Jumanne, 8 Desemba 2015
Huyu ndio kocha anayenyemelea kibarua cha Louis van Gaal Man United, kakiri hapa …
Kuna mengi yanaendelea katika soka,
tetesi na uvumi katika soka ni moja kati ya vitu vinavyo ingia katika
headlines kila siku, vilabu vingi duniani vimekuwa vikijitahidi kuweka
usiri katika mambo yake, headlines za kocha wa Manchester United Louis van Gaal kutaka kuachia ngazi klabu hiyo zinazidi kuchukua nafasi.
Jumamosi ya December 5 kocha huyo alikiri kuwa yupo tayari kuondoka Man United
kama wachezaji wa klabu hiyo watapenda aondoke, kwani kumekuwa na uvumi
kuwa wachezaji hawana mahusiano mazuri na kocha huyo, stori zilizotoka
December 7 ni kuwa uongozi wa klabu ya Man United unapanga kumuongezea mkataba, yote hayo yanaandikwa na vyombo vya habari.
Stori ni kuwa kocha wa zamani wa klabu ya Chelsea na Real Madrid muitaliano Carlo Ancelotti amekiri kuvutiwa na kujiunga na Man United
licha ya kuwa hana mpango wa kujiunga na timu yoyote katikati ya msimu,
swali ambalo alijibu mara baada ya kuulizwa kama angependa kuwa kocha
wa Man United.
“Sio
kwamba natafuta klabu iliyo na mipango mikubwa sana kwani naweza
kusubiri kwa sasa sababu sina mpango wa kujiunga na timu katikati ya
msimu, tusubiri hadi mwisho wa msimu kwani nina mipango ya kurudi kazini
msimu ujao. kuhusu kuvutiwa na nafasi ya kuwa kocha wa Man United,
bilashaka hakuna kocha asiyevutiwa na nafasi ya kuwa kocha wa Man
United” >>>> Carlo Ancelotti
Louis van Gaal ambaye ni kocha wa klabu ya Man United
ana mkataba na klabu hiyo hadi mwaka 2017 ila amekuwa akihusishwa kuwa
na mpango wa kuachana na klabu hiyo mwishoni mwa msimu na kupanga
mipango ya kustaafu ili apate muda wa kupumzika na mkewe, stori ambazo
zimekuwa zikiandikwa katika vyombo vya habari mara kadhaa.
Mawaziri wa Jakaya Kikwete Hawajahama Nyumba za Serikali
Wakati
Watanzania wakisubiri kufahamu sura zitakazoingia kwenye baraza jipya
la mawaziri katika Serikali ya Rais John Magufuli, baadhi ya mawaziri wa
awamu iliyopita ya Jakaya Kikwete hawajaziachia nyumba za Serikali
walizokuwa wanaishi.
Kwa
mujibu wa Kanuni za Utumishi wa Umma, mawaziri wanastahili kuishi
kwenye nyumba za Serikali kuanzia pale uteuzi wao unapotangazwa ili
kuanza kutekeleza majukumu yao wakiwa katika mazingira salama, wao na
familia zao. Haki hiyo hukoma mara moja; pale wanapovuliwa wadhifa huo
au baraza husika linapovunjwa baada ya kukamilisha muhula wake au sababu
nyingine yoyote.
Maandalizi
ya Rais Magufuli katika uteuzi yanakwenda sambamba na taasisi
zinazohusika kutekeleza wajibu wao wa kuandaa makazi ya wateule
wanaotarajiwa, lakini zinakwamishwa na mawaziri ambao hawajahama.
“Tumepata
fedha za kutosha kukarabati nyumba zenye uhitaji huo kutoka wizarani.
Nyumba 15 zipo katika utekelezaji. Kuna baadhi tunasubiri waliomo wahame
ili tuweze kuendelea,” alisema Mhandisi Edwin Nnunduma, kaimu
mkurugenzi wa ushauri wa Wakala wa Nyumba za Serikali Tanzania (TBA).
