Jumatano, 17 Septemba 2014
Home »
» Sentensi 4 kwanini maandamano ya CHADEMA Dodoma kesho yamezuiliwa.
Sentensi 4 kwanini maandamano ya CHADEMA Dodoma kesho yamezuiliwa.
Polisi Dodoma wametangaza kuyazuia maandamano ya chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA yaliyokua yamepangwa kufanyika Alhamisi ya tarehe 18/09/2014 ambapo wametaka Wananchi wayapuuze.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi wa Polisi Emmanuel Lukula amesema kufuatia viongozi wa CHADEMA kutaka kufanya maandamano kuelekea viwanja vya ofisi za bunge kwa ajili ya kupinga bunge la katiba linaloendelea, maandamano hayo ni batili na yanakiuka Sheria iliyoliwekwa kwa bunge hilo.
Ripoti ya Polisi iliyosambazwa Septembet 17 2014 inasema Kamanda Lukula ametaja sababu za msingi za kuzuia maandamano haya kuwa ni:- 1 . siku ya maandamano ya tarehe 18/09/2014 ni siku ya kazi kwa sababu yalipangwa kufanyika kuanzia saa nne asubuhi mpaka saa sita mchana hivyo yataathiri ufanisi wa watu waliopo makazini/maofisini.
2. Bunge maalumu la Katiba linaloendelea kwa sasa lipo kisheria na hakuna tamko lolote lililotolewa na Mahakama yoyote kulisitisha hivyo moja ya kazi ya jeshi la polisi ni kulinda sheria na wale wanaofuata sheria.
Kuna kesi Mahakamani ya kupinga Bunge hilo kuendelea na hadi sasa shauri hilo linaendelea Mahakamani hivyo kwa CHADEMA kuandamana ni kuingilia Uhuru wa Mahakama.
Baadhi ya wilaya barua za kufanya maandamano zimechelewa kufika kwa wakuu wa polisi wilaya kabla ya saa 24 kisheria hivyo Kamanda Lukula amesisitiza kuwa CHADEMA Mkoa na Wilaya za Dodoma wayasitishe maandamano na kama hawajaridhika wakakate rufaa kwa waziri wa mambo ya ndani ya nchi.
0 comments:
Chapisha Maoni