Jumanne, 4 Julai 2017
Home »
» NILIIBIWA sana Facebook – Mch Anthony Lusekelo Afunguka
NILIIBIWA sana Facebook – Mch Anthony Lusekelo Afunguka
Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC), Anthony Lusekelo maarufu kama ‘Mzee wa Upako’ amefunguka kuwa yeye ni moja ya Wachungaji ambao wapo nyuma sana kwenye mitandao ya kijamii na kukiri kuwahi kuibiwa kwenye mtandao wa Facebook na watu wanaotumia jina lake.
Mzee wa Upako amesema kutokana na kuwa na elimu ndogo ya mitandao ya kijamii amewahi kuibiwa na watu mitandaoni waliokuwa wanawatapeli waumini wake kwa kutumia jina lake na kuwaomba watu hela.
“Nina akaunti ya Instagram na nimewafuata watu wanne tuu Magufuli, Jakaya, BBC na vyombo vingine vya habari….(kuhusu Facebook) kule niliibiwa sana kuna watu walikuwa wanatumia jina langu wanajiita Mzee wa Upako na kuwachangisha watu pesa,” amesema Mch. Antony Lusekelo kwenye mahojiano yake na kipindi cha Chomoza cha Clouds TV.
Hata hivyo Mzee wa Upako amesema kwa sasa kwenye simu yake hakuna hata Group moja la WhatsApp huku akidai kuwa wingi wa simu za kawaida zinazoingia ndiyo unamfanya asijiunge na makundi hayo kwani yanamaliza chaji
Related Posts:
Taarifa ya Kikao cha Kamati Ndogo ya Kamati Kuu cha Dharura cha CHADEMA...!!! CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA) TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI JUU YA MAAZIMIO YA KIKAO CHA KAMATI NDOGO YA KAMATI KUU 1.0 UTANGULIZI Kikao cha Kamati Ndogo ya Kamati Kuu cha dharura kilichoketi ta… Read More
Baada ya Kumuita Nyani, Iyobo Amvaa Tena Harmorapa...!!!! KIONGOZI wa madansa ambaye ni dansa tegemezi wa Wasafi Classic Baby (WCB) Mose Iyobo amefunguka kuwa yeye hana imani na Harmorapa na anashangaa anavyotajwa kila mahali kwani yeye hajawahi kusikia kazi yake yoyote hi… Read More
MSUMBIJI: Mwanamke wa Kitanzania Abakwa Mpaka Kufa. Serikali Imefungwa Pasta? Jamani, Hii inasikitisha sana tangu kuanza kusikika kwa sakata la watanzania kufurushwa uko msumbiji mengi yametokea lakini serikali yetu inaonesha kuwakandamiza watanzania kuwaonesha hawakuwa wakiish kihalali kabis… Read More
Yaliyojiri Mahakamani Kisutu Kesi ya Masogange..!!!! KIMUHEMUHE kilitanda kwenye viunga vya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Feb 17, 2017, kufuatia ndugu, jamaa na marafiki wa model, Agness Masogange kufurika huku wakitarajia kumuona ndugu yao huyo akifikishwa … Read More
Uwoya ni Gusa Unate..!!!! Msanii maarufu wa filamu Bongo, Irene Uwoya (pichani) anatajwa kuwa kati ya mastaa wa kike Bongo aliyewahi kutoka na mastaa na vigogo mbalimbali huku ikidaiwa kuwa, kila aliyekuwa naye alimuacha yeye na si kua… Read More
0 comments:
Chapisha Maoni