Nnunduma
alisema kila kitu kipo tayari na mapokezi ya viongozi hao
hautacheleweshwa kwa namna yoyote ile kwa kuwa nyumba zipo za kutosha
kuwahifadhi ili walitumikie Taifa kwa viwango vinavyohitajika.
Takwimu
zinaonyesha kuwa wakala huyo anasimamia jumla ya nyumba 93 na kati ya
hizo 29 zilikuwa zinakaliwa na mawaziri wa Serikali iliyopita ya Rais
Jakaya Kikwete ambao, kwa mujibu wa kanuni walistahili kuziachia mara tu
baada ya Rais Magufuli kuapishwa, Novemba 5.
Kwa
mujibu wa Nnunduma, ukarabati huo unahusisha nyumba 35 ambazo
zinajumuisha 29 za mawaziri na sita wanazoishi baadhi ya makatibu wakuu
wa wizara.
Taarifa
zilizolifikia Mwananchi zinaeleza kuwa wapo baadhi ya mawaziri ambao
wamekaidi kuondoka kwenye nyumba hizo, licha ya kanuni na sheria
kuwataka kufanya hivyo na agizo la Katibu Mkuu Kiongozi lilikwishatolewa
likiwataka kurudisha magari na nyumba za Serikali.
Alipoulizwa
kuhusu suala hilo, Mnunduma alisema, “Kuna waraka wa Katibu Mkuu
Kiongozi uliowataka wahame kwenye nyumba hizo ndani ya siku 30 baada ya
kuapishwa kwa Rais mpya. Muda huo uliisha jana (juzi), naamini bado
baadhi hawajahama mpaka sasa. Nilikuwa safarini hivyo sina uhakika ni
nani na nani hawajafanya hivyo.”
Novemba
5, mara baada ya kuapishwa kwa Rais Magufuli, Katibu Mkuu Kiongozi,
Ombeni Sefue, aliwaagiza mawaziri na manaibu waziri kurudisha magari ya
Serikali ikiwa ni siku yao ya ukomo wa uongozi. Katika agizo hilo,
alisema baada ya bendera ya Rais anayemaliza muda wake kuteremshwa na
kabla ya ile ya Rais mpya kupandishwa, magari hayo yanatakiwa
yabadilishwe namba kwa kuondoa herufi ya cheo na kuwekwa zile za
Serikali.
Wakati
urejeshaji wa magari ulifanywa mara moja, uhamaji kwenye nyumba za
Serikali ulipewa muda wa siku hizo 30, ili kutoa fursa kwa familia
husika kuandaa mazingira hayo ikiwa ni pamoja na kusafirisha mali husika
za viongozi hao na walio nao.
Kukawia
huko kwa baadhi ya mawaziri kunaelezwa kuwa huenda kukawa na sababu
mbili; ama uhakika wa kurudi kwenye baraza jipya au kutokana na ukosefu
wa mahali pa kuhamia baada ya utumishi kukamilika na muda wa kutafuta
mahali pengine penye hadhi sawa na yao kuwa changamoto.
“Wapo
baadhi ya mawaziri ambao walichaguliwa siku za mwisho ambao kabla ya
hapo walikuwa wanaishi majimboni kwao. Mwezi mmoja uliotolewa unaweza
usitoshe kwa wao kutafuta nyumba nyingine hapa mjini itakayowafaa
kulingana na mahitaji yao,” kilisema chanzo ambacho hakikutaka kutajwa.
Uchunguzi
wa gazeti hili katika mitaa Mikocheni, Masaki na Kijitonyama ziliko
nyumba za mawaziri ulibaini baadhi zikifanyiwa ukarabati na baadhi ya
walinzi waliohojiwa wakibainisha kuwa mawaziri wengi walishaondoka
katika makazi hayo.
Hata
hivyo, ofisa wa TBA anayeshughulikia makazi ya mawaziri Kanda ya
Masaki, Juma Hamis alisema mawaziri waliokuwa wamebakia kwenye eneo lake
ni Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Januari Makamba
na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tamisemi, Hawa Ghasia.
“Kwa taarifa nilizonazo, hawa mawaziri wanahama leo (jana) kwani tayari wameanza kuhamisha baadhi ya vitu vyao,” alisema Juma.
