Ijumaa, 16 Machi 2018

Dogo Janja Amekuwa James delicious ?- Young Tusso

                                          Dogo Janja Amekuwa James delicious ?- Young Tusso
Msanii wa HipHop nchini Tanzania, Young Tusso amefunguka na kumtaka Dogo Janja aende kuwaomba radhi wananchi wa mkoa wa Arusha kwa madai amewakosea sana kwa kitendo chake cha yeye kujifanya mwanamke katika video yake mpya ya Wayuwayu.

Young Tuso ametoa kauli hiyo wakati alipokuwa anazungumza kwenye kipindi cha e Newz inayorushwa na tinga namba moja kwa vijana EATV baada ya kupita siku kadhaa tokea Janjaro kutoa video ya wimbo huo na kupelekea kupondwa kwa watu wengi kwa kitendo alichokionesha licha ya kuwa wimbo huo mpaka sasa kuonekana kupendwa.

"Nilistushwa sana baada kuona instagram picha za Dogo Janja kumuona amekuwa mwanamke maana hata hivyo video haikuwa na ulazima wa weye kuwa mwanamke kwa hiyo mimi nimemtazama kama mtoto wa kiislamu. Dogo Janja sasa inabidi akaiombe msamaha Arusha", amesema Young Tusso.

Pamoja na hayo, Young Tusso ameendelea kwa kusema "nafikili mimi nipo tofauti kidogo sikubaliani na yeye kuwa 'video vixen'. Unajua kumuona msanii kama Dogo Janja halafu wa HipHop ambaye anatokea Arusha wenye asili ya ugumu kidogo kwa hiyo mwisho wa siku unamuona amekuwa James delicious tena inanipa tabu sana kuona hivyo"

Related Posts:

  • Waaga mchuano baada ya kuagizwa kuvua hijab Timu ya wanawake ya Qatar ya mchezo wa mpira wa kikapu imejiondoa kutoka mashindo ya bara Asia. Timu ya wanawake ya Qatar ya mchezo wa mpira wa vikapu imejiondoa kutoka mashindo ya bara Asia yanayofanyika huko Korea Kus… Read More
  • Van Gaal:tuna mlinzi wa kati mmoja tu  Kocha wa Manchester United Louis Van Gaal. Kocha wa machester United, Louis van Gaal amesema Manchester united ina mlinzi wa kati mmoja tu mwenye uzoefu wakati huu kikosi hicho kinapotarajia kukipiga na west ham kat… Read More
  • 'VIPIMO VYA SKETI KIGEZO CHA SARATANI'  Baadhi ya watafiti wana sahuku ikiwa vipimo vya sketi vitamtahadharisha mwanamke kuhusu tisho la Saratani. Utafiti unaonyesha kuwa wanawake wanaonenepa maishani bila ya kuwa waangalifu wanajiweka katika hatari ya kupa… Read More
  • NI KIVUMBI LIGI YA MABINGWA ULAYA   Katika michuano ya Klabu Bingwa barani Ulaya leo kuna kivumbi kingine ambapo CSKA Moscow itakuwa na kibarua kigumu pale watakapowakaribisha Bayern Munich. Wakati huo huo Man City waliopigwa bao moja na Bayer… Read More
  • Taarifa kuhusu kifo cha msanii wa bongofleva Side Boy Mnyamwezi. Ingawa Nafasi yake katika muziki wa Bongo Fleva ilikuwa ikipanda taratibu kulingana na aina ya muziki aliokuwa akiumba,single iliyomtambulisha zaidi kwenye muziki wa Bongo Fleva inaitwa Kua uone ambayo alimshirikisha A… Read More

0 comments:

Chapisha Maoni