Wabunge nchini Afrika Kusini wamepigana bungeni baada ya spika kuamuru maafisa wa usalama kuwaondoa kwa lazima wabunge wa upinzani ambao walimbeza rais Jacob Zuma alipoingia bungeni tayari kulihutubia kikao.
Rais Zuma ambaye ameshindwa katika kesi mbili kuu zinazomhusisha na ubadhirifu wa mali ya umma na usimamizi mbaya alikuwa amefika bungeni kwa mara ya kwanza tangu kushindwa mahakamani.
Hata hivyo ujio wake uliwakera sana wabunge wa chama cha upinzani Economic Freedom Fighters (EFF).
Wabunge hao chini ya kiongozi wao Julius Malema walipiga mayowe na kumtupia matusi bw Zuma jambo lililomlazimu spika wa bunge kuamuru wabunge hao wa EFF kuondolewa nje.
Ijumaa iliyopita mahakama ya juu ya Afrika Kusini iliamua kuwa rais Zuma anapaswa kufikishwa kizimbani kufuatia kesi za ufisadi dhidi yake.
Kesi hiyo inahusiana na ufisadi uliotokea katika ununuzi wa silaha zenye thamani ya mabilioni ya dola mwaka wa 1999.
Zuma amekanusha madai yote dhidi yake, Anatarajiwa kukamilisha hatamu yake mwaka wa 2019.
Uamuzi huo wa mahakama ulikuwa msumari wa moto kwa kidonda cha Zuma ambaye mwezi uliopita alipatikana na hatia ya matumizi mabaya ya madaraka yake alipokaidi amri yakulipa pesa za umma zilizotumiwa kukarabati nyumba yake ya Nkandla.
Alhamisi, 5 Mei 2016
Home »
» Wabunge warushiana makonde Afrika Kusini
Wabunge warushiana makonde Afrika Kusini
Related Posts:
Magazeti ya Tanzania October 26, 2016 kuanzia, Udaku, Hardnews na michezo Share Tweet Share Share comments October 26 2016 naanza kwa kukusogezea post ya stori zote kubwa zilizobebwa kwenye Magazeti ya Tanzania kua… Read More
UKOCHA: Pluijm Amwaga Mboga Yanga Usemi wa Waswahili kuwa, ukimwaga ugali, nami namwaga mboga umetimia kwa klabu ya soka ya Yanga ambayo licha ya uongozi wake jana kukanusha kuajiriwa kwa kocha Mzambia George Lwandamina na kuachana n… Read More
Kinara wa Matusi Instagram Akamatwa na Polisi Baada ya Kutoa Matusi Makubwa Kuhusu Perfume Mpya ya Diamond Kijana mmoja ambaye anatumia jina la Shilolekiuno_official Huko Instagram hatimae amekamatwa na jeshi la polisi kwa kutukana na kukashifu watu mbali mbali mtandaoni, kijana huyo amekuwa akiandika matusi m… Read More
Rais Magufuli Aongoza Kura Kuwania Tuzo ya ‘Forbes Africa Person of The Year’ Rais John Magufuli anaongoza kura za kuwania tuzo ya ‘Forbes Africa Person of The Year’, ambayo hutolewa kwa watu walioonyesha mchango kwa jamii. Huku zikiwa zimebaki siku 21 kwa mshindi wa tuzo hiyo kuta… Read More
Mimba ya Nisha Bebee Yazua Balaa..Adai Baba Kijacho Wake Hawezi Hata Kujinunulia Sabuni ya Kufulia Boxer Ujauzito wa Mwigizaji Nisha Bebee umezidi kuzua sinto fahamu kutokana na vichambo anavyopost mtandaoni kwenda kwa Muhusika wa Ujauzito huo..leo tena amepost akimtolea uvivu kama ifuatavyo: "Watu wanasema n… Read More
0 comments:
Chapisha Maoni