Hata
hivyo, Makamba alipoulizwa alisema hajawahi kuishi kwenye nyumba ya
Serikali tangu aanze kuwatumikia wananchi kwa nafasi tofauti alizowahi
kuzitumikia.
Alisema, “Siku zote naishi kwenye nyumba yangu. Tangu nilipokuwa ikulu na hata nilipoondoka na kuwa waziri.”
After Lots of Rumors Finally Quick Racka Confirms Dating Kajala
There have been lots of speculations and
rumors about Kajala dating Bongo Flava singer Quick Racka. Media did
write about their secret relationship although they both denied it. Even
Quick Racka had tattoo of Kajala's name. But speaking with Clouds fm
Quick Racka was asked wheather he is still with Kajala or have already
parted ways the singer replied they are still together ...
"Sometimes some things have to stay private because when love life get in public all the time rumors spread all the time too so sometimes it is better to be private but we are doing good...words on the streets are lots but we are the ones who know the truth" said Quick Racka
"Sometimes some things have to stay private because when love life get in public all the time rumors spread all the time too so sometimes it is better to be private but we are doing good...words on the streets are lots but we are the ones who know the truth" said Quick Racka
Umeiona video mpya ya Belle 9 ‘Burger Movie Selfie’?ninayo hapa……
Belle 9 baada ya kutambulisha rasmi single yake mpya Burger Movie Selfie katika vituo mbalimbali vya radio Dec 7 2015, sasa time hii pia ametusogezea na video mpya ya single hiyo.
Kwa mujibu wa msanii huyo ni kwamba video imeshutiwa Morogoro na director GQ wa Morogoro, itazame hapa.
Kutokuwapo Kwa Mawaziri Kumeokoa Mamilioni
Uamuzi
wa Rais John Magufuli kukaa zaidi ya mwezi mmoja bila kuteua Baraza la
Mawaziri huenda ukawa umeisaidia Serikali kwa kuokoa takribani Sh683.3
milioni za walipa kodi, bila kuhusisha gharama za ununuzi wa
‘mashangingi’.
Kiasi
hicho cha fedha kimetokana na hesabu inayokadiriwa kuwa matumizi ya
waziri iwapo Rais Dk Magufuli angeendelea na ukubwa wa Baraza la
Mawaziri la mwisho la Rais Jakaya Kikwete la mawaziri 55, kati ya hao 24
wakiwa manaibu waziri.
Hata
hivyo, Dk Magufuli ameshatangaza kuwa na baraza dogo la mawaziri,
ingawa hajaweka bayana litakuwa na jumla ya mawaziri wangapi.
Kwa
mujibu wa aliyekuwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya
Makazi, Goodluck Ole-Medeye, Waziri hulipwa mshahara wa kati ya
Sh3.8milioni mpaka Sh 5milioni kwa mwezi ambazo ni sawa na mshahara
wanaolipwa wabunge.
Kwa
mantiki hiyo, kwa mawaziri 55, Serikali ilitakiwa ilipe Sh209 milioni
kwa ajili ya mishahara ya Novemba, lakini hazikulipwa kwa kuwa bado
kiongozi huyo hajawateua.
Kanuni
za kudumu za utumishi wa umma toleo la mwaka 2009, zinaitaka Serikali
kumpatia nyumba mtumishi anayetakiwa kupatiwa huduma hiyo kwa aidha
kumpa nyumba ya Serikali au kumkodishia nyingine yenye hadhi ili aweze
kutimiza wajibu wake ipasavyo.
Kanuni
hizo zinamtaka Wakala wa Majengo (TBA) kufanikisha zoezi hilo la kutoa
huduma za nyumba au kusimamia ukodishaji wa nyumba husika ya mtumishi.
Mawaziri
ni miongoni mwa watumishi wanaopatiwa nyumba za Serikali ambazo nyingi
zinapatikana katika maeneo ya vigogo ya Masaki, Oysterbay au Mikocheni
jijini Dar es Salaam.
