Ijumaa, 9 Juni 2017

Kajala Aibuka na Haya Kuhusu Wema Sepetu..Adai Hata Mwanae ni Shahidi..!!!



TASNIA ya filamu nchini imepambwa na wasanii wa kike wenye urembo unaovutia macho na hakika kwenye orodha ya waingizaji wenye kipaji, uwezo na mvuto huwezi kumuacha, Kajala Masanja.

Huyu ndiyo bosi wa kampuni ya Kajala Entertment,  ambayo imetengeneza filamu nyingi ikiwemo ile ya Sikitu ambayo chini ya mpicha Farid Uwezo iliweza kufanikiwa  kuliteka soko hilo la filamu.


Juma3tata wiki hii lipo na mrembo huyu, mpenzi wa chakula aina ya ndizi na samaki sato ambapo amefunguka mambo kadha wa kadha yanayohusu maisha yake ya ustaa na yale ya kawaida.

MKASA WA JELA WAMFUNZA

“Nina mfano halisi kabisa katika maisha na nitahakikisha namfunza mwanangu Paula asije akakutana na mkasa ulionikuta mimi na kufanya niingie jela kwa kuwa nilimsapoti mtu hata kwa yale yasiyostahili kisa nilikuwa nampenda,” alisema Kajala.

HATAKI KUFANYA TENA KOSA

Kajala amezidi kulifahamisha Juma3tata kuwa hapendi kulikumbuka tukio lile lililomfanya akae jela kwa muda wa mwaka mmoja na kumwacha mtoto wake kwenye wakati mgumu na hataki tena kufanya uzembe uliosababisha kosa lile.

 “Naweza sema ni uzembe ambao nilijitakia mwenyewe,  kumwamini mtu wakati kabisa najua ananiingiza shimoni ni kitu ambacho hakitafutika maishani mwangu, sitafanya kosa tena” anasema Kajala.

AWAONYA WAREMBO WENGINE

“Nataka wasichana wenzangu wajifunze kupitia mimi yaani hata kama unampenda mtu, usikubali akushawishi uvunje sheria za nje, jitahidi ujinasue kwani mwisho wake ni mbaya sana,” anasema.

HATASAHAU HURUMA YA WEMA SEPETU

Mara baada ya kuhukumiwa kifungo cha miaka 7 au faini ya shilingi milioni zaidi ya kumi, Kajala na ndugu zake  waliingiwa na hofu kwani fedha hiyo ilikuwa ni kubwa kwao na hapo ndipo Wema Sepetu alipoibuka shujaa.

“Kama asingekuwa Wema Sepetu kunilipia zile  pesa sijui sasa hivi ningekuwa wapi, kwani hata ndugu zangu walichanganyikiwa kusikia kiasi kikubwa kile cha fedha ila moyo wa huruma wa Madame ulisababisha nitoke, siachi kumwombea katika sala zangu mwanangu pia analijua hilo,” anasema Kajala.

AZIPONDA TIMU MTANDAONI

Aidha aliweka wazi kusikitishwa timu katika mitandao ya kijamii zinazoibua maneno ya kuchochea ugomvi kati yake na Wema kitu kinachomuumiza kwani kwake ni mtu wa thamani mno.

KUFA KWA SOKO LA FILAMU

Katika hatua nyingine  mrembo huyo  alizungumzia anguko la filamu huku akikanusha taarifa hizo kwa kuwa wasanii wa bongo bado wanapiga kazi huku wengine wakishirikishwa na wasanii wa mataifa mengine.

“Kama soko la filamu limekufa basi wasanii wasingepata kazi za nje, sasa hivi wasanii tunaitwa kufanya filamu nchi za nje kwa malipo mazuri, tamthilia zetu pia zinaruka kwenye ving’amuzi mbalimbali, nchi nyingi zinazojifunza Kiswahili zinategemea filamu zetu kwa hiyo tunazidi kuvuka mipaka na kufanya vizuri,” anasema Kajala.

AWACHANA WASAMBAZAJI

Kajala amewataka wasambazaji kuwalipa wasanii kwa wakati mara wanapowekeana saini mikataba ya kusambaza filamu zao na siyo kuwalipa wasanii kwa awamu kitu kinachowafilisi wasanii.

 “Wasambazaji wa Kihindi waache  kutuzungusha kwenye malipo, kingine waache kubagua wasanii, waache kuangalia staa gani yupo ndani ya filamu ndiyo wanunue, waangalie ubora wa kazi na siyo sura,” anasema.

ANAAMINI KWA WASANII WACHANGA

Staa huyu wa filamu amesema anaamini katika vipaji vya wasanii wachanga, anaamini kuna kazi nzuri zinatengenezwa na wasanii wachanga lakinni wasambazaji huzikataa kwa sababu hawana ustaa.

0 comments:

Chapisha Maoni