WIZARA ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto imekiri 
kwamba mashine ya CT Scan iliyofungwa katika Hospitali ya Taifa ya 
Muhimbili ilikuwa ni ya kituo cha kisasa cha kutolea huduma za afya cha 
Benjamin Mkapa kilichopo katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).
Akijibu swali la nyongeza bungeni mjini Dodoma, Naibu Waziri wa Afya, 
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Khamis Kigwangalla 
alisema mashine hiyo iliingia nchini kwa lengo la kupelekwa katika kituo
 hicho lakini ikapelekwa Muhimbili kutokana na kutokamilika kwa majengo 
ya kufungwa mashine hiyo katika kituo hicho.
Alisema, uamuzi huo waliuchukua pia kwa sababu hela ya kununua mashine 
nyingine ambayo itapelekwa kufungwa katika kituo hicho ilikuwepo na kwa 
sasa mchakato wa ununuzi unaendelea.
Dk Kigwangalla alikuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Chemba, 
Juma Nkamia (CCM) aliyetaka jibu la Serikali kama ni kweli ilichukua 
mashine ya kituo hicho na kufunga katika Hospitali ya Taifa Muhimbili 
ama ilinunua.
Awali katika swali la msingi msingi, Nkamia alitaka kujua mpango wa 
Serikali wa kununua mashine mpya ya CT -Scan kwa ajili ya Hospitali ya 
Taifa Muhimbili.
 Kuhusu hilo, Dk Kigwangalla alisema, Desemba mwaka jana Serikali 
ilipeleka mashine ya CT-Scan katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili 
ambayo inatumia teknolojia ya kisasa yenye X-ray tube mbili na uwezo wa 
kupiga picha ya 128 slice mara mbili.
Ijumaa, 5 Februari 2016
Home »
 » Imebainika Mashine ya CT Scan Iliyofungwa Muhimbili Hospital ni ya Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) 







 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
0 comments:
Chapisha Maoni