Naibu Waziri Wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Dkt.
Hamis Kigwangalla amesema kuwa atawaweka hadharani wanaume wote
wanaojihusisha na mapenzi ya jinsi moja (mashoga) ambao hufanya biashara
hiyo kupitia mitandao ya kijamii.
Naibu Waziri aliyasema hao jana usiku kupitia ukurasa wake wa Twitter
ambapo alieleza kuwa yupo katika ziara jimboni kwake na mara
atakaporejea jijini Dar es Salaam kabla ya kuhamia Dodoma rasmi ataiweka
orodha hiyo hadharani.
Aidha, amesema kuwa wale wote wanaodhani kuwa vita dhidi ya wanaume
wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja ni mzaha, wataona hali
itakavyokuwa kwani vita hiyo ni kubwa sana na wataishinda.
Kigwangalla ambaye pia ni mtaalamu wa afya alisema kuwa suala la mtu
kuwa shoga si suala la kibaolojia (asili) bali ni watu tu kujiendekeza
na hivyo watakahikikisha wanalikomesha.
Sheria ya ndoa ya Tanzania inapinga watu wa jinsia moja kujihusisha na
mahusiano ya kimapenzi, lakini pia ni kitu kilichozuiliwa katika vitabu
vitakatifu vya dini.
Dr. Kigwangalla,
Uchunguzi dhidi ya watuhumiwa wa ushoga unaendelea. Watakamatwa kimya
kimya! Serikali ina mkono mrefu. Wakipatikana watatusaidia wenza wao!
Dr. Kigwangalla,
Kuna watu wanadhani vita dhidi ya ushoga ni ya mzaha, ni vita kubwa na
tutaishinda. Mtandao ni mrefu na nitaendesha operation kamata kamata!
Dr. Kigwangalla, H.
Namalizia ziara jimboni. Nikirudi Dar, kabla ya kuhamia rasmi Dodoma,
nitaweka wazi orodha ya watuhumiwa wa ushoga wanaojiuza mitandaoni!
Dr. Kigwangalla, H.
Kuna nchi marafiki zetu zinafanya jitihada za kupenyeza ushoga Tanzania
na kudai ni haki ya binadamu kuchagua ampendaye, sisi tunasema NO!
Dr. Kigwangalla, H.
Ushoga hauna addiction wala siyo wa kuzaliwa nao, wanaofanya hivyo
wanajiendekeza tu! Ushoga siyo biological. Mashoga wote waache mara moja
Jumatano, 15 Februari 2017
Home »
» Naibu Waziri wa Afya kuweka hadharani majina ya mashoga Dar es Salaam
Naibu Waziri wa Afya kuweka hadharani majina ya mashoga Dar es Salaam
Related Posts:
HATIMA YA TORRES CHELSEA;HIKI NDICHO ALICHOKISEMA Fernando Torres amemaliza kipindi kigumu kabisa cha miaka mitatu na nusu kwenye maisha yake ndani ya klabu ya Chelsea baada ya kukubali kuondoka katika timu hiyo. Fernando alijiunga na Chelsea mnamo mwaka 2011 January kw… Read More
Je Toni Kroos ndio kamkimbiza Alonso Madrid? Xab Alonso ajibu.Kiungo wa kimataifa wa Spain Xabi Alonso amejiunga na klabu ya FC Bayern Munich ya Ujerumani akitokea kwa mabingwa wa ulaya Real Madrid kwa ada ya uhamisho wa paundi millioni 5. Alonso ambaye alijunga na Real Madrid… Read More
Baada ya Okwi kutangaza kujiunga na Simba,hiki ndicho walichokifanya Yanga. Ikiwa imepita siku moja toka klabu ya Simba kumtangaza Emmanuel Okwi kama mchezaji wao rasmi wa klabu hiyo,taarifa nyingine iliyotolewa leo na uongozi wa Yanga ni kumshitaki Okwi. Klabu ya Young Africans imemshitaki Emman… Read More
Dr. Hamisi Kigwangalla atangaza nia ya kugombea Urais 2015, zisome hapa points zake. September 7 2014 Dr. Hamisi ambae ni mbunge wa Nzega kwa ruhusa ya CCM alikutana na Waandishi Dar es salaam akiwa ameongozana na mke wake pamoja na watoto wao na kisha kuweka wazi kwamba yuko tayari kugombea k… Read More
BAADA YA OKWI KUIDHINISHWA SIMBA, HIKI NDIO WALICHOAMUA YANGU Siku moja baada ya shirikisho la soka nchini TFF kumtangaza mchezaji Emmanuel Okwi kuwa huru na hivyo anaweza kusajiliwa na klabu ya Simba – leo hii uongozi wa klabu ya Yanga umeitisha mkutano wa waandishi wa h… Read More
0 comments:
Chapisha Maoni