Alhamisi, 15 Septemba 2016

GAVANA BOT AFICHUA SIRI YA KILIO CHA FEDHA KUPOTEA MTAANI


Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Profesa Benno Ndulu jana alitolea ufafanuzi hali ya kiuchumi nchini huku akieleza siri ya kilio kinachovuma cha fedha kupotea mtaani na nyingine zikidaiwa kufichwa.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Profesa Ndulu alisema kuwa kwakuwa taasisi hiyo ndiyo inayofahamu fedha zote zilizopo benki na zilizopo mtaani, inafahamu kuwa hakuna fedha iliyopotea bali fedha zimepotea kwa watu waliokuwa wanazipata kwa njia ya udanganyifu kwakuwa sasa Serikali imebana mianya hiyo.

“Hakuna fedha iliyopotea, Serikali imebana shughuli za watu na ‘mission town’ sasa shughuli zote zinafanywa na Serikali. Hivyo, kwao fedha zimepotea, lakini kwetu hazijapotea,” alisema Profesa Ndulu.

Hata hivyo, Profesa Ndulu alikiri kupungua kwa fedha katika mabenki nchini hali iliyopelekea kupunguza kasi ya utoaji mikopo kwa wananchi. Alisema hali hiyo ilitokana na kuhamishwa fedha za mashirika ya umma na taasisi kutoka benki za biashara kwenda BoT.

“Fedha hizo zitarudi katika benki hizo wakati zitakapopelekwa kwenye Halmashauri kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali,” Profesa Ndulu aliahidi.

Katika hatua nyingine, Gavana huyo wa Benki Kuu alisema kuwa uchumi unatarajiwa kukuwa kwa asilimia 7.2 mwaka huu, huku akibainisha kuwa moja kati ya sababu zinazopelekea ukuaji huo ni  ongezeko la uzalishaji wa umeme na saraju.

Akizungumzia hali ya deni la taifa, alisema kuwa deni la taifa la ndani limeongezeka kutoka shilingi  trilioni 8.6 Mwezi Desemba mwaka jana hadi shilingi trilioni 10 mwezi Juni mwaka huu.

Profesa Ndulu alibainisha kuwa wakati deni linalotokana na kukopa ndani likipaa, deni linatokana na ukopaji wa limepungua baada ya Serikali kupunguza ukopaji nje ya nchi.

EDWARD LOWASSA AMPONGEZA RAISI JOHN POMBE MAGUFULI


Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Edward Lowassa amempongeza Rais Magufuli kwa kuondoa urasimu katika taasisi za serikali na kusema hiyo itasaidia kurejesha utendaji kazi kwa ufanisi.

Lowassa ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na mtangazaji wa BBC, John Nene nchi Kenya ambapo alisema urasimu umepungua na hili amejitahiidi lakini kuna mambo baadhi hayako vizuri.

Lowassa hakuwa tayari kusema ni mambo gani haswa hayakua yakienda sawa lakini alimkosoa Rais Magufuli kwa kile alichodaiwa kuwa analeta dalili za udikteta.

Lowassa alikuwa ni mpinzani mkuu wa Rais Magufuli katika uchaguzi mkuu mwaka 2015 akigombea kupitia CHADEMA na kuungwa mkono na vyama vinavyounda UKAWA.

Amekosoa pia uamuzi wa serikali ya awamu ya tano kupiga marufuku maandamano, mikutano na vikao vya ndani vya vyama siasa huku vyombo vya habari vikifungiwa na wale wote wanamkosoa wakifikishwa mahakamani.

Akielezea Opersheni UKUTA, Lowassa alisema kuwa walipanga kuandamana ili kupinga dalili za udikteta alizoanza kuzionyesha Rais Magufuli.

