Ijumaa, 21 Novemba 2014
Home »
» Kipa wa Chelsea yuko sokoni.
Kipa wa Chelsea yuko sokoni.
Klabu za Arsenal , Liverpool na Real Madrid ziko kwenye vita kali ya kuwania kumsajili kipa wa Chelsea Petr Cech .
Chelsea inaalzimika kumuuza kipa huyo kwa kuwa hana nafasi ya kudumu kwenye kikosi cha kwanza baada ya kurudi kwa kipa Mbelgiji Thibaut Courtois .
Hadi sasa Chelsea haijapoteza mchezo wowote msimu huu huku Thibaut akicheza kwenye mechi karibu zote hali inayomfanya Cech kulazimika kutafuta mahali kwingine ambako atakuwa chaguo la kwanza .
Cech ameidakika Chelsea kwa mafanikio makubwa kwa muda wa miaka 11 tangu aliposajiliwa kwa mara ya kwanza akitokea Rennes ya Ufaransa .
Katika kipindi hicho Cech amefanikiwa kutwaa mataji kadhaa yakiwemo matatu ya ligi kuu ya England , UEFA Champions league na UEFA Europa League bila kusahau kombe la Fa na kombe la Carling ambalo siku hizi hufahamika kama Capitol One Cup.
Akijibu maswali ya waandishi wa habari kocha wa Chelsea Jose Mourinho alikanusha taarifa kuhusu Cech kuwa mbioni kuhama ambapo alisema kuwa hajawahi kupata taarifa yoyote kama hiyo .
Kwa upande mwingine wakala wa Cech Viktor Kolar ameendelea kushikilia msimamo ulioripotiwa na vyombo vya habari kuwa kuna klabu zisizopungua tano ambazo zimeonyesha nia ya kumsajili kipa huyo .
Hadi sasa inafahamika kuwa Arsenal ndio iko kwenye nafasi ya juu kumsajili Cech kwa thamani ya puandi milioni 7 lakini kumekuwa na ishara toka kwa klabu za Ac Milan , As Roma , Real Madrid na Liverpool za kutaka kumsajili Cech .
0 comments:
Chapisha Maoni