Taarifa kutoka mjini Washngton 
zinaeleza kua mwanamume mmoja aliyekua ameshikilia kisu mikononi mwake 
aliruka uzio wa makao ya Rais wa Marekani Brack Obama na kukimbia 
kuelekea kwenye makazi hayo mwezi huu .
Maafisa wa Ikulu hiyo 
wamemtambua mtu huyo kua ni Omar Gonzalez,askari wa zamani aliyepigana 
Iraq, alikua pamoja na kisu,alikuwa akikimbilia katika mlango mkuu wa 
makazi ya Rais Obama kabla hajakatwa na maofisa wa Ikulu hiyo maarufu 
kama White House .Taarifa zinaeleza kuwa kiboksi chenye kengele ya tahadhari kilikuwa kimezimwa .Mkuu wa shughuliza siri za ikulu hiyo Julia Pearson anatarajiwa kuhojiwa kufuatia tukio hilo na jopo la wanasheria.
Wakati hayo yakitukia Rais Obama na familia yake hawakuwa katika Ikulu hiyo.






 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
0 comments:
Chapisha Maoni