Amejitokeza mtu mmoja na kufanya press conference kwa jina anajulikana
kama Methusela Gwajima , huyu Bwana ni Mwanasheria na ameajiriwa kwenye
law firm ya Francis Stolla ambaye anagombea Urais wa TLS .
Huyu Mwanasheria sio mdogo wake na Gwajima wa kuzaliwa , bali ni ndugu katika Ukoo wao huo, naye ni wa KOLOMIJE .
Historia yake ya Kazi inaonyesha kuwa Aliwahi kuwa Katibu msaidizi wa
CCM Wilaya ya Singida na katika Wilaya ya Nzega katika cheo hichohicho
kwa nyakati tofauti. Kwa sasa ni miongoni mwa wanasheria wa CCM .
CCM wameamua kumtuma kada wao wakifikiri kuwa anaweza kuaminika au
kunyamazisha mjadala wa kudai vyeti halisi vya BASHITE ambaye kwa sasa
ana stress nyingi sana na amezidiwa kabisa kabisa , baada ya watanzania
kuamua kumuunga mkono Rais Magufuli katika zoezi la kuhakiki Vyeti
linaloendelea.
Mjadala wa BASHITE utashika kasi sana kwenye vikao vya CCM na hasa
kwenye Halimashauri Kuu ambako tayari yule Mbunge wa kule Geita ambaye
ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa ameomba kuwasilisha hoja mahususi kwenye kikao
cha Halimashauri Kuu kuwa Bashite anakichafua Chama , hivyo anataka
waazimie kuwa aondolewe na kama halitafanyika basi hoja itawasilishwa
Bungeni ili kumwazimia PM ambaye yuko kwenye Mamlaka yao.
0 comments:
Chapisha Maoni