Diamond Platnumz amesema akiachana na muziki anataka kuwa Waziri wa 
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ili kuweka vitu sawa na kutoa fursa 
zaidi kwa vijana.
Akizungumza katika kipindi cha Papaso cha TBC FM, Diamond alisema kama 
akiingia kwenye siasa basi nia yake ni kuwa Waziri wa Michezo.
“Kwa sasa hivi siasa bado ila nikiingia kwenye siasa baadaye akimaliza 
mheshimiwa Nape nachukua mimi kile cheo cha Waziri wa Michezo,” alisema 
na kuongeza;
“Kile nakiweza kabisa kwa sababu mimi ukinimbia sijui kuhusu mpira, 
movie mimi naweza kabisa nikiwa Waziri, nikavifanya na vikawa na 
maendeleo.
"Ni kitu ambacho naweza siyo nasema nataka kuwa mbunge ila mimi nataka 
ile siku nimeacha kufanya muziki naingia kwenye siasa basi nakuwa Waziri
  wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na kuboresha vitu”
Diamond ambaye hakuweka wazi kwamba ataingia kwenye siasa kupitia chama 
gani, mwaka jana katika kampeni za uchaguzi mkuu uliomuingiza rais 
Magufuli madarakani, alishiriki kikamilifu kwenye kampeni za CCM na 
kutengeneza wimbo pamoja na video.
Jumanne, 26 Januari 2016
Home »
 » Diamond Platnumz: Baada Ya Nape Nnauye Mimi Ndo Waziri wa Habari Na Michezo Mtarajiwa 







 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
0 comments:
Chapisha Maoni