Alhamisi, 15 Septemba 2016

INSTAGRAM: MANENO MATATU ALIYOYAANDIKA SHILOLE BAADA YA KUMPOST NUH MZIWANDA

Jana September 15 2016 Mrembo kutoka Bongoflevani Shilole amezichukua headlines baada ya kupost kwa mara ya kwanza aliyekuwa mpenzi wake wa zamani Nuh MziwandaShilole ametumia mtandao wake wa Instagram kupost picha ya Nuh na kuandika maneno haya.
God Bless u‘>>>Shilolescreen-shot-2016-09-15-at-12-16-54-pm


TUNDU LISSU AISHUKIA SERIKALI KUHUSU KUTUMIA PESA ZA MIFUKO YA JAMII BILA KURUDISHA


*Anaandika Tundu Lissu*
Pesa za mifuko ya hifadhi ya jamii hazitajenga kiwanda chochote. Ni siasa tu.
Pesa za mifuko ya hifadhi ya umma sio pesa za serikali, ni pesa za wafanyakazi. Zinatokana na makato yao ya mishahara.

Serikali imekuwa inatumia pesa hizi kama zake, wakati sio zake. Pesa hizo zimetumika kujenga UDOM kwa makubaliano kwamba serikali hii ingerudisha pesa hizo kwa mifuko hiyo. Haijarudisha hata senti moja.

Pesa hizo zimejenga jengo la Usalama wa Taifa OysterBay Dar. Serikali haijarudisha hata senti moja kwa mifuko ilikochota pesa hizo. Pesa za mifuko zimejenga jengo la Machinga Complex Ilala Dar na nyumba za polisi Kurasini Dar. Serikali haijarudisha hata senti moja. Ndizo zilizojenga Daraja la Mwalimu Nyerere Kigamboni. You can rest assured haitarudi hata senti moja.

Ukweli, kama alivyosema CAG kwenye mojawapo ya taarifa zake za mwaka, mifuko ya hifadhi ya jamii ina hali mbaya ya kifedha. Hii ndio sababu wenye mamlaka wanataka kuondoa fao la kujitoa. Wameigeuza mifuko ya hifadhi ya jamii kuwa shamba la bibi mpaka mifuko inakaribia kufilisika.

Sasa wanataka kuficha uchafu huu kwa blangeti la uzalendo uchwara. Wafanyakazi wa Tanzania wakikubali udanganyifu huu wataliwa kama ambavyo pesa zao zimeliwa kwenye miradi niliyoitaja.
Suala sio tuache siasa. Hatuwezi kuacha siasa. Suala ni tuache siasa za aina gani. Hawa wanasiasa wanaojivika uzalendo uchwara kuhusu hela za wafanyakazi wao wenyewe wametengenezewa utaratibu maalum ambapo wanakatwa na NSSF halafu baada ya kumaliza ubunge wanarudishiwa pesa zao. Hawasubiri wafikishe miaka sitini ndipo wapate mafao yao ya kujitoa.

Halafu wanawahubiria wafanyakazi wasubiri miaka sitini ndipo wapate mafao yao. Wana ndimi mbili kama za nyoka. Wafanyakazi wa Tanzania amkeni, hamna chochote cha kupoteza isipokuwa minyororo yenu.



UTAFITI WA TWAWEZA: WATANZANIA 96% WANAMPONGEZA RAISI MAGUFULI


Taasisi inayojishughulisha na kufanya tafiti mbalimbali nchini ya TWAWEZA. Leo imetoa ripoti inayoonyesha kuwa asilimia 96 ya Watanzania wapongeza utendaji wa Rais Magufuli, huku asilimia 68 wapongeza uwajibikaji wa wabunge wao.

Aidha katika ripoti hiyo inabainisha kuwa jambo maarufu alilofanya Rais Magufuli ni uondoaji watumishi hewa huku zuio la kuingiza sukari likikosa umaarufu.