Kwa
mujibu wa tovuti ya uuzaji na ukodishaji nyumba na viwanja ya Lamudi,
nyumba za bei ya wastani ambayo inaweza kwenda na hadhi ya waziri
inakodishwa kwa kiasi kisichopungua Sh5 milioni kwa mwezi.
Hivyo
basi, kama nyumba za mawaziri hao ambazo hukarabatiwa na kuhudumiwa na
TBA, zingekuwa zimekodishwa kutoka kwa watu binafsi kwa kipindi cha
mwezi mzima basi Serikali ingelipa Sh275 milioni.
Ili
kutimiza majukumu yao vyema wakiwa bungeni mjini Dodoma, mawaziri pia
hupatiwa nyumba za kuishi tofauti na zile za Dar es Salaam ambazo zipo
chini ya TBA.
Hata
hivyo, Ole-Medeye alisema Serikali huwalipa mawaziri Sh800, 000 kwa
mwezi kwa ajili ya huduma za nyumba za Dar es Salaam, mawasiliano na
ankara nyingine za kumsaidia kimaisha.
Iwapo
kiwango hicho cha Sh800, 000 kwa mwezi kingetumika kumlipa kila waziri
kama sehemu ya fedha za makazi, bado Serikali ingehitajika kutoa Sh44
milioni kwa ajili ya gharama za kuhudumia nyumba na mawasiliano.
“Hivi
Sh800, 000 utapata wapi nyumba ya kukodi akaishi waziri? Kwa bei ya
sasa nyumba za kiwango hicho ni Dola za Marekani 3,000 (Sh6 milioni) au
zaidi.
“Sasa
fedha hiyo umlipe mtumishi wa ndani, gharama za umeme, mawasiliano na
maji ndiyo maana nasema uwaziri ni kazi ya kuhudumia jamii,” alisema
Ole-Medeye akieleza kuwa waziri hupatiwa posho ya Sh80, 000 kwa siku
akiwa mikoani kwenye ziara.
Gharama
za posho za mawaziri hao zingetegemea na siku ambazo wangekaa mikoani
kwa kipindi hicho cha siku 31, na hivyo si rahisi kujua kiwango chake.
Gharama za samani
Miongoni
mwa mambo ambayo Serikali hugharamia kwa mawaziri wake ni samani za
ndani ya nyumba, ambazo pia huongezeka au kupungua kulingana na ukubwa
wa baraza.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dk Adelhelm Meru alisema ununuzi
wa samani za ndani ya nyumba za waziri husimamiwa na Mamlaka ya
Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA) kwa wizara zote na hununuliwa kila
baada ya miaka mitano.
Hata hivyo, Dk Meru alitoa angalizo kuwa matumizi ya waziri husika huchangiwa pia na ukubwa wa wizara na kiwango cha bajeti.
“Mawaziri wengine wanaishi kwenye makazi yao na siyo wote wamepewa makazi ya Serikali.
“Lakini wanapewa huduma ya umeme, maji, posho ya majukumu na gari,” alisema Dk Meru.
Mashangingi
Mawaziri
pia hupatiwa magari kwa ajili ya usafiri na mara nyingi huwa na ama
Toyota Land Cruiser VX V8 au GX V8 ambayo hujulikana kama “mashangingi.”
Ili
kufanikisha shughuli zao, kila waziri hupatiwa lita 1,000 kwa mwezi za
mafuta. Kwa bei elekezi ya sasa ya Mamlaka ya Udhibiti wa huduma za
Nishati na Maji (Ewura), iliyoanza kutumika Desemba 2, bei ya dizeli
jijini Dar es Salaam ni Sh1,823 kwa lita.
Gari
moja la waziri mmoja iwapo lingetumia lita zote 1,000 Serikali
ilitakiwa kulipa Sh1.823 milioni ambazo kwa baraza zima ingekuwa jumla
ya Sh100.3 milioni.
Pia, magari hayo huitaji kufanyiwa matengenezo kwa kila baada ya kilomita zinazoshauriwa na mtengenezaji.
