Jumamosi, 30 Agosti 2014

Baada ya Okwi kutangaza kujiunga na Simba,hiki ndicho walichokifanya Yanga.

Ikiwa imepita siku moja toka klabu ya Simba kumtangaza Emmanuel Okwi kama mchezaji wao rasmi wa klabu hiyo,taarifa nyingine iliyotolewa leo na uongozi wa Yanga ni kumshitaki Okwi. Klabu ya Young Africans imemshitaki Emmanuel Okwi kwenye Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na kuwasilisha nakala kwa shirikisho la soka Barani Afrika (CAF) na shirikisho la soka duniani (FIFA)...

Je Toni Kroos ndio kamkimbiza Alonso Madrid? Xab Alonso ajibu.

Kiungo wa kimataifa wa Spain  Xabi Alonso amejiunga na klabu ya FC Bayern Munich ya Ujerumani akitokea kwa mabingwa wa ulaya Real Madrid kwa ada ya uhamisho wa paundi millioni 5. Alonso ambaye alijunga na Real Madrid akitokea Liverpool ametambulishwa rasmi leo hii kwenye mkutano waandishi wa habari na kutoa sababu ambayo imemfanya mpaka akaamua kuondoka Santiago...

HATIMA YA TORRES CHELSEA;HIKI NDICHO ALICHOKISEMA

Fernando Torres amemaliza kipindi kigumu kabisa cha miaka mitatu na nusu kwenye maisha yake ndani ya klabu ya Chelsea baada ya kukubali kuondoka katika timu hiyo. Fernando alijiunga na Chelsea mnamo mwaka 2011 January kwa ada ya uhamisho ambayo ilivunja rekodi ya usajili nchini Uingereza – £50m akitokea Liverpool – leo hii imethibitishwa rasmi kwamba mchezaji huyo sasa...

Na hii ni nyingine tena! Wasanii walioandamana nusu uchi Nairobi Kenya.

  Siku hizi ishu ya kuvua nguo kuonyesha msisitizo au kulipigia kelele jambo flani imekua kawaida, yani wengi wameitumia hii njia kufikisha malalamiko yao na mfano mzuri ni hivi karibuni kwa Wanafunzi wa kike kwenye shule ya sekondari ya Wasichana Tabora Tanzania kubaki nusu uchi kwa nia ya kupigia kelele matatizo ya shule ikiwemo maji. Nchi jirani ya Kenya matukio...

Alhamisi, 21 Agosti 2014

VIONGOZI WATUMIA MADARAKA YAO KUJINUFAISHA

Mstaafu wa Awamu ya Pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi (katikati) akifungua semina ya majadiliano kati ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma na wanahabari waliojadili rasimu ya Sheria Mpya ya Kudhibiti Mgongano wa Maslahi kwa Viongozi wa umma. Mstaafu wa Awamu ya Pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi akifungua semina ya majadiliano kati ya Sekretarieti ya Maadili...

RATIBA LIGI KUU BARA 2014/2015 HII HAPA

Kocha mkuu wa Simba sc Patrick Phiri akiongea na wachezaji wake Kocha mkuu wa Yanga akiongea na msaidizi wake Baraka Mpenja, Dar es salaam RATIBA ya ligi...

Israel na Hamas waendelea na mapigano

Mgogoro kati ya Israel na Palestina unaendelea. Pande zote mbili zimekuwa zikishambuliana kwa maroketi. Wakati huo huo, Misri inataka mazungumzo ya kuleta amani yaanze tena. Hali ya wasiwasi imerejea tena kwa wakaazi wa Israel na ukanda wa Gaza. Awali Israel na Hamas walikubaliana kuendeleza muda wa kusitisha mapigano. Lakini makubaliano hayo hayakuheshimiwa....

Waandamanaji wataka Nawaz Sharif ajiuzulu

Waandamanaji wanopinga serikali nje ya bunge la Pakistan, hawaonyeshi ishara yoyote ya kuondoka,hadi pale waziri mkuu Nawaz Sharif atakapojiuzulu, dai ambalo serikali imekataa kwa misingi ya kuwai kinyume na katiba. Wakati huo, huo jeshi lenye nguvu la Pakistan limeonya pande zote kutatua mzozo wao kupitia majadiliano. Maelfu ya waandamanaji wanopinga...

Taarifa ya Jeshi la Polisi kuhusu ajali iliyotokea Tabora Aug 19.

Taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora ambayo ameitoa leo kwa Waandishi wa habari ni kuhusu ajali ambayo ilitokea jana Aug 19 majira ya saa 9 alasiri ambayo ilihusisha mabasi mawili. Mabasi hayo ni AM Coach na Sabena ambapo chanzo cha ajali hiyo kimedaiwa kuwa ni mwendo kasi wa mabasi hayo,majeruhi wamelazwa kwenye hosptali ya rufaa ya mkoa wa Tabora Kitete...

WATU 32 WAMEFARIKI KWENYE MAPOROMOKO YA ARDHI

Watu  32 wamefariki katika maporomoko ya ardhi(landslide) katika mkoa wa Hiroshima nchini Japan.Maporomoko hayo yamesababishwa na mvua kubwa zilizonyesha kwa saa 24 kuamkia Jumatano asubuhi zikiwa sawa na kipimo cha mvua za mwezi mzima imesema mamlaka ya hali ya hewa ya Japan. Picha kutoka eneo la tukio zimeonyesha nyumba zikiwa zimefukiwa katika matope na miamba...

Mfanyakazi wa benki afikishwa mahakamani kwa kuiba pesa za abiria walipotea na Malaysia airline

Mwanamke mmoja mwenye cheo cha juu katika bank kubwa iliyopo Kuala Lumpur Malaysia pamoja na mumewe wameshtakiwa kwa kuiba pesa kutoka katika account za abiria na wafanyakazi wa ndege ya Malaysia iliyopotea kwenye bahari ya hindi. Pamoja na kushtakiwa huko mtu na mkewe hao waliepuka makosa mengine 16 kati ya makosa hayo yamo wizi,kukaidi amri ya mahakama na makosa mengineyo. Ofisa...

Uliipata hii ya Wanafunzi Kenya kupelekwa Mahakamani baada ya kukutwa wamelewa?

  Sio kitu kigeni kuona watu wenye umri zaidi ya miaka 18 wanakunywa Pombe wanalewa na hata pombe hiyo kugharimu maisha yao ila sio kawaida kukutana ama kuona mtoto wa miaka kati ya 14-17 ni mlevi wa kupindukia na mtumiaji pia wa dawa za kulevya. Ripoti mpya iliyotolewa na Mamlaka ya kudhibiti vileo nchini Kenya (NACADA) inaonyesha kwamba ni watoto zaidi ya...

Jumanne, 5 Agosti 2014

Umeipata hii ya Weusi kusemekana wamecopy wimbo?

Kupitia You heard ya August 04,Weusi wamesemekana kucopy wimbo na kuurudia kuanzia namna wanavyorap mpaka beat iliyotumika kwenye wimbo huo,Joh Makini kaongea na kapatikana pia producer wa wimbo huo NahReel nae kazungumza. 88.0 Clouds Fm inasikika ukiwa Tabora. Bonyeza play kusikiliz...

Sina muda kujadili upuuzi huu kuhusu Ridhiwani – Rais Jakaya Kikwete

Taarifa kutoka ofisi ya Rais kuhusu maneno yanayosemekana kwamba Rais Jakaya Kikwete kushiriki kusaidia kumwokoa mwanae ambaye ni mbunge wa jimbo la Chalinze Mheshimiwa Ridhiwani Kikwete baada ya kukwamatwa na dawa za kulevya nchini China. Hii ni taarifa kutoka ofisi ya Rais yenye maneno ya Rais Jakaya Kikwete. ...

Magazine yamuomba msamaha 2 Face Idibia baada ya kesi ya Naila milioni 100.

Icon Weekly magazine walitoa habari kwamba 2 Face Idibia ametoka nje ya ndoa yake na kuanzisha uhusiano na mfanyakazi wa benki. Magazine hiyo haikuishia hapo iliendelea kusema kwamba 2 face amempa ujauzito mwanamke huyo. Habari hiyo ilimchafua 2 face kwasababu yupo ndani ya ndoa na ndio ilikuwa habari kubwa ya magazine kwa kuwekwa mbele ya cover. Baada ya magazine...

Yaliyoikuta Yanga Kagame Cup baada ya kupeleka kikosi cha Pili

Baada ya jana usiku katibu mkuu wa Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) Nicholas Musonye kutoa onyo kwa Yanga kuwasilisha majina mapya ya wachezaji wa kikosi cha kwanza kwa ajili ya Kagame Cup, leo hii CECAFA wametoa uamuzi mpya dhidi ya Yanga. Yanga SC sasa rasmi imeondolewa kwenye michuano ya Kagame kutokana na Baraza la Vyama vya Soka Afrika...