KIMUHEMUHE kilitanda kwenye viunga vya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu 
leo  Feb 17, 2017, kufuatia ndugu, jamaa na marafiki wa model, Agness 
Masogange kufurika huku wakitarajia kumuona ndugu yao huyo akifikishwa 
mahakamani hapo .
Ndugu hao waliwasili Kisutu mapema asubuhi na kuweka kambi mahakami ili 
kusikiliza kesi ya masogange anayehusishwa na tuhuma za matumizi ya dawa
 za kuleya.
Licha ya Masogange kutokufikishwa mahakamani hapo kwa kile kinachodaiwa 
kuwa majibu ya Mkemia Mkuu wa Serikali kuhusu kipimo endapo mwanadada 
huyo anatumia madawa ya kulevya, kilikuwa hakijatoka lakini mpaka 
ilipotimu majira ya saa 9:00 mchana, ndugu hao walikuwa hawajakata 
tamaa. Baada ya kuona hakuna dalili zozote kwa ndugu yao kuletwa 
mahakamani hapo huku muda wa mahakama wa saa 9:30 ukiisha, ndipo ndugu 
hao waliamua kuondoka kwa unyonge eneo la Kisutu.
Taarifa iliyotolewa jana na Kamnada wa Polisi Kanda Maalum ya Dar, 
Kamishna Somon Sirro ilieleza kuwa, Masogange na wenzake 17, 
wanashikiliwa na jeshi hilo kwa tuhuma za kuhusika na matumizi ya dawa 
za kulevya, na kwamba jana walipelekwa kwa Mkemia Mkuu wa Serkali kwa 
ajili ya vipimo na endapo ikibainika wanatumia madawa ya kulevya, leo 
Ijumaa au Jumatatu ijayo watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma 
zinazowakabili.







 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
0 comments:
Chapisha Maoni