Dk
Meru alisema kwa kawaida kila gari hufanyiwa matengenezo baada ya
kilomita 5,000 kwa kiasi cha wastani Sh1.8 milioni kila moja.
Kwa
maana hiyo, katika Serikali ya “hapa kazi tu” inayohimiza viongozi wa
kutoka maofisini kwenda kusikiliza shida za wananchi vijijini, hapana
shaka kuwa mawaziri hao wangekuwa ama wameshatimiza kilomita
zinazohitaji matengenezo au wanakaribia.
Serikali kufanikisha matengenezo hayo, ingeweza kulipa kampuni husika ya matengenezo Sh99 milioni kwa mwezi.
Gharama
hizo ni mbali na fedha za kununua magari hayo ambayo kila moja
linakadiriwa kugharimu Sh250 milioni, hivyo mawaziri 55 wangetafuna
Sh13.75 bilioni.
Unafuu
wa gharama katika eneo la ununuzi wa mashangingi hayo utakuwa dhahiri
iwapo Rais Magufuli atatekeleza ahadi yake ya kuteua baraza dogo,
mathalan, akiteua mawaziri 20 atakuwa ameokoa mashangi ya mawaziri 35,
sawa na Sh8.75 bilioni.
Ukimya
wa Rais Magufuli kutoteua Baraza la Mawaziri kwa kipindi cha mwezi
kumeibua mtizamo tofauti miongoni mwa wachambuzi wa masuala ya Siasa na
utawala, wengi wakisema kuna faida nyingi kuliko hasara.
Rekodi 5 za kuvutia za Lionel Messi ambazo hazijawahi kuvunjwa na mchezaji yoyote …
Lionel Messi ni staa wa soka wa kimataifa wa Argentina ambaye kwa sasa anakipiga katika klabu ya FC Barcelona ya Hispania aliyojiunga nayo mwaka 2001 na mwaka 2003 akaanza kuichezea FC Barcelona C. Lionel Messi anatajwa kuwa ni moja kati ya wachezaji soka wenye rekodi za kusisimua zaidi duniani. Hizi ni rekodi 5 za kusisimua za Lionel Messi stori kutoka sokkaa.com
5- Lionel Messi sio tu anatajwa kuwa mchezaji bora wa Dunia, ila wachambuzi wa masuala ya soka wanamuita ni moja kati ya wachezaji bora wa soka waliowahi kutokea katika historia ya soka. Messi ndio mchezaji pekee ambaye amewahi kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa Dunia Ballon d’Or mara 4, kwani hakuna mwingine aliyewahi kufanya hivyo.
4- Mwaka 2012 Lionel Messi alifanikiwa kuvunja rekodi ya Muller ambaye alikuwa amefunga jumla ya goli 85 kwa mwaka, rekodi ambayo ilidumu toka mwaka 1972 ila Lionel Messi
mwaka 2012 amevunja rekodi hiyo kwa kufunga jumla ya magoli 91 katika
mechi za mashidano yote na kuvunja rekodi iliyodumu kwa miaka 40 bila
kuvunjwa.
3- Staa huyo wa Argentina
ndio mchezaji pekee mwenye rekodi ya kufunga magoli katika mechi 21
mfululizo za Ligi Kuu, rekodi ambayo aliiweka msimu wa 2012/2013.
2- Ni mchezaji wa kwanza kuzifunga mfululizo timu zote za Ligi Kuu, msimu wa 2012/2013 Lionel Messi alifanikiwa kuzifunga mfululizo timu zote 19 pinzani katika Ligi Kuu Hispania, licha ya kuwa Cristiano Ronaldo amewahi kufanya hivyo msimu wa mwaka 2011/2012 ila Lionel Messi amefunga mfululizo yaani kwa kufuatana.
1- Lionel Messi ndio mchezaji pekee aliyewahi kutwaa mara mbili tuzo ya golden ball ya michuano ya klabu Bingwa Dunia ambayo mwaka huu inafanyika Japan, rekodi ambayo aliiweka mwaka 2009 na 2011.




























