Bado mashabiki wa Man United wanashangazwa na maamuzi ya kocha Jose Mourinho kumuacha nahodha wao Wayne Rooney jijini Manchester na kusafiri hadi Uholanzi kucheza mchezo wao wa kwanza wa Kundi A dhidi ya Feyenoord, huo ni mchezo ambao umechezwa katika dimba la Stadion Feijenoord.
Kabla ya dakika 90 za mchezo huo kumalizika kwa Man United kuondoka vichwa chini kwa kukubali kipigo cha goli 1-0 lililofungwa na Tonny Vilhena dakika ya 79, takwimu ilikuwa inaonesha mara ya mwisho Novemba 5 1997 Man United alicheza katika uwanja huo na kuondoka na ushindi wa goli 3-1.
Rekodi dhidi ya Feyenoord haikuisaidia Man United na badala yake wameondoka na huzuni kwa kuvunjwa rekodi yao ya kufungwa mechi nne za Europa League mfululizo ugenini katika historia , Man United sasa watashuka dimbani Septemba 29 Old Traffordkucheza dhidi ya Zorya ya Ukraine katika mchezo wao wa pili
.
.
0 comments:
Chapisha Maoni