Ijumaa, 9 Juni 2017

Wema Sepetu Amzimikia Rayvanny Amtabiria Makubwa Tuzo za BET


Wema Sepetu na Raymond

RayVanny ni msanii pekee kutoka Tanzania na Afrika Mashariki ambaye anatuwakilisha kwenye tuzo za BET zitakazofanyika Marekani baadaye mwezi huu akiwania Viewers Choice Awards ama (Pendekezo la Mashabiki ama watazamaji) huku BET wakitangaza namna ya kuwapigia kura wasanii ili washinde tuzo hizo.

Pamoja na baadhi ya mastaa kama Elizabeth Michael kumpigia na kumuombea  kura RayVanny kwenye kurasa zao za Social media, Wema Sepetu naye ametumia ukurasa wake wa Instagram kumpigia kura RayVanny akiandika:

Umechaguliwa tu kuwania lakini kwangu wewe ni mshindi tayari …Unastahili kabisa! V-Vanny Boy. Na haiishii hapa Tuendelee kupiga kura. 
Wasanii wanaowania tuzo ya Viewers Choice Awards pamoja na RayVnanny ni pamoja na  Dave (UK ) Jorja Smith (UK) Amanda Black (South Africa) Changmo (South Korea) Daniel Caesar (Canada) Remi (Australia) Skip Marley (Jamaica).

Mkurugenzi wa Zamani FBI Amlipua Trump..!!!

                       

Aliyekuwa Mkuu wa Shirika la Upelelezi la Marekani (FBI), James Comey ameishtumu Ikulu ya Marekani kwa kumharibia jina na kusema uongo kuhusu shirika hilo.

Comey ambaye aliyefutwa kazi ghafla na Rais Donald Trump alisema hayo jana Alhamisi, baada ya kuanza kutoa ushahidi mbele ya maseneta nchini Marekani kuhusu tuhuma kwamba Urusi iliingilia Uchaguzi Mkuu wa Marekani mwaka uliopita.

Mkuu huyo wa zamani wa FBI amewaambia maseneta waliomhoji kuwa alikuwa na mazungmzo ya siri na Rais Trump. Aidha, ameshtumu matamshi ya Ikulu ya Marekani kuwa FBI ilikosa imani naye.

Trump alimfuta kazi Comey Mei 9, mwaka huu baada ya FBI kutangaza kuchunguza madai ya Urusi kuingilia Uchaguzi wa Marekani, madai ambayo Urusi imekanusha.

Comey amesema, Trump alimwambia asitishe mchakato wa FBI kumchunguza Michael Flynn, aliyekuwa mshauri wake wa masuala ya usalama wa Taifa kwa madai kuwa alikuwa na mawasiliano ya karibu na maofisa wa Urusi kipindi cha uchaguzi.

Duh..Kijana wa Kiume Akamatwa Akimfanyia Mtihani wa Chuo Mpenzi Wake wa Kike..!!!



Imetokea huko Zimbabwe,wote wamekamatwa wapo polisi kijana wa kiume alidai aliamua kumsaidia mpenzi wake maana amerudia mara nne anafeli tu.




Kamanda wa Pwani Afafanua Mauaji ya Watu Watatu..!!!


Kamanda wa Polisi mkoa wa Pwani, Onesmo Lyanga amesema kwa taarifa alizonazo, watu wawili wamepigwa risasi katika kijiji cha Nyamisati, Kibiti, kisha waliofanya uhalifu huo kuwachukua majeruhi na kuondoka nao.

Awali taarifa zilizotolewa na mashuhuda wakazi wa kijiji hicho zilisema watu watatu wameuawa kwa kupigwa risasi usiku wa kuamkia leo.

Lakini akizungumza na Mwananchi leo asubuhi, Kamanda Lyanga amesema watu wawili wamejeruhiwa kwa risasi na wahalifu kutokomea nao kusikojulikana.

“Tunaendelea na uchunguzi.” Amesema Kamanda Lyanga

Ijumaa, 17 Machi 2017

Jinsi ya Kuishi na Mwanamke Asikuloge au Kukupa Limbwata..!!!

