Vikosi vya usalama nchini Lebanon
vimemkamata mkewe kiongozi wa kundi la wapiganaji wa kiislamu la IS Abu
Bakr al-Baghdadi karibu na mpaka na Syria na mwanawe mvulana.
Jeshi
linasema kuwa Mkewe Baghdadi alikamatwa pamoja na mwanawe ingawa majina
yao hayajatolewa. Walikamatwa na wakuu wa ujasusi baada ya kuingia
Lebabon siku kumi zilizopita.Jarida la al-Safir liliripoti kuwa mkewe Baghdadi anahojiwa katika ofisi za waizara ya usalama nchini Lebanon.
Mnamo mwezi Juni, Baghdadi alitajwa kama kiongozi wa kundi hilo katika maeneo ya Syria na Iraq ambayo yanadhibitiwa na IS.
Mwezi jana kundi hilo lilikannusha madai kuwa kiongozi huyo aliuawa au kujeruhiwa, katika shambulizi la angani lililofanywa na majeshi ya Marekani, mjini Mosul.
Kundi lenyewe lilitoa kanda ambapo lilisema utawala wao unapanuka na kutoa wito kwa wapiganaji wa jihad kujitolea mhanga.
Jarida lililoripoti kukamatwa kwa mkewe Baghdadi, limesema kuwa maafisa wa usalama walikuwa wameiweka operesheni yao kama siri kubwa kiasi kwamba hakuna aliyekuwa na taarifa kuhusu operesheni yenyewe.
Mwandishi wa BBC Jim Muir, ambaye yuko, anasema kuwa kukamatwa kwa mkewe Baghdadi na mwanawe kutawaweka katika hali tatanishi ambayo inaendelea kuibuka Lebanon.
Kundi la IS pamoja na kundi lengine la jihad al-Nusra linawazuilia wanajeshi 20 wa Lebabon kama mateka.
0 comments:
Chapisha Maoni