DADA WA DAIMOND ESMA PLATNUMZ AKIRI KUMPENDA SANA PETIT MAN AWAOMBA NYAKU NYAKU WASIMNYAKUE



Dada wa Diamond ameamua kufunguka ya moyoni na kudai anampenda sana mume wake Petit Man ambae walitengana kwa muda kutokana na kutokuelewa hapa na pale lakini kwa sasa inaonekana wameweka mambo sawa...Ameandika haya kwenye ukurasa wake

_esmaplatnumz
Baby dady mkimuona mwambieni mi Nampenda tuu ukiniuliza hata sijui... kuna wakati unaweza kufichaficha au kujionesha hupendi au ukajikaza usiseme unachojisikia kusema but mi naona bora uwe muwazi ili roho yako Iwe na Amani... Jamani mi Nampenda huyu kaka plz nyakunyaku kuweni makini huyu mi nahisi km kafika kigoma mwisho wa reli...na natania msije nikomoa...hamchelewi...

FAIZA ALLY AFUNGUKA KUMPENDA SUGU KUTOKA MOYONI..ADAI HAOGOPI KUCHEKWA KWA KIGEUGEU CHAKE


Faiza Ally Amefunguka haya Katika ukurasa wake wa Instagram:



Leo nimeamka akili yangu inawaza mapenzi tu... Mkatae mkubali mapenzi yana nafasi kubwa sana ktk maisha... Na mapenzi hayana baunsa...😅 Mimi nampenda sana baba mtoto wangu - Nina mpenzi yes lkn nampenda yeye zaidi - ana mpenzi Sawa lkn hainizui kuongea hisia zangu... Nachekwa Sawa lkn wanao nicheka hawako ktk maisha yangu Kwa hiyo sio muhimu sana na sioni aibu kusema hisia zangu Kwa mtu ninae mpenda... Nampenda Kila siku Kila mwaka Na sijui nta Acha lini kumpenda.... Ila naamini Kama Mungu alivyo mleta-alivyo muondoa Ndio atakavyo nisahaulisha Na kuniletea mwingine au pengine kum rudisha .... Mapenzi kwangu yana sound hivi➡️➡️➡️➡️ muonyesha unampenda - ajue unampenda- kuwa mkweli- usimuogope- simama Kwenye ukweli- kuwa halisi Na uache maisha yaendelee - usilazimishe- usijikaze -usijifiche- usijifanye ..... Mimi ni Karatasi jeupe nisome lkn ni hiari yako kunielewa sio lzm unielewe lkn mwisho wa siku silazimishi yote heri ..... Nakupenda sana baba mtoto - pengine una niona uchafu au sina dhamani lkn moyo wangu ndio ume kuchagua - usinihukumu -usinichukie iko siku Mungu ataleta heri zake ntakusahau utapata Amani Na mpenzi wako Na mm Na wangu au labda ntakufa hutanisikia Tena ila Kwa sasa Naomba uniache vile najisikia .....Nakupenda Joseph Tanzania inajua.... Mama yangu anajua... Mtoto wetu anajua na nitaka dunia ijueeeeeeeeeee😭 Nakupenda sanaaaaa baba Sasha - usiniulize Kwa nini.... mm mwenyewe sijui Nakupenda tu hivyo yani ........ Tag him mwambie mama Sasha anakupenda zaidi Kila siku Na hakunaga Na sizani Na Kama unapendwa zaidi ya ninavyo kupenda ! Na Kama unapendwa Basi una bahati sana mshukuru Mungu Maana Natamani kupendwa Kama ninavyo kupendwa.....💔💔💔 Acha nichoreke haina kwere kuchoreka Kwa ninae mpenda sio kesi ...😭

WASANII NA VIONGOZI WA WCB WAALIKWA NYUMBANI KWA RAISI MSTAAFU JAKAYA KIKWETE


Rais mstaafu wa awamu ya nne Jakaya Kikwete Jumatano hii aliwaalika wasanii wa label ya WCB pamoja na viongozi nyumbani kwake na kula nao chakula cha mchana. JK ambaye ni mmoja kati ya marais ambaye amesupport sana wasanii wa muziki nchini, aliwaalika wasanii hao nyumbani kwake na kuzungumza nao mambo mbalimbali kuhusu muziki wao. Mmoja kati ya viongozi wa juu wa label hiyo, Sallam alimshukuru rais huyo kwa kuwaalika nyumbani kwake na kuzungumza nao mawili matatu kuhusu muziki. 
 “Former President JM Kikwete and Former First Lady Mama Salma Kikwete. Asanteni kwa mwaliko wenu!! Allah awape afya njema,” Sallam aliandika instagram.