                          

Nipo tena kwa Mara nyingine katika kubadilishana uzoefu juu ya mambo mbalimbali yanayohusu mahusiano,kuna jambo limekuwa likiniumiza kichwa sana ni swala zima la kulogwa au kupewa limbwata na mwanamke.

Nidhahiri kabisa mambo haya katika jamii yetu yanafanyika kwa baadhi ya wanawake huwa wanawafanyia wanaume,na tatizo hilo limezidi kushamiri zaidi kutokana na ongezeko kubwa la waganga wa kienyeji.

Nimefanya research kwa baadhi ya waganga wameniambia wateja wao wakubwa ni wanawake na shida kubwa wanayokuwa wanahitaji ni kuolewa au kuwadhibiti wanaume zao.

Nami mekuja kugundua wanaume wengi huwa wanafanyiwa madawa ila wakati mwengine mungu huwalinda hawazuriki bila ya wao kujua na wanaume wengi ambao wapo katika hatari hiyo ni wale wenye kipato kidogo ambacho kinarizisha.

Sasa basi nimejaribu kutafuta prevention za ki psychology, ambanzo hazihusiani na mambo ya kishirikina ambazo zinaweza kukusaidia uepukane na janga hilo nimejaribu kutumia experience yangu ni kama zifuatazo:

Kwanza kabisa kama mwanaume unapoanza mahusiano ya kimapenzi na mwanamke unatakiwa umwambie mwanamke vitu ambavyo huvipendi na moja katika ya vitu ambavyo utamwambia hupendi ni mambo ya kishirikina na unatakiwa umsisitizie kwamba endapo kama wewe utagundua yeye anapenda mambo ya kwenda kwa waganga umwambie siku hiyo ndio itakuwa mwisho wa mapenzi yenu.

Jambo la pili ukiwa unaishi na mwanamke ndani usipende kula chakula peke yako hata kama umechelewa kurudi umerudi labda saa sita usiku mwambie mke wako mle wote chakula cause peke yako hujazoea kula au kama mna mtoto wenu ama ndugu wa mwanamke kula nae chakula.

Kwa kufanya hivyo mwanamke atajua hupendi kula peke yako na unampenda yeye na ndugu zake kumbe unalako moyoni unajilinda na limbwata,jambo la tatu pendelea kufanya ibada ukitaka kula na ukitaka kulala na mshirikishe mkeo katika ibada na wakati mwingine msomee maandiko ya vitabu vya mungu ambayo yanakataza ushirikina na adhabu zake watakazo zipata wanaofanya mambo hayo,mengine mnaweza mkaongezea.

Note:Mwanamke anaweza akawa sio mshirikina lakini akashawishiwa na marafiki zake akufanyie hivyo,kwa hiyo kama mwanaume ni bora ukachukua tahadhari mapema.

Kama Huwezi Kuachana Naye Usijaribu Kuchungulia Mawasiliano Yake....!!!


Kuna siku nilijifanya Mjuaji nikadukua mawasiliano ya mchepuko wangu niliyokutana nayo huko sasa ni hatari tupu, sms ya kwanza kuingia jamaa anampongeza kwa shughuli yao ya jana kuja huku whatsaap shughuli nzito nikajikuta naumwa ghafla pressure inanipanda mara nikaona dunia inazunguka mara nataka kuaga dunia ikabidi majirani zangu wafanye mawasiliano na mchepuko wangu maana walikuwa wanaufahamu ile unakuja home. baby jamani unaumwa nn? aiseeeh nikiuangalia homa inanizidia nikifikiria kuucha siwezi.............kilichoendelea.....................ila mpaka sasa nadunda nao course niliona bora tu nijikaze 

Vijana Tuache tabia ya kudukua mawasiliano ya tunaowapenda wakati jeuri za kuwaacha hatunazo, huo ni ushauri tu kama jasiri endelea kupanga mikakati ya kudukua mawasiliano ya mke au mchumba ako soon tu itabaki story

Alikiba Kuweka Muziki Wake Wasafi.com ni Sawa na Safari ya Mwezini..!!