Kiwango cha kukubalika cha Rais Magufuli katika utafiti mpya ni cha juu kuliko marais 128 wa Afrika.

CONGO DRC: WAASI WA MAI MAI WAMEWATEKA MADEREVA 5 WA TANZANIA, WANATAKA $ 4,000 KWA KILA DEREVA



KUNA TAARIFA KUWA waasi wa Mai Mai wamewateka madereva wa Tanzania watano na kuchoma baadhi ya magari. Wanadai usd 4000 kwa kila Dereva amasivyo watawapiga risasi. Wametoa deadline ya majeshi kuondoka pia.

Chama cha Wamiliki wa Magari ya Mizigo nchini Tanzania (TATOA) kinaripoti kwamba, waasi wa Mai Mai nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), wamewateka nyara madereva wa Tanzania na kuchoma baadhi ya magari ya mizigo. Waasi hao wanadai dola za Kimarekani elfu nne (karibu shilingi za Kitanzania milioni tisa) kwa kila dereva ama sivyo watawapiga risasi madereva wote. Pia waasi hao wametoa siku ya mwisho (deadline) ya majeshi yanayolinda amani nchini humo kuondoka.

TATOA inasema imezungumza na mmiliki wa kampuni ya Simba Logistics, Mzee Azim Dewji ambaye amethibitisha taarifa hizi na pia balozi wa Tanzania DRC pamoja na Wizara ya Mambo ya Nje tayari serikali inashughulikia suala hili. Jumla ya magariyaliyotekwa ni 12 kati ya hayo magari 8 ya Tanzania na 4 ya Kenya. Magari 4 ya Tanzania yamechomwa moto na madereva wote walichukuliwa na waasi lakini bahati nzuri madereva wawili wa Tanzania walifanikiwa kuwatoroka. Tukio hilo limetokea sehemu inaitwa Kasebebena na Matete, wastani wa kilomita 30 kutoka mji wa Namoya.

TATOA inawashauri wanachama waliopakia mzigo kuelekea huko kuwasiliana na madereva wao ili wasitishe safari, kusubiri taarifa ya hali ya usalama kutolewa.

Mai Mai Kata ni kundi la waasi nchini DRC ambalo linadai kupigania uhuru wa jimbo la Katanga, na linaongozwa na Gédéon Kyungu Mutanga, ambaye aliunda kundi hilo mara tu alipotoroka kutoka gerezani mwaka 2011.


Tumezungumza na mmiliki wa kampuni ya Simba Logistics Mzee Azim Dewji amethibitisha taarifa hizi na tayari tumezungumza na balozi wa Tanzania DRC pamoja na wizara ya mambo ya nje tayari serikali inashughulikia swala hili. Jumla ya gari zilizotekwa ni 12 kati ya hizo gari 8 za Tanzania na 4 za Kenya.

Gari 4 za Tanzania zimechomwa moto na madereva wote walichukuliwa na waasi lakini bahati nzuri madereva wawili wa Tanzania walifanikiwa kuwatoroka. Tukio limetokea sehemu inaitwa Kasebebena na Matete kilometer 30 kutoka mji wa Namoya.

Tunawashauri wanachama waliopakia mzigo kuelekea huko kuwasiliana na madereva wao wasitishe safari ili kusubiri taarifa ya hali ya usalama kutolewa.

Tutazidi kuwapatia update information.

NAMANGA: EDWARD LOWASSA ASIMAMISHWA NA WANANCHI WAMWELEZE UGUMU WA MAISHA


Mh Edward Lowassa Mjumbe wa kamati kuu wa chama Cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA ) na Chama kikuu cha Upinzani TANZANIA na Waziri Mkuu mstaafu amesimamishwa na Wananchi wa Namanga Mpakani mwa Tanzania na Kenya . 