Ijumaa, 1 Julai 2016

MAHAKAMA YA MAFISADI KUANZA RASMI LEO

MAHAKAMA Maalumu ya kushughulikia Makosa ya Rushwa na Ufisadi, inaanza rasmi leo Julai mosi.

Pamoja na kuanza kwa mahakama hiyo, serikali imeanza mchakato kuifanyia marekebisho Sheria Namba 11 ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini ya Mwaka 2007 ili kuongeza ukubwa wa adhabu zinazotolewa sasa.

Mahakama hiyo iliyoahidiwa na Rais John Magufuli wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 na imo katika Ilani ya Uchaguzi wa Chama Cha Mapinduzi, itaimarisha zaidi taasisi za uwajibikaji zinazohusika na mapambano dhidi ya rushwa.Ahadi hiyo ambayo inatimizwa ndani ya kipindi cha miezi isiyozidi saba tangu Serikali ya Awamu ya Tano iingie madarakani ni sehemu ya mapambano ya kujenga misingi ya uchumi kwa kudhibiti rushwa na mianya yake na kuleta uwajibikaji.

Akiahirisha Bunge jana mjini hapa, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alisema utekelezaji wa ahadi hiyo unakwenda sambamba na kuonesha dhamira ya serikali ya kushughulikia makosa ya rushwa na kuweka misingi imara ya uwajibikaji katika sekta zote.

“Mahakama itawafanya watu waliozoea rushwa na ufisadi kujiuliza mara mbili kabla ya kufanya uhalifu huo yaani kuwa deterrent,” alisema Waziri Mkuu na kuongeza kuwa kuwapo kwake kutahamasisha wafanyabiashara kufanya shughuli zao bila shaka huku umuhimu kwao, ikiwa ni kulipa kodi.

Akielezea umuhimu wa mahakama hiyo, alisema kwamba itasaidia kuendeleza nia ya serikali ya watu kulipa kodi kwa maendeleo ya taifa.

Jiunge nasi  Insta@ubuyuhotz ,fb@ubuyuhotz


Jumapili, 5 Juni 2016

UN WAKUNWA NA KASI YA JPM


SHIRIKA la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), limeeleza kuridhishwa kwake na utendaji wa Rais John Magufuli katika mapambano ya rushwa, kuongeza uwajibikaji na ukusanyaji wa mapato.
Mwakilishi Mkazi wa UNDP nchini, Alvaro Rodriguez, alisema hayo jana katika semina ya wabunge kuhusu Malengo 17 ya Maendeleo Endelevu ya Dunia.
Alisema Serikali ya Awamu ya Tano, imekuwa ikipambana na rushwa na kusimamia kwa karibu ukusanyaji mapato, hali aliyosema itasaidia maendeleo kwa kuwa hakuna nchi iliyoendelea bila kuchapakazi.
Rodriguez alisema mbali na kuona maendeleo katika baadhi ya mikoa na mitaa, ameona jitihada hizo za Serikali na amefurahishwa na kuridhika nazo.
Mwakilishi huyo pia alisema Serikali ya Tanzania na Ofisi ya Umoja wa Mataifa (UN), zimekuwa zikifanya kazi pamoja katika harakati za usambazaji wa malengo ya dunia kwa Watanzania.
Alisisitiza umuhimu wa malengo hayo kueleweka kwa wabunge, ili katika jukumu lao la kuisimamia Serikali, wawe mabalozi wa utekelezaji wa malengo hayo katika ufuatiliaji kwenye ngazi zote za utawala.