Jumanne, 14 Novemba 2017

Mnunuzi Feki wa Nyumba za Lugumi Kupimwa Akili

Bilionea Dkt. Luis Shika ambaye wiki iliyopita alitangaza kununua nyumba za kifahari za mfanyabiashara za Said Lugumi, zilizopo eneo la Bweni JKT jijini Dar es salaam anatarajiwa kupelekwa hospitali kupimwa afya ya akili.Hayo yamesemwa na Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Mwandamizi Msaidizi wa Jeshi la Polisi (SACP), Benedict Kitalika, ambapo...

Dk Cheni Awapa Makavu Wanaomsakama Lulu Kuhusu Dhamana

MSANII mkongwe katika tasnia ya maigizo Bongo na mshereheshaji (MC), Mahsein Awadhi ‘Dk. Cheni’ ambaye ni mlezi wa mwigizaji Elizabeth Michael ‘Lulu’ ametoa maoni yake kwenye mtandao wa kijamii baada ya kuibuka maneno mengi kwenye mitandao hiyo ambapo watu wengine wanasema Lulu amepewa adhabu ndogo na wengine wakipendekeza angefungwa kwa miaka mitano na kuendelea.Dk Cheni...

Yanga Yasajili Straika Mpya wa Maana

ZIKIWA zimebaki siku moja kabla ya kufunguliwa kwa dirisha dogo la usajili hapa nchini, uongozi wa Yanga unajipanga vilivyo kuhakikisha unakiimarisha kikosi chake ili kiweze kufanya vizuri katika mechi zake zijazo za Ligi Kuu Bara lakini pia katika michuano ya kimataifa. Uongozi unahitaji kusajili wachezaji wanne katika dirisha hili dogo la usajili kwa ajili ya kuziba upungufu...

Wabunge Wanaotaka Pensheni Watakiwa Kuanzia Bungeni Kabla ya Kufika Serikalini

Serikali imewataka wabunge wanaotaka utaratibu wa kulipwa pensheni mara baada ya kumaliza kipindi cha ubunge urejeshwe, walipeleka jambo hilo kwanza kwenye  Tume ya Utumishi ya Bunge kabla ya kulifikisha serikalini. Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana na Ajira, Anthony Mavunde amesema leo Jumanne bungeni kwa niaba ya Waziri wa Katiba na Sheria wakati...

Idriss Atuma Salamu za Pole kwa Mama Lulu "Mama Ndio Tunahitaji Kukuangalia Zaidi"

MCHEKESHAJI na mshindi wa Big Brother Africa, Idris Sultan, ametoa pole kwa mama wa mwigizaji Elizabeth Michael ‘Lulu’, Lucresia Kalugira, kwa kipindi kigumu alichokianza jana baada ya bintiye kuhukumiwa kifungo cha miaka miwili jela kutokana na kumuua bila kukusudia msanii mwenzake, Steven Kanumba. Sultan amesema jamii impe faraja na kumtia moyo wakati akiwa katika huzuni...

Mange Kimambi Afunguka baada ya Lulu kupigwa mvua ya Miaka Miwili

From @mangekimambi_ - Breaking newzzzzzzzz..... Lulu amekutwa na hatia ya kuuwa bila kukusudia na amehukumiwa miaka miwili jela..........Dah huyu jaji anawaza kama mimi posti yangu niliyoposti masaaa mawili yaliyopita nilisema ningekuwa jaji ningemkuta na hatia ila ningempa adhabu ndogo mwaka mmoja au miwili jela.........Jaji ametenda haki......Sio kama nimefurahi Lulu kafungwa...