BAADHI ya vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani Bunda wamemtuhumu
 mwenyekiti wa chama hicho wilayani hapa, Chacha Gimanwa, kwamba 
alichangia jimbo la Bunda Mjini kuchukuliwa na mgombea wa Chama cha 
Demokrasia na Maendeleo (Chadema) katika uchaguzi mkuu uliofanyika 
Oktoba 25 mwaka huu.
Vijana hao walitoa tuhuma hizo, juzi wakati wakitembea matembezi ya 
amani ya kushangilia ushindi wa mgombea urais wa CCM, Dk Jonh Magufuli 
katika mitaa mbalimbali ya mji wa Bunda.
Katika uchaguzi mkuu uliopita CCM ilipoteza jimbo hilo, baada ya Stephen
 Wasira aliyekuwa akitetea kiti hicho kushindwa na mgombea wa Chadema, 
Ester Bulaya.
Hata hivyo Wasira ambaye pia ni Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika 
hivi karibuni akizungumza na waandishi wa habari jijini Mwanza alidai 
kuwa katika uchaguzi huo kulikuwa na hujuma.
Wanachama hao wa CCM wakiwa wamebeba mabango baadhi yao walisikika 
wakimtaja moja kwa moja Gimanwa kwamba ndiye alisababisha CCM kushindwa 
katika jimbo hilo na kuomba uongozi wa juu wa chama hicho umchukulie 
hatua.
Hata hivyo, Gimanwa akizungumza na mtandao huu kwa njia ya simu jana 
alisema kuwa tuhuma hizo hazina msingi wowote na kwamba kamwe hawezi 
kukihujumu chama chake.
“Hicho ni kikundi cha watu wachache tu wanaotaka kuniharibia jina.Mimi 
kura yangu ni moja na wapiga kura ni wengi, sasa iweje mimi nisababishe 
mgombea wa jimbo la Bunda mjini ashindwe?” Alihoji.
 Alisema yeye kama mwenyekiti wa CCM alikuwa akifanya kampeni pia katika
 jimbo la Bunda vijijini, na siku tatu kabla ya uchaguzi mkuu alirudi 
tena Bunda mjini na kuendelea na kampeni.
Jumapili, 1 Novemba 2015
Home »
 » CCM Washikana 'Uchawi' Baada ya Kulipoteza Jimbo La Bunda







 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
0 comments:
Chapisha Maoni