
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Magufuli 
huenda akasafiri kwa mara ya kwanza nnje ya nchi toka aingie madarakani 
mwishoni mwa mwaka jana kuelekea nchini Ethiopia  ambapo atakutana na 
viongozi wa serikali na Nchi za Afrika zaidi ya 50 katika kikao cha 26 
cha Mkutano wa Umoja wa Afrika Mjini Addis Ababa, Ethiopia baadaye wiki 
hii.Masuala ya amani na ulinzi yatakuwa katika ajenda ya juu hasa 
ikichukuliwa kile kinachoendelea katika nchi ya Burundi na pia 
mashambulizi ya kigaidi yaliyofanyika katika nchi za Burkina Faso na 
Somalia.
Viongozi wa serikali na nchi za Afrika wanatazamiwa 
kushiriki katika kongamano la 26 la Baraza Kuu la Umoja wa Afrika, 
litakalofanyika kati ya Januari 30 na 31 ambapo pia watamchagua 
Mwenyekiti Mpya wa Umoja wa Nchi za Afrika(AU).Kwa mara nyingine tena 
viongozi wa Umoja wa Afrika(AU) wanatazamiwa kushinikiza kufanyika 
mageuzi katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.Licha ya pingamizi 
kutoka nchi 5 wanachama wa kudumu wa baraza hilo huko nyuma, viongozi wa
 AU wamesema kwa mara nyingine tena watashinikiza mageuzi katika chombo 
hicho, wakisisitiza kuwa muundo wa sasa wa baraza hilo hauakisi hali 
halisi ya siasa na uchumi wa dunia katika karne hii ya 21.Kamati ya nchi
 10 za Kiafrika juma lililopita ilifanya kikao na kuafikiana kuwa 
maslahi ya nchi Afrika katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ndio
 miongoni mwa ajenda kuu za kikao cha Addis Ababa. Nchi hizo ni Algeria,
 Libya, Senegal, Sierra Leone, Namibia, Zambia, Uganda, Kenya, 
Equatorial Guinea na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.Viongozi hao 
wanatazamiwa kurejea mwito wao wa kutaka nchi mbili za Kiafrika ziwe 
wanachama wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Kwa sasa 
nchi 5 wanachama wa kudumu wa Baraza la Usalama la UN ni Marekani, 
China, Russia, Ufaransa na Uingereza.Viongozi wa Kiafrika wanazituhumu 
nchi wanachama wa baraza hilo kuwa hazina demokrasia na kwamba zimekuwa 
zikitumia kura zao za veto kwa ajili ya maslahi yao binafsi.Viongozi wa 
Umoja wa Afrika aidha wanapendekeza kuongezwa idadi ya nchi wanachama wa
 Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kutoka 20 hadi 25.Hii itakuwa ni 
nafasi kwa Rais Magufuli kufanya safari ya nje ya nchi kwa mara ya 
kwanza tokea achaguliwe kuwa Rais wa Tanzania.Rais magufuli kwa sasa 
amekuwa gumzo katika majukwaa ya kimataifa kutokana na aina ya uongozi 
wake ambao wachambuzi wa kisiasa wanadai ni nadra kuupata kwa viongozi 
wan chi za Afrika ambapo rushwa, ufisadi, uvivu na ubadhirifu wa mali ya
 umma ni moja ya maisha ya viongozi wakuu wa nchi.






0 comments:
Chapisha Maoni