Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad,
amerejea kauli yake ya kutotambua kufutwa kwa uchaguzi mkuu wa Zanzibar
uliofanyika tarehe 25 mwezi uliopita.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam mara baada ya
kikao cha mashauriano na viongozi wa Umoja wa Katiba ya Wananchi UKAWA,
Maalim Seif amesema Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar Bw Jecha
Salim Jecha hana mamlaka ya kufuta uchaguzi huo, na kinachohitajika na
kuendelea na mchakato wa kuhakiki kura zilizobakia na mshindi
kutangazwa.
Kuhusu tamko lililotolewa na serikali juu ya kufutwa rasmi kwa uchaguzi
huo kupitia tangazo lililochapishwa kwenye gazeti rasmi la serikali
tarehe sita mwezi huu, Maalim Seif amesema tamko hilo limekosa uhalali
tangu lilipotolewa na Mwenyekiti wa ZEC.
Maalim Seif ambaye pia ni Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CUF amesema
Chama chake hakijalizingatia tamko hilo na wala hakijadili uwezekano wa
kurejewa kwa uchaguzi huo, kwa madai kuwa uchaguzi ulikamilika bila ya
kuwepo malalamiko kutoka chama chochote cha siasa na wala Tume ya
Uchaguzi.
Mapema akizungumza baada ya kikao hicho cha mashauriano, aliyekuwa
mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chadema Mhe.
Edward Lowassa amesema kikao hicho kilichojadili Mkwamo wa kisiasa
Zanzibar kimekwenda vizuri.
Hata hivyo amesema ufafanuzi zaidi utatolewa Jumapili ijayo ambapo
viongozi hao wanakusudia kuzungumza na waandishi wa habari jijini Dar es
Salaam.
Kabla ya kikao hicho Maalim Seif alifanya mazungumzo na Balozi wa Umoja
wa Ulaya (EU) Bw. Filberto Seregondi katika hoteli ya Serena jijini Dar
es Salaam na kuelezea hatua zinazochukuliwa kukwamua mkwamo wa kisiasa
Zanzibar.
Balozi Seregondi ambaye anamaliza muda wake wa utumishi hapa
nchini,aliambatana na ujumbe wa waangalizi wa uchaguzi mkuu wa Tanzania
kutoka Umoja huo.
Ijumaa, 13 Novemba 2015
Home »
» Maalim Seif azugumza na Balozi wa EU na viongozi wa UKAWA....Atoa Msimamo Mzito
Maalim Seif azugumza na Balozi wa EU na viongozi wa UKAWA....Atoa Msimamo Mzito
Related Posts:
Maneno ya DC Paul Makonda kuhusu kufanikisha kutatua mgomo wa kiwanda cha URAFIKI Dar.. Siku chache zilizopita wafanyakazi wa kiwanda cha nguo cha urafiki walifanya mgomo kwa madai ya kutolipwa mishahara yao kwa muda mrefu kupelekea mkuu wa wilaya … Read More
Home Shoppinga Center Yajitokeza Kujibu Tuhuma Za Kukwepa Kodi Baada ya kusambaa kwa taarifa kwenye mitandao zikieleza kuwa kampuni ya Home Shopping Centre imefunga maduka yake kutokana na kukwepa kodi na kuhusika kwenye sakata la makontena yaliyopotea bandarini, uongozi wa kampun… Read More
Wema Sepetu Kortini Kwa Uwizi wa Umeme..Tanesco Waeleza Makubwa KIMENUKA! Baada ya Miss Tanzania 2006 aliye pia nyota wa sinema za Bongo, Wema Sepetu ‘Madam’ kunaswa na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) akidaiwa kutumia umeme wa shirika hilo kinyemela, kuna madai atapandishwa kort… Read More
Huyu ndio kocha anayenyemelea kibarua cha Louis van Gaal Man United, kakiri hapa … Kuna mengi yanaendelea katika soka, tetesi na uvumi katika soka ni moja kati ya vitu vinavyo ingia katika headlines kila siku, vilabu vingi duniani vimekuwa vik… Read More
Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumanne Ya Disemba 8, Ikiwemo ya Magufuli Kufuta Nyayo za Sitta na Mwakyembe … Read More
0 comments:
Chapisha Maoni