Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es salaam, limemtaka Mwenyekiti wa
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kujisalimisha Polisi mara
moja kwa ajili ya Mahojiano yanayohusu vita vya dawa za kulevya baada ya
juhudi za kumsaka katika makazi yake kushindikana huku simu yake ya
mkononi ikiwa imezimwa
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam Kamanda wa
Polisi Kanda Maalum Simon Sirro amesema Bw. Mbowe aliahidi kwenda
mwenyewe juzi tarehe 15, lakini hakwenda lakini jeshi la hilo
lilimtafuta usiku na mchana katika makazi yake na kumpigia simu lakini
simu yake ilizimwa
Aidha jeshi hilo limesema watuhumiwa watatu Agnes Masogange, Rashid Idd
au Chid Mapenzi na Wallis Latif Nasher ambaye ni muuza magari katika
eneo la mikocheni watapandishwa kizimbani Jumatatu kwa kosa la kukutwa
na dawa za kulevya lakini pia walibainika wanaotumia dawa hizo baada ya
kupelekwa kwa Mkemia Mkuu
Katika kupambana na Askari feki, jeshi limemtia mbaroni aliyekuwa askari
Magereza wa cheo cha Koplo Peter Elias Msigwa aliyekuwa mtumishi katika
gereza la keko, ambaye alifukuzwa kazi Desemba mwaka jana, lakini
alikamatwa jana akiwa na mavazi ya kiaskari tena akiwa amejipandisha
cheo kutoka koplo hadi Sajenti wa Polisi
Jeshi hilo pia limesema limewatia mbaroni watu 65 kwa kosa la kukutwa na
dawa za kulevya pamoja na watuhumiwa 73 wa wizi na ujambazi wa kutumia
silaha, mitambo mitano ya Gongo, lita 270 pamoja na Puli 250 za bangi.
0 comments:
Chapisha Maoni