NAIJUA familia ya mboga saba? Wengine wanapenda kuwaita watoto wa kishua
ama familia bora. Hii ikiwawakilisha watoto wanaozaliwa kwenye familia
yenye uwezo mkubwa wa kiuchumi, kiasi cha kutumia mlo mmoja ukiwa na
mboga tofauti na zinazobadilishwa kila uchao. Ndio, kuna familia
nyingine bhana mlo unakuwa na mboga moja na huwa ni hiyo hiyo deile
mpaka inachosha.
wee
Ingawa kuna dhana kuwa watoto wa kishua huwa wavivu kujitafutia kwa
sababu kila anachokotaka hukipata tu nyumbani, lakini ukweli sio wote.
Kuna wengine wanaamua kuchakarika kutafuta maisha yao wenyewe, hata
hawalingani na wale waliotokea familia za watu duni ambao walikatisha
masomo ili kusaka noti wakiwa kwenye umri mdogo kabisa.
Mwanaspoti inakuletea baadhi ya mastaa wa kike waliozaliwa kwenye
familia ya mboga saba, lakini wanakomaa kivyao vyao ile mbaya
wakijichanganya na wenzao kusaka noto kwa jasho na damu.
VANESSA MDEE
Vanessa Mdee maarufu kama Vee Money alizaliwa mjini Arusha mwaka 1988.
Vanessa anatokea familia bora ya Sammy Mdee ambaye kwa sasa ni marehemu.
Enzi za uhai wake, baba ya Mzee alikuwa mtu mzito kwenye nchi hii akiwa
mume wa Sophia.
Akiwa na umri mdogo Vanessa aliweza kusafiri nchi mbalimbali duniani.
Vanessa Mdee alikulia miji ya New York , Paris, Nairobi na Arusha,
lakini kwa sasa jamaa anatisha mbaya kwenye fani ya muziki akitamba
ndani na nje ya Afrika.
JOKATE MWENGELO
Huyu unaweza kumuita mtoto wa Oysterbay kwani ndio alipokulia huku baba yake akifanya kazi serikalini.
Kumbuka Jokate alizaliwa Washington DC, Marekani ambapo wazazi wake
walikua wakifanya kazi huko. Alipomaliza masomo ya juu ya Sekondari pale
Loyola ndipo alipoanza kujichanganya kwa kuwania taji la Miss Tanzania
mwaka 2006 na kushika nafasi ya 2 nyuma ya Wema Sepetu, kisha kuhamia
kwenye fani ya muziki, utangazaji, mitindo na ubunifu na sasa akipiga
fedha.
WEMA SEPETU
Wema Sepetu ni msichana anayetoka kwenye familia ya kibalozi akiwa ni
mtoto wa mwisho katika familia ya wasichana wanne wa marehemu Balozi
Isaac Sepetu.
Wema alizaliwa mwaka 1988 katika hospitali ya St. Andrew ya Dar es
Salaam na amesoma elimu yake ya awali mpaka sekondari kwenye Shule ya
Academic International iliyopo Dar es Salaam kabla ya kwenda Malaysia
kusomea mambo ya biashara za kimataifa katka Chuo Kikuu cha Limkokwing.
Alianzia shindano la urembo akitwaa mataji kadhaa ikiwamo la Miss
Tanzania 2006 kisha kuhamia kwenye filamu na sasa anaendelea kukimbiza
akimiliki kampuni yake na akizalisha bidhaa zenye jina lake. Achana
kabisa, ila ukiamua kubisha we bisha tu.
Jumanne, 25 Oktoba 2016
Home »
» Mastaa wa Kike Kutoka Familia za Mboga Saba Bongo
Mastaa wa Kike Kutoka Familia za Mboga Saba Bongo
Related Posts:
Model Maarufu Bongo Aibua Shutuma Nzito Kwenye Tasnia ya Mitindo..Adai Tasnia Imejaa Machoko ili Usonge Mbele ni Lazima Uwakaze Model wa Kiume Anayejulikana kama @calisah Huku Instagram Ameibuka na Tuhuma nzito iliyopo kwenye Tasnia hiyo ya Mitindo na Urembo ... Ameandika Haya Kwenye Ukurasa Wake wa Instagram: |Sikutaka kuandika chochote kuhusia… Read More
Soma Story ya Kusikitisha ya Huyu Dada, Mume Wake Anamlazimisha Kufanya Mapenzi ya Watu Watatu na Amegundua Kuwa ni Shoga Pia Kutoka Instagram: MMH DUNIA HII INA MAMBO KWAKWEL.COZZ LEO NIKO KI EMOTION ZAID EMBU NGOJA NI SHARE NA NYIE BAADHI YA STORY NAZO POKEA INBOX...kuna dada nilikuwa naongeaga nae ila kutokana na sababu zangu nisingependa m… Read More
LIVE TOKA BUNGENI: Rais Magufuli Ampa Hongera Zitto Kabwe Kwa Kutokuleta Fujo Bungeni na Kubakia Ndani ya Bunge Wakati Ukawa Wametoka LIVE TOKA BUNGENI:Muda huu Rais Magufuli Anatoa Hotuba yake ndani ya Bunge na Amempa Hongera Zitto Kabwe Kwa Kutokuleta Fujo Bungeni na Kubakia Ndani ya Bunge Wakati Ukawa Wametoka Baada ya Kutolewa na Spika kutokana … Read More
Maalim Seif azugumza na Balozi wa EU na viongozi wa UKAWA....Atoa Msimamo Mzito Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, amerejea kauli yake ya kutotambua kufutwa kwa uchaguzi mkuu wa Zanzibar uliofanyika tarehe 25 mwezi uliopita. Akizungumza na waandishi wa habari jijin… Read More
JE Unakichukuliaje Kitendo cha ZITTO KABWE Kubaki Bungeni Wakati Wabunge wa Upinzani Wote Wametoka Nje ? JE Unakichukuliaje Kitendo cha ZITTO KABWE Kubaki Bungeni Wakati Wabunge wa Upinzani Wote Wametoka Nje Kushinikiza Maalim Seif Atangazwe Mshindi wa Urais Zanzibar? TOA MAONI YAKO … Read More
0 comments:
Chapisha Maoni