Katika hali isiyo ya kawaida mama mmoja mwenyeji wa mkoa huu wa mbeya 
mji mdogo wa mbalizi, usiku wa kuamkia leo alienda kaburini alikokua 
kafukiwa mwanae aliyefariki dunia Siku ya jumatatu na kuzikwa jumanne ya
 wiki Hii na kufukua kaburi hilo na kuitoa maiti 
Kwa mujibu wa mama huyo maarufu Kama mama vumi anadai aliambiwa na 
mchungaji kuwa mwanae hajafa Bali Kuna sehemu anafanya kazi hivo aende 
akaitoe ile maiti kaburini ili iombewe irudi kuwa binadam wa kawaida,
Jana usiku yule mama ndio akaenda kuifanya kazi aliyotumwa na mchungaji 
wake ambapo leo asubuhi ndio raia wakagundua ishu na kwenda kukinukisha 
kwa yule mama, polisi walifika eneo la tukio na kumuokoa yule mama toka 
kwenye mikono ya wananchi wenye hasira Kali na kuondoka nae pamoja na 
maiti ya mtoto







 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
0 comments:
Chapisha Maoni