Siku chache zilizopita wafanyakazi wa
kiwanda cha nguo cha urafiki walifanya mgomo kwa madai ya kutolipwa
mishahara yao kwa muda mrefu kupelekea mkuu wa wilaya ya Kinondoni, DC Paul Makonda kuagiza
shughuli zote za kiwanda hicho zisimame mpaka mgogoro wa kimaslahi kati
ya wafanyakazi na wamiliki wa kiwanda hicho utakapotatuliwa.
Sasa leo kupitia kwenye ukurasa wa
instagram DC Paul Makonda aliandika maneno kuhusu namna alivyotatua
mgogoro huo na kufanikisha kile kiasi wanachotakiwa kulipwa
wafanyakazi kiwanda cha nguo cha URAFIKI kilichopo eneo la Shekilango Dar es Salaam.
‘Asante
Mungu kwa kuniwezesha kuwatetea wanyonge wenzangu na wafanyakazi wa
kiwanda cha urafiki na kufikia kulipwa kiwango 150000 tofauti na hapo
zamani walipokuwa wanalipwa 80000 kwa mwezi….Jambo ambalo wameliomba
tangu 2007′>>>>Paul Makonda
0 comments:
Chapisha Maoni