Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi(UVCCM) umemtaka Waziri Mkuu
aliyejiuzulu kwa kashfa ya Rchmond Edward Lowassa kuacha uongo kwani
hana historia ya kupigania maslahi ya umma.
Aidha, imesema madai ya lowassa kwamba aliwahidi wananchi angeunda Tume
ya kupitia mikataba ya madini kama angeshinda urais ni uongo na kutaka
kujitafutia umaarufu wa kisiasa.
Pia umoja huo umemtaka Lowassa kuonyesha ushahidi video ya matamshi yake
wakati akiwa katika mkutano wa hadhara akihutubia mkoani Geita
ikionyeaha kama kweli alitoa matamshi hayo.
Hayo yalielezwa jana na Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Shaka Hamdu Shaka
alipozumgumza waandishi wa habari jana ofisini kwake Upanga jijini Dar
Es Salam.
alisema Lowassa hama nguvu za uzalendo wa kupigania au kuzungumzia
mapambano dhidi ya ubadhirifu wa mali za umma kwasababu hata kujiuzulu
kwake kulitokana na shinikizo la bunge huku akihusishwa na sakata la
ufisadi.
Shaka alibainisha kuwa hakuna ushahidi wala kumbukumbu inayoonyesha kuwa
Lowasa siku moja aliwahi kutetea maslahi ya umma wakati akiwa
serikalini kama Waziri au alipoteuliwa kuwa Waziri Mkuu na Rais Mstaafu
Jakaya Kikwete.
"UVCCM tumemestushwa na matamshi ya Lowasa yanayodai wakati wa kampeni
za uchaguzi mkuu akiwa Mkoani Geita kuwa aliwahi kutamka kama angeshinda
urais angeunda Tume ya kupitia mikataba ya madini , hakuna ushahidi huo
na hawezi kuthibitisha ni uongo mtupu "Alisema Shaka.
Shaka alisema kama kweli angekuwa na ujasiri huo wakati alipokuwa waziri
mkuu angeweza kutamka maneno hayo au kumshauri Rais iundwe Tume lakini
alishindwa kwa sababu hana ujasiri na uzalendo kama anavyotaka
kuwaaminisha wananchi baada ya kuona Rais John Magufuli akiungwa mkono
kitaifa na kimataifa.
Kaimu huyo Katibu mkuu alikumbushia kuwa alichosikika akisema Lowasa ni
kwamba akiwa Rais atawakaribisha wawekezaji zaidi pamoja na marafiki
zake wenye nguvu za fedha na mitaji mikubwa ili kuiendeleza migodi na
uchimbaji wa madini ambayo itamtajirisha kila wananchi bila kuelezea
mbinu za utekelezaji huo.
"Waziri pekee jasiri, mzalendo na aliyekuwa mchapakazi kwa bidii katika
serikali ni Dk Magufuli kwani hata Lowassa alipomnadi Dk Magufuli wakati
akiwania ubunge mwaka 2005 alimtaja mbele ya wananchi kwamba ni jembe
na turufu muhimu "Alisema Shaka.
Aidha alieleza sifa peke ya Lowassa akiwa serikali ni tabia yake ya
kumshauri jambo Rais na kama litafanyika, hugeuka na kuwaambia watu
kwamba yeye ndiye akiyemshauri Rais na kama si yeye kisingefanyika.
Shaka alisema upo ushahidi kwamba aliwahi kumshauri suala fulani Rais
mstafu Mzee Ali Hassan Mwinyi kisha akawaambia wapambe wake kwamba yeye
ndiye aliyeshauri kitendo kilichomfanya Mwalium Julius K. Nyerere amwite
kilichjambo lililomfanya mwalimu Julius Nyerere amwite Lowassa nyumbani
kwake msasani na kumkanya.
"Lowasa aliitwa mbele ya aliyekuwa Katibu Mkuu wa UVCCM Sukwa Said Sukwa
nyumbani kwa mwalimu Msasani akasemwa vikali sana na mwalimu kwa
kitendo hicho pia akaonywa aache kutumia magazeti kusaka uongozi na
umaarufu"Alieleza Shaka
Pia Shaka alimtaka Lowassa kuacha tabia ya kutaka kuvika joho lisilo na
hadhi yake na akumbuke tuhuma ambazo amewahi kurushiwa na viongozi wa
chadema wakipita huku wakimnadi nchi nzima haziwezi kufutika kwa mtindo
anaotaka wa kujifagilia kwa uzushi.
Hata hivyo kaimu katibu mkuu huyo alisema si kweli kama ujasiri,
uzalendo na utashi wa kutaka kufanya mabadiliko ya kiuchumi, kupambana
na ufisadi na kupitia mikataba michafu haiwezekani kufanyika bila katiba
mpya kama anavyodai Lowasa.
"Ujasiri, uzalendo na uthubutu wa kutenda mambo yoyote magumu hakuhitaji
mabadiliko ya katiba , aidha kwa kuwepo wa katiba mbaya au nzuri
kwasababu vitu hivyo havishabihiani , katiba iliopo ni nzuri na Dk
Magufuli ataleta maajabu ya kihistoria chini ya katiba ya sasa
"Alisisitiza Shaka
Alimtaka Lowasa kufuta ndoto na matumaini kwamba itatokea siku moja
akawa Rais wa nchi hii na kuacha kueneza uzushi kuwa alikatwa jina lake
kwa kumhofia angepitia mikataba ya madini.
"Jina la Lowassa liliondolewa kwasababu kadhaa ikiwemo matumizi mabaya
ya madaraka, viongozi wa CHADEMA kumnanga nchi nzima pamoja na ukiukaji
wake wa taratibu, miiko na maadili huku akitumia nguvu za fedha kutaka
ateuliwe jambo ambalo CCM imelikataa "Alisema Shaka .
Baadhi ya vyombo vya habari jana vilimnukuu Lowassa akimpongeza Rais Dk
Magufuli kwa kuunda Tume ya kupitia mikataba ya madini huku akijigamba
naye aliwaahidi wananchi wakati kampeni akiwa mkoani Geita kwamba
akishinda urais angeunda Tume jambo ambalo pia lilifanya jina lake
kukatwa ndani ya CCM.
0 comments:
Chapisha Maoni