Tatizo la uwezo wa kufanya tendo la ndoa linazidi kukua miongoni wa
wanandoa na wapenzi wengi. Takwimu za kitafiti zinaonyesha kuwa karibu
ndoa 4 kati ya 10 zenye umri wa miaka 3 na kuendelea zinakabiliana na
tatizo hili. Aidha wanaume 6 kati ya 10 wanatajwa kulalamikia upungufu
wa nguvu za kiume.
Pamoja na matatizo mengine kutajwa kuchangia upungufu wa nguvu za kiume
na kushuka kwa msisimko wa tendo miongoni mwa wanandoa, uchunguzi
umeonesha kuwa utumiaji holela wa vyakula hasa vyenye mafuta ni moja
kati ya sababu zinazochangia kwa kasi tatizo hili.
Kwa kuzingatia hilo, watafiti wa masuala ya uhusiano wa kimapenzi
wamebaini aina mbalimbali ya vyakula ambavyo vina uwezo wa kumuongezea
mtu nguvu ya kufanya tendo la ndoa. Vyakula hivyo ni hivi vifuatavyo:
1. PILIPILI
Kama tunavyojua wote mara nyingi chakula ambacho kimeungwa pilipili
hufanya hata mapigo ya moyo kuwa tofauti na wakati mwingine hata jasho
au kamasi hutoka. Ndani ya pilipili kuna kitu kinaitwa capsaicin ambacho
hufanya pilipili iwe na hali ya ukali. Capsaicin huwezesha ubongo kutoa
homoni ya endorphins ambayo huleta mgusu wa hisia za raha wakati wa
kufanya tendo la ndoa.
Pia pilipili husisimua mfumo wa fahamu (nerves) wa ubongo na katika
kufanya hivyo huwezesha kuamshwa haraka kimapenzi (kunyegeka) wakati wa
tendo la ndoa na pia ukiguswa au kubusiwa au kunyonywa au kupapaswa
unapata hisia kila sehemu ya mwili.
2. MATUNDA NA MBOGA ZA MAJANI
Ulaji wa matunda na mboga za majani una matokeo makubwa sana katika hamu
ya tendo la ndoa kwa njia nyingi. Kwanza matunda na mboga za majani
hupunguza kiwango cha mafuta na unene (cholesterol). Kuongezeka kwa
mafuta mwilini huzuia mzunguko wa damu kwa kubana mishipa ya damu.
Pia kula matunda na mboga za majani huhakikisha balance ya uzito kwani
unene (obesity) kwa wanaume kuna matokeo mabaya katika kuzalisha homeni
za testoeterone na hatimaye jogoo kushindwa kuwika na kuwa na pia
mwanaume anakuwa na hisia za mapenzi (libido) kidogo.
Na pia wanandoa wanapozidi kunenepeana ndipo na hali ya kufurahia au
kuwa na hamu ya tendo la ndoa huzidi kupungua. Kitalaam inashauriwa kula
milo (potions) 3-5 za matunda kwa siku.
3. NAFAKA ZISIZOKOBOLEWA
Nafaka hasa zisizokobolewa kama mahindi, ngano, uwele, nk zina
nyuzinyuzi (fibre) na sukari ngumu (complex sugar) ambazo kusaidia
kutunza uzito wa mwili. Nafaka husaidia katika kuzalisha homoni za
testosterone kwenye damu. Na pia nafaka huwezesha mtu kuwa na nguvu
hatimaye kwenda masafa marefu wakati wa tendo.
Kula nafaka nzima kama vile brown bread badala ya white bread, pia kula
nafaka halisi badala ya cornflakes ni jambo zuri linalokuhakikisha afya
nejama na mahusiano mazuri ya ndoa yako.
4. TANGAWIZI
Tangawizi ni kiungo cha mboga ambacho husisimua sana na kusaidia mfumo
wa mzunguko wa damu mwilini. Tangawizi zinajulikana sana kwa kusukuma
damu kwenda sehemu za viungo vya uzazi yaani uke na uume hivyo kuwa na
umuhimu sana katika kuboresha ufanyaji wa tendo la ndoa. Inaweza kuliwa
mbichi, au kuliwa ikiwa imeungwa kwenye chakula au kusagwa na kuwa kama
unga na kutumiwa kama chai.
5. ASALI
Asali ina madini yanayoitwa boron, ambayo husaidia mwili kutumia homoni
ya estrogen ambayo ni homoni inayohusika na viungo ya uzazi na mapenzi
kwa mwanamke.
Pia kuna utafiti unaoonesha kwamba asali huongeza nguvu, kitendo ambacho
kitapelekea mwanamke kuwa uwezo na hamu ya tendo la ndoa au libido.
6. KARANGA
Karanga huhusika katika kuchochea mfumo wa mzunguko wa damu (vascular
system). Mzunguko wa damu ulio sawasawa katika uke na uume huwezesha
mwanaume na mwanamke kupata msisimko wa mapenzi haraka hatimaye tendo la
ndoa kuwa murua. Pia karanga zina madini muhimu kama vile magnesium,
asidi ya folic na zinc ambayo ni muhimu sana katika usalishaji wa mbegu
za mwanaume.
7. CHAZA (OYSTERS) NA PWEZA
Hawa ni aina ya samaki ambao hupatikana katika maji chumvi. Huwa na
kiasi kikubwa sana cha madini ya zinc na haya madini ndiyo huhusika
zaidi na uzalishaji wa homoni ya testosterone kwa wanaume.
Pia imethibitika kwamba wanaume wenye ukosefu wa madini ya zinc huwa na
matatizo ya nguvu za kiume. Pia madini mengi ya zinc mwilini huongeza
kiwango cha shahawa kwa wanaume.
8. SOYA
Pamoja na kuwa na kiwango kidogo sana cha mafuta (fat) na pia kuwa na
kiwango kizuri cha protein, soya zina phytoestrogens ambayo husaidia
sana wanawake ambao wamefikia menopause kutengeneza homoni estrogen ya
ziada.
Husaidia uke kuwa laini (wet, lubricated) mwanamke akisisimuliwa wakati wa tendo la ndoa.
9. CHOKOLETI
Chocolate ina phenylethylamine, kemikali ambayo husababisha hisia
(feelings) za furaha wakati wa mwanamke au mwanaume kufika kileleni
(orgasm). Inasaidia sana kula chocolate masaa machache kabla ya kuanza
kufanya tendo la ndoa.
10. PARACHICHI
Aina nyingine ya chakula ambacho husaidia kuongeza uwezo wa mtu kufanya
tendo la ndoa ni Parachichi. Tunda hili linauwezo mkubwa wa kuzalisha
vitamini E ambayo husaidia katika uzalishaji wa homoni. Inatajwa kuwa
watu wanaotumia tunda hili kwa wingi huwana msisimko mkali wa kimapenzi
na kwa upande wa wanawake husaidia kuongeza majimaji yenye utelezi
sehemu za siri na hivyo kuzuia uwezekano wa kuchubuka wakati wa
kujamiiana.
Jumanne, 25 Oktoba 2016
Home »
» Vyakula Vinavyoongeza Hamu na Nguvu ya Kufanya Tendo la Ndoa
0 comments:
Chapisha Maoni