Usiku wa Alhamisi ya Septemba 15 2016 ilikuwa siku ambayo macho ya watanzania wengi waliyaelekeza Australia kumuangalia nahodha wao wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars Mbwana Samatta akiandika historia mpya katika maisha yake ya soka kwa kucheza mchezo wake wa kwanza wa hatua ya makundi ya Europa League akiwa naKRC Genk.
Samatta ambaye alicheza kwa dakika 77 kabla ya kocha wake Peter Maes kumtoa na kumuingiza mgiriki Nokolaos Karelis, alitolewa wakati ambao timu yake ipo nyuma kwa goli 3-1 kabla ya dakika ya 90 mjamaica Leon Bailey kufunga goli la pili kwa mkwaju wa penati na kuufanya mchezo umalizike kwa sare ya goli 3-2.
Kipindi cha kwanza licha ya Genk kuzidiwa hali ya umiliki wa mpira kwa asilimia 53 kwa 47 walienda mapumziko wakiwa mbele kwa goli moja lililofungwa na Leon Bailey ikiwa ni assist safi iliyotoka kwa Pozuelo alipewa mpira na Samatta, hali ilibadilika kuanzia dakika ya 51 hadi 60 Genk waliporuhusu kufungwa goli 3 ndani ya dakika 10.
Magoli ya Rapid Wien yalifungwa na Stefan Schwab dakika ya 51, Joelinton Cassiodakika ya 59 na nyota wa Genk aliyejifunga baada ya kumrudishia mpira kipa wakeMarco Bizot na kuukosa dakika ya 60, KRC Genk watacheza mchezo wao wa pili waEuropa League Septemba 29 wakiwa nyumbani dhidi ya klabu ya Sassuolo Calcio yaItalia.
0 comments:
Chapisha Maoni