Mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara (Chadema) ametolewa nje ya Bunge baada ya kutaka kumkwida Mbunge wa Kasulu Vijijini, Agustine Holle (CCM) aliyedai kuwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu na Mbunge wa Kibamba, John Mnyika wote wa Chadema kuwa wanaugua kichaa.
Waitara alionesha kukerwa na kauli hiyo hasa pale Holle alipokataa kufuta kauli yake, licha ya kutakiwa kufanya hivyo na Naibu Spika, Dk Tulia Akson.
Wakati Holle akichangia, Waitara alinyanyuka kwenye kiti chake na alipofika alipo mbunge huyo alimzungumzisha maneno ambayo hayakusikika na kuonesha kama kutaka kumpiga kabla ya kukaa kwenye kiti kilicho mbele yake ndipo, Holle alisikika akisema “wewe unataka nini” ndipo Naibu Spika alipogundua kuwa Waitara anataka kumpiga Holle na kumuamuru atoke nje lakini hakutii amri hiyo.
Kutokana na kutotii, Naibu Spika aliamuru askari wamtoe ndipo walipoingia zaidi ya askari watano na kutoka naye hadi nje ya geti kubwa la kuingilia bungeni.
Holle wakati anachangia bajeti ya Wizara ya Katiba na Sheria kwa mwaka wa fedha 2016/2017, alimtaja Lissu ambaye ni Waziri Kivuli wa Wizara hiyo kuwa ana taarifa kuwa Lissu amewahi kuugua ugonjwa wa kichaa na hadi sasa ana faili kwenye Hospitali ya Vichaa ya Mirembe iliyopo mkoani Dodoma.
Hata hivyo, alipopewa nafasi na Naibu Spika kufuta kauli yake akasema “nafuta kauli yangu lakini kwa taarifa zilizozagaa nimeamini ni kweli na mbona kwao(Chadema) wapo wengi hata Mnyika sasa hivi yupo Muhimbili anatibiwa kichaa”.
Kutokana na kauli hiyo, Lissu alisema licha ya kuifahamu Hospitali ya Mirembe, hajawahi hata kuingia kwenye geti la hospitali hiyo wala kuugua ugonjwa huo na kutaka kiti cha Naibu Spika kimtake Holle athibitishe ; na akishindwa kanuni zielekeze hatua za kuchukua kama zilivyowekwa.
Ijumaa, 6 Mei 2016
Home »
» Mwita Waitara Azusha Tafrani Bungeni.......Ni Baada ya Kutaka Kumchapa Ngumi Mbunge wa Kasulu Aliyedai Tundu Lissu na Mnyika Ni Vichaa
Mwita Waitara Azusha Tafrani Bungeni.......Ni Baada ya Kutaka Kumchapa Ngumi Mbunge wa Kasulu Aliyedai Tundu Lissu na Mnyika Ni Vichaa
Related Posts:
Makonda Amkumbusha Spika Kuwapima Wabunge Kilevi Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda, amemkumbusha Spika wa Bunge. Job Ndugai, kuhusu kusudio lake la kuanza kuwapima wabunge kubaini kama wametumia kilevi kabla hawajaiingia kwenye ukumbi wa chombo hicho cha kutu… Read More
Hivi ni Kwanini Wanawake Wengi Hujivunia Sana Makalio Yao? Angalia hata picha wanazopiga wanawake utaona jinsi wanavyojibinua ili wanaonekane wana makalio makubwa. Hata wakati wa kutembea pia wengine hutembea tofauti ili kuhakikisha kuwa makalio yake yanatikisika na nd… Read More
Mke Wangu Anunuliwa Nguo za Ndani na Mwanaume Baada yakudakua mawasiliano ya mke wangu na kukuta Jamaa akimwambia zawadi yako ipo tayari hivyo watafutane ampatie.. Baada ya siku mbili tatu nakaona kimfuko kipo na chupi nne na brazia mbili, sikuuliza ila nikahisi hii … Read More
UTAFITI: Wanawake Weupe Wanaringa Kuliko Weusi Home Urembo UTAFITI: Wanawake Weupe Wanaringa Kuliko Weusi UTAFITI: Wanawake Weupe Wanaringa Kuliko Weusi Urembo Kutokana na utafiti nil… Read More
Huwa Napata Shida sana Nikikutana na Wanawake Wenye Hii Tabia Huwa napata shida sana nikikutana na Wanawake wenye hii tabia...Unampenda Mwanamke kabisa from ur heart,unajipanga unampiga saundi..anakujibu,''How old are you kaka'' unamwambia am 29 years..utamsikia,''Oh my Gho… Read More
0 comments:
Chapisha Maoni