Mpinzani mkuu wa Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, Dk. Kizza Besigye ambaye amekuwa akipinga ushindi wa Rais huyo, amekamatwa na polisi wa nchi hiyo baada ya jana kujiapisha kuwa Rais ikiwa ni siku moja tu (leo) kabla ya Museven kuapishwa.
Haijulikani ni vipi Dr Kiiza Besigye alikwepa vizuizi vya polisi na kuibukia mjini Kampala ambapo alikutana na wandani wa chama chake na ''kula kiapo cha urais wa taifa hilo''.
Katika video inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii Dr Besigye anaonekana ''akila kiapo'' mbele ya mtu aliyevalia mavazi sawa na ya ''jaji wa mahakama ya juu''.
Video hiyo ilisambazwa kwa kasi kwenye mitandao ya kijamii na kusababisha mamlaka inayosimamia mawasiliano nchini Uganda kuamrisha kampuni zinazotoa huduma za simu nchini humo kufunga huduma za mitandao ya kijamii
Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilimtangaza Yoweri Museveni kuwa mshindi katika uchaguzi mkuu uliopita akiwaacha kwa mbali wapinzani wake wakuu, Kizza Besigye na Amama Mbabazi.
Kadhalika, Mahakama Kuu nchini humo ilihalalisha ushindi wa Museveni baada ya kutupilia mbali shauri la pingamizi la ushindi huo lililowasilishwa na Amama Mbabazi.
Alhamisi, 12 Mei 2016
Home »
» Mpinzani wa Museveni , Dr Kiiza Besigye Akamatwa Baada ya Kujiapisha Kuwa Rais
Mpinzani wa Museveni , Dr Kiiza Besigye Akamatwa Baada ya Kujiapisha Kuwa Rais
Related Posts:
Real Madrid wakubali kuacha point tatu katika dimba la El Madrigal dhidi ya Villarreal Baada ya December 12 watani zao wa jadi klabu ya FC Barcelona ya Hispania kucheza mchezo wake wa 15 wa Ligi Kuu Hispania dhidi ya klabu ya Deportivo La… Read More
Nape: Nitaanza Kushughulikia Sheria na Nidhamu Michezoni Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo, Nape Nnauye ameahidi kushughulikia sheria mbalimbali zinazosimamia sekta hiyo ili kuongeza nidhamu michezoni. Nape aliyeapishwa juzi kuanza kibarua hicho, ataiongoza wi… Read More
Diamond Platnumz na Zari Washinda Tuzo Nchini Uganda STAA wa muziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platinumz’ pamoja na mchumba wake Zarinah Hassan ‘Zari The Bossy Lady’ wamepata Tuzo za Abryanz Style and Fashion (ASFA 2015) zilizofanyika Kampala, Uganda usiku wa… Read More
Giroud na Ramsey waipeleka Arsenal kileleni, huku wakiiombea ushindi Chelsea December 13 mechi za Ligi Kuu Uingereza ziliendelea kama kawaida, baada ya December 12 kupigwa michezo kadhaa ya muendelezo wa Ligi. Mchezo wa kwanza kupigwa Ju… Read More
Kazi ya kwanza kuifanya Naibu Waziri Kigwangwala baada ya kuapishwa Dec 12 (+video). Kwenye zama hizi za Hapa kazi tu za Mheshimiwa Rais John Magufuli,tunashuhudia mambo mengi ambayo mengine tulikua hatuyafi… Read More
0 comments:
Chapisha Maoni