Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Singida, Simion Mumbee amesimamishwa kazi baada ya kudaiwa kutoa taarifa za uongo kuhusu watumishi hewa.
Katika taarifa hiyo, Mumbee anadai watumishi hewa 19 waliogundulika kwenye halmashauri hiyo hawajaisababishia hasara Serikali jambo linalodaiwa kuwa si kweli.
Akizungumza jana kwenye ufunguzi wa kikao cha maendeleo mkoani humo, Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mathew Mtigumwe alisema anamsimamisha kazi mkurugenzi huyo ili kupisha uchunguzi.
“Nilipotuma tume kufuatilia suala la watumishi hewa katika Halmashauri ya Wilaya ya Singida, ilibaini wapo na wameisababishia Serikali hasara ya zaidi ya Sh125 milioni,” alisema Mtigumwe.
Alisema taarifa ya Mumbee ililenga kuidanganya Serikali. Mtigumwe alimuagiza Katibu Tawala wa Mkoa, Dk Angela Lutambi kumuandikia barua ya kumsimamisha kazi mara moja.
Mtigumwe alisema hana nafasi ya kufanya kazi na watumishi wa aina ya Mumbee.
Wakati huo huo; Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Said Mwambungu amemsimamisha kazi Ofisa Utumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea, Philbert Mtweve kwa tuhuma za kuwalipa mishahara watumishi hewa wanane na kuisababishia Serikali hasara ya Sh27 milioni.
Ijumaa, 6 Mei 2016
Home »
» Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Singida Asimamishwa Kazi Baada ya Kutoa Taarifa za Uongo Kuhusu Watumishi HEWA
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Singida Asimamishwa Kazi Baada ya Kutoa Taarifa za Uongo Kuhusu Watumishi HEWA
Related Posts:
Shetta Akanusha Taarifa Kuwa Diamond Amewahi Kutoka Kimapenzi na MkeweShetta amekanusha taarifa zilizozagaa mitandaoni kuwa Diamond amewahi kutoka kimapenzi na mama Qayllah. Wiki kadhaa zilizopita Shetta alifuta picha zote kwenye akaunti yake ya instagram huku akiwaacha mashabiki wake wakijiuli… Read More
Viongozi Wakuu Wote wa Taifa Wako nje ya Nchi ..Nani Anaongoza Nchi Kwa Sasa?Viongozi wakuu wote wa Taifa wako nje ya nchi katika ziara za kiserikali kwenye mataifa tofauti. Rais John Magufuli aliwasili Uganda jana asubuhi kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais mteule wa nchi hiyo, Yoweri Museveni z… Read More
MAHAKAMA YA MAFISADI KUANZA RASMI LEOMAHAKAMA Maalumu ya kushughulikia Makosa ya Rushwa na Ufisadi, inaanza rasmi leo Julai mosi. Pamoja na kuanza kwa mahakama hiyo, serikali imeanza mchakato kuifanyia marekebisho Sheria Namba 11 ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa… Read More
Mpinzani wa Museveni , Dr Kiiza Besigye Akamatwa Baada ya Kujiapisha Kuwa RaisMpinzani mkuu wa Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, Dk. Kizza Besigye ambaye amekuwa akipinga ushindi wa Rais huyo, amekamatwa na polisi wa nchi hiyo baada ya jana kujiapisha kuwa Rais ikiwa ni siku moja tu (leo) kabla ya Musev… Read More
UN WAKUNWA NA KASI YA JPM SHIRIKA la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), limeeleza kuridhishwa kwake na utendaji wa Rais John Magufuli katika mapambano ya rushwa, kuongeza uwajibikaji na ukusanyaji wa mapato. Mwakilishi Mkazi wa UNDP nchini, Alvaro… Read More
0 comments:
Chapisha Maoni