Taasisi ya mwalimu Nyerere imeitaka tume ya uchaguzi ya Zanzibar ZEC
kufanya kazi kwa kuzingatia katiba ya nchi na sheria na sio kutanguliza
mbele maslahi binafsi ya kisiasa hatua ambayo inaweza kusababisha
machafuko na umwagaji wa damu.
Akizungumza na vyombo vya habari mjini Musoma, mkurugenzi mtendaji wa
taasisi hiyo mzee Joseph Butiku, amesema amekerwa na tabia ya ZEC
kusitisha uchaguzi na kushindwa kuwatangazia wananchi kiongozi wao
waliomchagua, huku ikishindwa kuheshimu matakwa ya wananchi waliopiga
kura katika visiwa vya Zanzibar.
Aidha mzee Butiku amewataka wananchi wa Zanzibar kutokubali tena kurudia
upigaji wa kura hadi hapo yatakapotolewa maelezo ya kuridhisha na
wahusika waliosababisha uchaguzi huo kufutwa pia waweze kuchukuliwa
hatua kali za kisheria
Kwa sababu hiyo amewataka viongozi kuheshimu sheria na katiba ya nchi na
kwamba chama ambacho kinadhani kimeshindwa katika uchaguzi huo kikubali
matokeo badala ya kuifanya zanzibar ni mali ya chama fulani pekeee.
Jumapili, 1 Novemba 2015
Home »
» BUTIKU: WAZANZIBAR MSIKUBALI KURUDIA UCHAGUZI
0 comments:
Chapisha Maoni