Alikiba ametolea ufafanuzi post yake ya Instagram iliyozua mjadala kwa
mashabiki mbalimbali wa muziki ambao waliipokea kwa hisia tofauti.
Siku ya Jumatatu Nov.16 Muimbaji huyo wa single mpya ‘Nagharamia’ aliandika, “Asanteni
sana najua mmepiga kura sana lakini nilikuja kugundua baada ya
kufuatilia kuwa kuna mambo yanaendelea ya watu wanadiriki hata kupoteza
pesa zao kwaajili yangu ila nawaomba fans msinielewe vibaya I will
always be there for you #hapakazitu #kingkiba,” post ambayo baadae aliifuta.
Kupitia kipindi cha Ala Za Roho cha Clouds Fm na Diva The Bawse, king
Kiba amesema kuwa watu walimuelewa vibaya kwenye post hiyo na ndio
sababu kubwa ya kuamua kuifuta,
“watu walinielewa vibaya mimi nilikua
nawaambia mafans wangu, sababu wao ndo wananipigia Kura mimi
sikumaanisha kuhusu tuzo walinielewa vibaya” alisema Kiba.
Hata hivyo licha ya kwamba yeye hakushinda kipengele hata kimoja kati ya
vinne alivyotajwa kuwania kwenye tuzo za AFRIMA 2015, lakini
hakumpongeza hata msanii mmoja wa Tanzania aliyeshinda ambao ni Diamond
na Vanessa Mdee. Kusuhu hilo Alikiba alisema,
“Siwezi ku-post kitu kuhusu Kushinda Kwao,
unajua hakuna uzalendo. watu wangapi wanafanya Vitu vizuri hawapongezwi?
Mimi nafanya vingapi? Sisi sio wazalendo…Unajua watu mimi hawanijui
Wanahisi kama mimi nina ringa hivi au nina wivu, ila mimi nawapenda
wasanii wote pia mziki mzuri” alisema Alikiba.
Alipoulizwa kuhusu uhusiano wake na Diamond ukoje kwa sasa, ndipo alimpongeza Platnumz kwa ushindi wa tuzo 3.
“Mimi sina tatizo na Diamond, nasikia kashida
tuzo 3, nampongeza Sana sababu tumepata mtu ambaye anatutambulisha
kimataifa ni Kitu poa Sana…Mimi na Diamond we are good” alimaliza Alikiba.
Ijumaa, 20 Novemba 2015
Home »
» Alikiba Atolea Ufafanuzi Post ya ‘Utata’ Aliyoandika Instagram, na Ampongeza Diamond Kwa Ushindi wa AFRIMA
Alikiba Atolea Ufafanuzi Post ya ‘Utata’ Aliyoandika Instagram, na Ampongeza Diamond Kwa Ushindi wa AFRIMA
Related Posts:
KAMPUNI YA TTCL YATWAA TUZO YA MAONESHO YA BIASHARA SABASABA Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya TTCL wanaoshiriki Maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa wakipiga picha ya pamoja na tuzo yao mara baada ya kutwaa tuzo hiyo. Muonekano wa Banda la TTCL kwenye Maonesho ya 38 ya Biasha… Read More
MAMBO YA SABASABA JIJINI DAR ES SALAAM Muonekano wa lango kuu la kuingia ndani ya banda la Makampuni ya MeTL Group kwenye maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar-es-salaam yaliyozinduliwa rasmi jana kwa kupewa baraka na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar … Read More
AJARI YA GARI MAENEO YA POSTA IRINGA Ni ajali ambayo imehusisha gari mbili aina ya Suzuki Carry na Toyota inayomilikiwa na Asas, hata hivyo hakuna aliyejeruhiwa kwenye ajali hiyo.… Read More
MFARANSA AJA TANZANIA KUONYESHA UMAHIRI WA KUCHEZA MPIRA WA MTAANI Mwanamichezo kutoka nchini Ufaransa Sean Garnier (katikati) ambaye yuko nchini Tanzania kwa ziara maalum ya kimichezo akifafanua machache mbele ya waandishi wa habari mara baada ya kutambulishwa. Pembeni yake kulia ni Menej… Read More
MBUNGE APIGWA RISASI MOGADISHU Kundi la al-shabab limesema limempiga risasi na kumuua mbunge mmoja maarufu mjini Mogadishu. Ahmed Mohamud Hayd aliuawa na watu waliokua ndani ya gari, wakati akitoka hoteli aliyofikia katika eneo linalolindwa vikali,… Read More
0 comments:
Chapisha Maoni