Kamishna-Generali wa Magereza nchini Kenya
Isaiah Osugo amekataa ombi la wafungwa kuruhusiwa kufanya tendo la ndoa
na wake zao wakiwa gerezani.
Katika mazungumzo ya kipekee na BBC
Swahili, Osugo amesema hili ni jambo ambalo linahitaji kuwepo vyumba vya
faragha kuwaruhusu na yote haya yanahitaji pesa nyingi.Mara kwa mara baadhi ya wafungwa nchini Kenya hasa wale ambao wamefungwa maisha na wale wlaiofungwa kwa miaka mingi wametoa ombi kwa serikali waruhusiwe kufanya tendo la ndoa na wake zao.
Wengi wao wanadai kuwa wakitoka jela na hupata wake zao wametoroka na hivyo basi ndoa zao kusambaratika.
Lakini Osuogo amesema hilo kwa sasa sio jambo la muhimu kwao.
"kwa sasa hatuna nyumba ya kumpa mfungwa starehe kama hii. Tuna vyumba ambavyo wafungwa wanalala wawili, wengine watatu na kuna wale wanalala kama hamsini kwa chumba kikubwa kabisa, na tunazidi kujenga ili tuwape nafasi ya kutosha,'' anasema Osugo.
"Hatujafikia hapo bado, kama mtu anataka hiyo strarehe ni vizuri ajizuie kufanya makosa asiletwe jela kwa sababu akiwa ndani ajue hapa ni mahali pa kumrekebisha.''
Na je barani Afrika kuna nchi ambayo inaruhusu jambo hili?
"Nilisikia Afrika Kusini walijaribu lakini sijui kama walifanikiwa. Unajua tena hao wana wafungwa wachache lakini sidhani kama nchi yoyote ya Afrika inawapa wafungwa ruhusa ya kuonana na mabibi wao kwa starehe kama hizo.''
Osugo anasema tofauti na baadhi ya mataifa ya ulaya ambayo yanawapa wafungwa nafasi hii, Afrika bado iko mbali sana kwa mambo kama haya.
"Nchi kama Canada wanaruhusu wafungwa saa 72 kuonana na wapenzi wao kwenye nyumba nzuri ambazo ziko ndani ya jela. Hapa sisi hatuwezi. Na tukianza hivyo si wafungwa wote watataka.''
Osugo anasema kwa hivi sasa wana mambo mengi mhimu ya kutekeleza, na endapo ombi hili la wafungwa litatekelezwa basi litakua la mwisho kabisa kufanyika lakini hajasema ni lini Kenya itaweza kuwaruhusu wafungwa kujamiIana na wake Zao.
Ombi hili ni la wafungwa wa kiume hapa Kenya lakini kwa upande wa wafungwa wanawake ni nadra sana watoe ombi kama hili.
0 comments:
Chapisha Maoni