzia yeye direct hivi… watu wamekuza akili zao 
zikaenda mbali zaidi kimawazo lakini, kwamba inawezekana ile singo 
umemwimbia yeye hivi kwamba bado unamzimia japokuwa bado kama kakutosa 
hivi…“
Diamond  : “.. Waswahili
 wanasema ‘A’ na ‘B’ yote majibu, halafu ukisikiliza ile nyimbo kama 
kweli mtu mwenye ufahamu wako, kweli kabisa hauwezi kuwa na maswali 
mengi …“
Kuhusiana na mahusiano yake na Zari the Boss Lady, Diamond amejibu hivi:
Diamond  :- “..
 Zari ni rafiki yangu tu, alipokuja hapa mimi ndio nilikuwa mwenyeji 
wake Tanzania na kama mimi ndiyo mwenyeji sikutaka kuleta roho za 
kibaguzi, unajua hata alipokuja Davido pia ilibidi awe na mimi karibu 
ili hata kesho na kesho kutwa  mimi nikiwa Nigeria basi Davido anipokee 
hivyo hivyo…“
Iko hapa full Interview ya Diamond kwenye XXL, unaweza kuisikiliza kwa kubonyeza play.






 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
0 comments:
Chapisha Maoni