Watu sita wamefariki dunia baada ya gari ndogo waliokuwa wakisafiria
kugongana uso kwa uso na basi la abiria mali ya kampuni ya Princess
Muro, lililokuwa likitokea Dar es salaam kuelekea Tunduma, katika eneo
la hifadhi ya taifa ya Mikumi, barabara kuu ya Morogoro-Iringa.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro Leonard Paulo amethibitisha kutokea
kwa ajali hiyo katika eneo la hifadhi ya taifa ya Mikumi, ikihusisha
gari ndogo la abiria aina ya Toyota Noah lenye namba za usajili T 359
BBA iliyokuwa imebeba abiria sita wakiwemo wanawake wawili na wanaume
wanne ambayo ilipasuka tairi ya Mbele ya kuyumba ovyo barabarani na
kugongana na basi hilo la Princess Muro lenye namba T 160 BBC na
kusababisha vifo kwa abiria wote wa Noah.
Amesema basi hilo la abiria aina ya Zangton lililoharibika zaidi mbele
huku Noah ikiharibika kabisa, likuwa likiendeshwa na Silos Wilfred (55)
mkazi wa Mbeya ambaye anahojiwa na polisi kuhusiana na tukio hilo, na
kwamba basi alilokuwa akiendesha lilikuwa na abiria 59 ambao hawakupata
madhara makubwa, isipokuwa michubuko kidogo kwa baadhi yao na
walitafutiwa usafiri kuendelea na safari.
Katika upekuzi wa miili ya abiria waliokuwa kwenye Noah inayodaiwa
kuhusika na ubebaji wa magazeti, viligundulika vitambulisho vimne vya
Ali Nduti Mohamed (27), mkazi wa Mbeya,Sani Elion Mkwabe (24) mkazi wa
Kunduchi, Patrick Mkelegene (43) mkazi wa Buguruni Malapa na Selemani
Omary (30) ambaye makazi yake hàyajaweza kujulikana Mara moja.
Miili ya watu hao waliopoteza maisha imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro.
Jumapili, 1 Novemba 2015
Home »
» Watu Sita Wapoteza Maisha Katika Ajali ya Gari Morogoro
Watu Sita Wapoteza Maisha Katika Ajali ya Gari Morogoro
Related Posts:
Ban Ki Moon asema Iraq inapaswa kuunda serikali ya umoja wa kitaifa Watu waliokuwa na silaha wameushambulia msafara uliokuwa umewabeba wafungwa kaskazini mwa mji mkuu wa Iraq, Baghdad, na kusababisha makabiliano makali na majeshi. Wafungwa zaidi ya 50 na wanajeshi kumi wameuawa katika sha… Read More
AJARI YA GARI WALIYOPATA WAIMBAJI WA NYIMBO ZA INJIRI AKIWEMO BAHATI BUKUKU. Gari lenye namba IT 7945 Toyota Nadia likiendeshwa na EDSON MWAKABUNGU (31) mkazi wa Tabata Dar es Salaam liliacha njia na kugonga gema na kusababisha majeraha kwa watu watatu baada ya kugongwa na gari jingine … Read More
Ndege ya abiria ya Algeria yaripotiwa kuanguka kaskazini mwa Mali Maafisa wa Jeshi wa Burkina faso wamesema ndege hiyo iliyokuwa chini ya shirika la ndege la Algeria imeanguka karibia kilomita 50 kutoka mpaka wa Burkanafaso. Waongoza ndege wali… Read More
KAMPENI YA UGAWAJI WA VYANDARAU VYA HATI PUNGUZO Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii imeandaa kampeni kwa ajili ya ugawaji wa vyandarua vya hati punguzo katika kaya nchini, inayotarajiwa kuanza mwezi Aprili mwaka 2015. Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini … Read More
Mnigeria aliebeba dawa za kulevya alivyokamatwa Nairobi baada ya rubani kuugua.Mwanamume mmoja Raia wa Nigeria imebidi alazwe kwenye hospitali ya taifa ya Kenyatta Nairobi Kenya baada ya kugundulika alikua na mzigo wa dawa za kulevya wa vidonge 57 tumboni mwake. Huyu jamaa alikua anazisafirisha hizi… Read More
0 comments:
Chapisha Maoni