Poda ya Johnson, iliyodhaniwa kuwa ni kipodozi na tiba mujarabu kwa watoto na watu wazima duniani kote imebainika kusababisha saratani.
Jana, Mahakama ya St Louis ya Marekani, iliiamuru kampuni inayotengeneza poda hizo, Johnson & Johnson kumlipa Deane Berg wa Sioux Falls, South Dakota, Dola za Marekani 55 milioni (Sh118 bilioni ) baada ya kujiridhisha kuwa kipodozi hicho kilimsababishia saratani ya mayai ya uzazi (ovarian cancer).
Mpaka sasa, zaidi ya wanawake 1,000 wameshafungua kesi kuishtaki kampuni hiyo kwa madai ya kuwasababishia saratani hiyo baada ya kutumia poda ya Johnson kwa miaka mingi.
Ofisa Uhusiano wa Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania, (TFDA), Gaudensia Simwanza alisema wanazo taarifa juu ya madhara ya poda hizo ingawa bado hawajathibitisha kitaalamu kwa poda zilizopo nchini.
Alisema TFDA ilishafanya uchunguzi wa kimaabara kuhusu poda hizo lakini haikuona madhara yoyote.
Simwanza alisema FDA ilitakiwa pia kuwapa taarifa watumiaji wa bidhaa hizo duniani kuhusu madhara ya poda hizo.
Mwaka 2013, Berg alikuwa mwanamke wa kwanza kuishtaki kampuni hiyo baada ya kugundulika na saratani.
Baada ya kuridhishwa na malalamiko ya Berg, Mahakama iliamuru kampuni ya Johnson & Johnson kutoa onyo kuwa poda hizo, Johnson Baby Powder na sabuni ya Shower to Shower, zinasababisha saratani. Hata hivyo, kampuni hiyo haikufanya hivyo.
Baada ya mwaka mmoja, Berg alifungua tena kesi hiyo na Mahakama iliamuru alipwe kiasi hicho cha fedha.
Daktari wa Hospitali ya Wanawake, Brigham, Daniel Cramer alitoa ushahidi mbele ya Mahakama na kueleza kuwa zaidi ya wanawake 10,000 wamegundulika kuwa na saratani ya mayai ya uzazi kwenye hospitali hiyo.
Kadhalika, wanawake hao walibainika kuwa na chembechembe za ‘talcum’ kwenye kizazi.
Daktari wa Saratani wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, Herry Tungaraza alisema kuna uwezekano wa kemikali ya ‘talcum’ kupenya kwenye ngozi, hadi kwenye damu na kuingia kwenye mayai ya uzazi na kisha kusababisha saratani.
Alisema si lazima poda hizi zimuathiri mtu kwa kuzitumia sehemu za siri tu, hata kama akizitumia kwa kupaka usoni, zinaweza kusafiri na kuathiri mayai ya uzazi. “Kama ingekuwa zinadhuru kwa kuzipaka sehemu za siri tu, basi zingeathiri zaidi shingo ya kizazi au nyumba ya uzazi, lakini mayai yapo mbali na ndiyo yaliyoathiriwa na saratani,” alisema.
Shahidi mwingine wa katika kesi ya Berg alithibitisha kuwa aliona chembechembe za ‘talcum kwenye uvimbe ulioko kwenye mayai ya Berg.
Mwathirika mwingine
Mei mwaka jana, Gloria Ristesund (62), alifungua kesi dhidi ya Johnson & Johnson kwa kushindwa kuwaonya wateja wake kuhusu poda hiyo kusababisha saratani.
Ristesund aligundulika na saratani, mwaka 2011 baada ya kutumia poda hiyo kwa kuipaka sehemu za siri kwa miaka kadhaa hasa. Mahakama iliamuru Ristesund pia kulipwa Dola 55 milioni.
Tovuti ya CNN inaeleza kuwa utafiti kuhusu kemikali za ‘talcum’ kusababisha saratani ulitolewa miaka mingi nyuma lakini Johnson & Johnson hawakutaka kuweka wazi ukweli huo kwa wateja wao.
“Ni kama kampuni zinazotengeneza sigara, wanajua kuwa imeshathibitishwa kuwa uvutaji wa sigara unasababisha saratani ya mapafu lakini wanauficha umma kuhusu hili,” ilisema taarifa ya CNN.
Alhamisi, 5 Mei 2016
Home »
» Kampuni yatozwa Sh118 Bilioni Poda yake Kusababisha Saratani
Kampuni yatozwa Sh118 Bilioni Poda yake Kusababisha Saratani
Related Posts:
Wasira: Uzee Haunizuii Kudai Haki Yangu Waziri wa muda mrefu na mbunge wa zamani wa Bunda, Steven Wasira amewajibu wanaodai kwamba amelazimika kustaafu siasa baada ya mpinzani wake, Ester Bulaya kuwashinda wapigakura wanne waliokuwa wakipinga ushindi w… Read More
Wakili wa Serikali Amuomba Radhi Hakimu kwa Kushindwa Kumkamata Tundu Lissu Wakili wa Serikali, Patrick Mwita amemuomba radhi Hakimu Mkazi Mkuu wa Kisutu kwa kushindwa kutekeleza amri ya kumkamata mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu anayekabiliwa na kesi ya uchochezi pamoja n… Read More
Soudy Brown Afanyiwa Interview, Kumbe Alikuwa Anafanya Kazi TBC Mzee wa Ubuyu Soudy Brownkafanyiwa interview na TBC amabapo ana dai ndio sehemu iliyomleaamefungukia aanvyotukanwa instagram na anavyochuliaPia amesema anapenda kuvaa mask kama swag tu, na akiivua anakuwa sio Soudy … Read More
Rais Mugabe Asema Anarogwa Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe, mwenye umri wa mika 92, anazungumzia kuhusu kustaafu , lakini swali ambalo bado watu wanahoji ni ikiwa kweli anamaanisha hilo.Mwishoni mwa juma Bwana Mugabe aliuambia mkutano wa watu … Read More
Dar Mpya ya Makonda: Makonda Aitaka Takukuru Kuchunguza Madai ya Ufisadi katika Mradi wa Nyumba ‘Avic Town’ Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amenusa ufisadi katika mradi wa ujenzi wa nyumba za Avic ‘Avic Town’ na kuitaka taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), kuuchunguza mradi huo uliopo Kigambo… Read More
0 comments:
Chapisha Maoni