Kwa takribani miaka mitatu sasa mafahari wawili wa muziki wa kizazi kipya yaani Bongo Flava Alikiba na Diamond Platinumz wamekuwa katika bifu zito sana, licha ya wao kujaribu kila siku kuukwepa ukweli huo. Hakuna kati yao ambaye amewahi kujitokeza hadharani na kukiri uhasama kati yao lakini ni wazi kuwa watu hawa hawapikiki chungu kimoja.

Mara kwa mara watu wa karibu wa Diamond wakiwemo watu walio kwenye management yake hususan, mameneja Sallam na Ricardo Momo, wamekuwa wakimtupia vijembe Alikiba. “Wao wakipost tembo, sisi tunapost show” na “waambie dada zao Kariakoo waje Ulaya” ni baadhi tu ya mistari ambayo Diamond amewahi kusikika akiimba ikiwa ni kuelekeza mashambulizi upande wa Alikiba na kambi yake.

Hivi karibuni Diamond akiwa kwenye Interview ya kipindi cha 360 cha Clouds FM, alikaririwa akisema kuwa hana tatizo na Alikiba, ni mtu anayeheshimiana naye na hata uongozi wake uko katika mazungumzo na uongozi wa Alikiba ili Kiba aweze kuuza nyimbo zake kwenye mtandao wa wasafidotcom ambao ni mradi mpya wa Diamond.

Baadaye usiku kupitia akaunti yake ya Instagram Alikiba aliandika caption zenye utata zilizotafsiriwa na mashabiki na wadau mbalimbali kuwa zimelenga kujibu maneno hayo ya Diamond Platnumz.

Wamarekani wana sera zao mbili ambazo wanazitumia sana katika kulifanya taifa lao kuendelea kuwa taifa kubwa duniani. Sera ya kwanza; njia pekee ya kumshinda adui ni kumfanya rafiki, ya pili; wamarekani hawahitaji rafiki dhati wala adui kweli, zaidi ni kutimiza interest zao.

Hivyo watakufanya rafiki ili wapate watakacho na utarudi kuwa adui wakishatimiza azma yao. Lakini Waingereza pia wanasema numbers don’t lie. Nimejaribu kufuatilia rekodi za nyuma za Alikiba katika mtandao wa mkito.com nikagundua kuwa Alikiba ni record breaker. Mwana iliweka rekodi, Chekecha Cheketua iliweka rekodi. Hata nyimbo ya Nisamehe aliyoshirikishwa na Barakah Da Prince pamoja na nyimbo ya Kajiandae aliyoshirikishwa na Ommy Dimpoz zimeingia kwenye Top 5 ya ngoma zilizopakuliwa zaidi kwenye mtandao wa Mkito mwaka 2016.

Kwa rekodu hizi ni dhahiri Diamond anahitaji amani na Alikiba kwasababu za kibiashara zaidi. Anatambua fan base aliyonayo Alikiba itabust zaidi mtandao wake, pesa atakayopata ni kubwa, pia number of visitors itaongezeka kwa kasi kwani kila mtu atataka kuamini ni kweli Ali yumo? Haikushangaza kuona editing kwenye mitandao ikionesha kua profile ya Alikiba ipo kwenye wasafidotcom.

Kwa hali ilivyo sioni na sidhani kama management ya Alikiba itaweza kukubali kuuza nyimbo kwenye mtandao wa Diamond. Kwanza wanajiamini sababu wameshauza kabla na kuweza kuweka baadhi ya rekodi kwenye mtandao wa Mkito. Pili kutoka kwa mfululizo wa mashambulizi ya maneno kutoka kwa Dimond na management yake kwenda kwa Alikiba itakuwa ni fedheha kubwa kwa mashabiki wa Ali kama Ali na uongozi wake utakubaliana na suala hili. Na ndio maana nasema sera za kimarekani za Dimond zimedunda kwa Alikiba