Baada ya kusambaa kwa taarifa kwenye
mitandao zikieleza kuwa kampuni ya Home Shopping Centre imefunga maduka
yake kutokana na kukwepa kodi na kuhusika kwenye sakata la makontena
yaliyopotea bandarini, uongozi wa kampuni hiyo umejitokeza na kupinga
taarifa hizo.
Kupitia taarifa yake kwa vyombo vya
habari, kampuni hiyo imeeleza kuwa habari hizo sio za kweli na kueleza
kuwa haijawahi kukwepa kodi na haihusiki kwa namna yoyote na makontena
yaliyopotea bandarini.
“Home Shopping Centre Co. Limited
haihusiki kabisa kwa njia yoyote ile na wizi, ukwepaji kodi, au potevu
wa makontena 349 na yale zaidi ya 2431 yaliyoibuliwa na Mheshimiwa
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na kamwe haijawahi kujihusisha na uhalifu
huo wa kuiba makontena na kukwepa kodi,” ilieleza taarifa hiyo
iliyosainiwa na Mfilisi wa kampuni hiyo, Yusufu Mohamed.
Mohamed alieleza kuwa kampuni hiyo ilifunga maduka yake kama ambavyo makampuni mengine hufanya na sio vinginevyo.
0 comments:
Chapisha Maoni