Saa chache baada ya rais Magufuli 
kutangaza baraza lake la Mawaziri ambalo limekuwa baraza dogo kama 
alivyoahidi, aliyekuwa mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) na mbunge 
wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu wamekosoa uteuzi wa Profesa 
Sospeter Muhongo na Dk. Harison Mwakyembe.
Dk. Mwakyembe alikuwa waziri wa Uchukuzi
 katika serikali ya awamu ya nne na hivi sasa ameteuliwa kuwa waziri wa 
Katiba na Sheria. Profesa Muhongo ambaye alijiuzulu kwa kashfa ya Escrow
 katika serikali ya awamu ya nne, amerudishwa katika wizara ya Nishati 
na Madini.
Profesa Lipumba amekosoa uteuzi wa profesa Muhongo kwa madai kuwa uteuzi wake umelitia doa baraza hilo.
“Kwa kitendo kama hiki, Rais Magufuli 
amejiwekea dosari kutokana na uteuzi huu. Maana yake ni kuwa katika 
kashfa ile Profesa Muhongo hakuwa na hatia,” Profesa Lipumba aliliambia 
gazeti la Mwananchi.
Profesa Lipumba aliongeza kuwa wananchi 
watapata ugumu kumuelewa Rais kutokana na ahadi zake kuwa atapambana na 
rushwa na ufisadi.
Naye Tundu Lissu aliliambia gazeti hilo 
kuwa uteuzi wa Dk. Harison Mwakyembe hakuwa sahihi kwa kuwa ndiye 
aliyekuwa waziri wa Uchukuzi na punde baada ya rais Magufuli kuingia 
ikulu, Mamlaka ya Bandari ikabainika kukumbwa na kashfa ya upotevu wa 
makontena.
“Juzi Rais Magufuli aliufumua uongozi wa
 Bandari ya Dar es Salaam kutokana na kashfa, miongoni mwa waziri 
waliokuwa wakisimamia sekta hiyo ni Dk. Harrison Mwakyembe, eti leo 
amemrudhisha kundini?” Lissu ananukuliwa.
Lissu aliongeza kuwa Muhongo pia hakufaa kuwa miongoni mwa mawaziri kwa kuwa alifukuzwa na Bunge kutokana na sakata la Escrow.
Hata hivyo, Profesa Lipumba alimpongeza rais kwa kutekeleza ahadi yake ya kuunda baraza dogo kwa lengo la kubana matumizi.
Ijumaa, 11 Desemba 2015
Home »
 »  Profesa Lipumba, Lissu wapinga uteuzi wa Muhongo na Mwakyembe







0 comments:
Chapisha Maoni