Wananchi wamemueleza Ugumu na ukali wa Maisha walionayo ikiwa ni pamoja na kudorora kwa mzunguko wa fedha mpakani hapo leo hii akiwa safarini Toka Nairobi Kenya alipokwenda kuhudhuria mazishi ya Marehemu Ole Ntimama.

GAVANA BOT AFICHUA SIRI YA KILIO CHA FEDHA KUPOTEA MTAANI


Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Profesa Benno Ndulu jana alitolea ufafanuzi hali ya kiuchumi nchini huku akieleza siri ya kilio kinachovuma cha fedha kupotea mtaani na nyingine zikidaiwa kufichwa.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Profesa Ndulu alisema kuwa kwakuwa taasisi hiyo ndiyo inayofahamu fedha zote zilizopo benki na zilizopo mtaani, inafahamu kuwa hakuna fedha iliyopotea bali fedha zimepotea kwa watu waliokuwa wanazipata kwa njia ya udanganyifu kwakuwa sasa Serikali imebana mianya hiyo.

“Hakuna fedha iliyopotea, Serikali imebana shughuli za watu na ‘mission town’ sasa shughuli zote zinafanywa na Serikali. Hivyo, kwao fedha zimepotea, lakini kwetu hazijapotea,” alisema Profesa Ndulu.

Hata hivyo, Profesa Ndulu alikiri kupungua kwa fedha katika mabenki nchini hali iliyopelekea kupunguza kasi ya utoaji mikopo kwa wananchi. Alisema hali hiyo ilitokana na kuhamishwa fedha za mashirika ya umma na taasisi kutoka benki za biashara kwenda BoT.

“Fedha hizo zitarudi katika benki hizo wakati zitakapopelekwa kwenye Halmashauri kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali,” Profesa Ndulu aliahidi.

Katika hatua nyingine, Gavana huyo wa Benki Kuu alisema kuwa uchumi unatarajiwa kukuwa kwa asilimia 7.2 mwaka huu, huku akibainisha kuwa moja kati ya sababu zinazopelekea ukuaji huo ni  ongezeko la uzalishaji wa umeme na saraju.

Akizungumzia hali ya deni la taifa, alisema kuwa deni la taifa la ndani limeongezeka kutoka shilingi  trilioni 8.6 Mwezi Desemba mwaka jana hadi shilingi trilioni 10 mwezi Juni mwaka huu.

Profesa Ndulu alibainisha kuwa wakati deni linalotokana na kukopa ndani likipaa, deni linatokana na ukopaji wa limepungua baada ya Serikali kupunguza ukopaji nje ya nchi.

EDWARD LOWASSA AMPONGEZA RAISI JOHN POMBE MAGUFULI


Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Edward Lowassa amempongeza Rais Magufuli kwa kuondoa urasimu katika taasisi za serikali na kusema hiyo itasaidia kurejesha utendaji kazi kwa ufanisi.

Lowassa ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na mtangazaji wa BBC, John Nene nchi Kenya ambapo alisema urasimu umepungua na hili amejitahiidi lakini kuna mambo baadhi hayako vizuri.

Lowassa hakuwa tayari kusema ni mambo gani haswa hayakua yakienda sawa lakini alimkosoa Rais Magufuli kwa kile alichodaiwa kuwa analeta dalili za udikteta.

Lowassa alikuwa ni mpinzani mkuu wa Rais Magufuli katika uchaguzi mkuu mwaka 2015 akigombea kupitia CHADEMA na kuungwa mkono na vyama vinavyounda UKAWA.

Amekosoa pia uamuzi wa serikali ya awamu ya tano kupiga marufuku maandamano, mikutano na vikao vya ndani vya vyama siasa huku vyombo vya habari vikifungiwa na wale wote wanamkosoa wakifikishwa mahakamani.

Akielezea Opersheni UKUTA, Lowassa alisema kuwa walipanga kuandamana ili kupinga dalili za udikteta alizoanza kuzionyesha Rais Magufuli.