Ijumaa, 9 Juni 2017

Vita Ya Malipo Kiduchu Haijawahi Kumuacha Modo Salama!


Amber Lulu
AMANDA Swartbooi moja kati ya wauza nyago katika video Afrika akitokea Afrika Kusini. Amanda ametokea kujizolea umaarufu kwa kipindi kifupi cha mwaka jana ambapo ametokea katika video kadhaa Afrika ikiwemo Coolest Kid ya Davido akimshirikisha Nasty C wa Afrika Kusini, Four4 ya JR pamoja na Show Me ya Rich Mavoko akiwa na Harmonize.

Licha ya kufanya poa huko, ameshawahi kukiri kuwa kuuza nyago katika video hizo kunamlipa kwani kumempa mafanikio ya kujisomesha katika Chuo Kikuu cha Afrika Kusini (UNISA) akiwa mwaka wa pili katika masomo ya biashara. Ukija Bongo wapo wauza nyago katika Video za Kibongo ambao ni ‘visu’ lakini wanaangushwa na malipo kiduchu kutoka kwa wasanii husika kiasi cha kufikia kuangalia kazi nyingine za kufanya huku baadhi wakijiingiza katika muziki.
Agness Masogange


Katika makala haya nimekuchambulia baadhi tu ya wauza nyago (modo)ambao vita hii ya malipo kiduchu haijawahi kuwaacha salama kwani wengine wameamua kuachana na kuuza sura na wengine kujiingiza katika kuimba.

Alikuja kwa kasi, akavuma katika Video ya Kwetu ya Rayvanny na baada ya hapo akatokomea. Kutokana na kuitendea haki video hiyo, wengi walimtabiri kama miongoni mwa wauza nyago watakaokuja kuliteka soko. Hajashiriki tena katika kuuza sura kwenye video nyingine hadi sasa huku ikisemekana kukwepa malipo kiduchu kwa kila anayemfuata kufanyanaye kazi.


Alianza kuuza sura katika Video ya Naogopa ya Mirror kisha katika Remix ya Burger Movie Selfie ya Belle9 na baada ya hapo aliamua kuachana na suala la kuuza nyago na kujiingiza rasmi kwenye Muziki wa Bongo Fleva. Lulu anasema malipo kiduchu na mastaa wengine wakitaka kumtumia bure katika video zao ndivyo vilivyomkimbiza kwenye kuuza sura na kuamua kuimba ambapo kwa sasa anabamba na Ngoma ya Usimuache.

lulu Diva
Ni modo ambaye pia muuza nyago katika video za Kibongo. Kutokana na malipo kiduchu katika video hizo kumemfanya kupotea kimyakimya katika orodha wauza sura Bongo. Ameshawahi kukiri kulipwa kiasi kikubwa katika video moja tu (Salome ya Diamond) tangu aingie katika kuuza nyago huku akiwa na kumbukumbu ya kulipwa kiduchu katika Video ya Magubegube ya Barnaba.
Gigy Money



Naye ni miongoni mwa wauza nyago walioanza kupotea kwenye ramani ya muziki Bongo kisa hazilipi. Alianza kutokea katika Video ya Masogange ya Belle9 na baada ya hapo akaonekana kwenye Video ya Magubegube ya Barnaba iliyotoka 2012. Mara ya mwisho kuonekana katika ulimwengu wa wauza nyago ilikuwa katika Video ya Msambinungwa ya Tunda Man akishirikiana na Ali Kiba iliyotoka mwanzoni mwa mwaka 2014.

0 comments:

Chapisha Maoni