Jamani Leo ni Siku ya saba tangia nikute chupi ya mke wangu chumbani kwa
 mdogo wangu wa kiume,nimekaa nalo moyoni naona niwashikirikishe 
wenzangu nione mnishauri nini
Ni hivi Ninaishi na mke wangu,mwaka wa NNE sasa,tuna mtoto mmoja,nina 
Mdogo wangu,anaishi hapa tangia January niliponunua bajaj ili awe 
anaendesha ili kusaidia wazazi wetu nyumbani kijijini,sasa jumapili 
iliyopita Wife aliwahi sana asubuhi kwenda kanisani pamoja na mtoto, 
Mimi nilibaki nimejilaza mpaka kama SAA moja na nusu Hivi, 
nilivyokumbuka kuwa nilikuwa na Ahadi Fulani, katika kufanya maandalizi 
sikiweza kuiona pass, so nikaenda straight chumbani kwa dogo katika 
kuitafuta ndo nilipo kutana na chupi ya mke wangu, ambayo Mimi mwenyewe 
nilimununulia so imechoka choka kiasi chake,nilishikwa na butwaa kwani 
namwani sana wife, dogo mwenyewe heshima kwa sana, nilichukua simu na 
kupiga picha kadha na kuzificha kwenye private vault, ile chupi 
nikaaicha palepale, wife hajasema chochote mpaka sasa, nawaza namna ya 
kuanza kumuulizia japo ameshahisi kuwa siko normal,coz nikimuona usoni 
nakuata hasira imepnada sana,kwa kifupi naogopa ukweli kuwa mke wangu 
amenisaliti kwa mdogo wangu,mpaka sasa simuoni kama mke wangu tena, 
namuona kama bundi kajificha chumbani kwangu, naomba mnishauri kwani 
Mimi kwa haraka haraka naona nimwite kaka yake aje amchukue kabla 
sijamfanya kitu mbaya, tatizo hasira zangu hupanda pole pole sana, 
kuzishusha ni kazi sana
Jumanne, 25 Oktoba 2016
Home »
 » Nimekuta Chupi ya Mke Wangu Chumbani Kwa Mdogo Wangu wa Kiume







0 comments:
Chapisha Maoni