Jumamosi, 30 Agosti 2014

Baada ya Okwi kutangaza kujiunga na Simba,hiki ndicho walichokifanya Yanga.

Screen Shot 2014-08-29 at 10.23.35 PM
Ikiwa imepita siku moja toka klabu ya Simba kumtangaza Emmanuel Okwi kama mchezaji wao rasmi wa klabu hiyo,taarifa nyingine iliyotolewa leo na uongozi wa Yanga ni kumshitaki Okwi.
Klabu ya Young Africans imemshitaki Emmanuel Okwi kwenye Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na kuwasilisha nakala kwa shirikisho la soka Barani Afrika (CAF) na shirikisho la soka duniani (FIFA) kwa kuingia mkataba na timu nyingine wakati akiwa bado ana mkataba wa miaka miwili na Yanga.

Je Toni Kroos ndio kamkimbiza Alonso Madrid? Xab Alonso ajibu.

toni-kross_1tw36alx3nokv1ra9kbdulb1wxKiungo wa kimataifa wa Spain  Xabi Alonso amejiunga na klabu ya FC Bayern Munich ya Ujerumani akitokea kwa mabingwa wa ulaya Real Madrid kwa ada ya uhamisho wa paundi millioni 5.
Alonso ambaye alijunga na Real Madrid akitokea Liverpool ametambulishwa rasmi leo hii kwenye mkutano waandishi wa habari na kutoa sababu ambayo imemfanya mpaka akaamua kuondoka Santiago Bernabeu.
Kiungo huyo ambaye juzi alitangaza kujiuzulu kuichezea timu ya taifa ya Hispania amesema kwamba kilichomfanya kuhama Madrid sio upinzani wa namba kama inavyodhaniwa na wengi. 
“Klabu haikutaka niondoke, ulikuwa uamuzi wangu mwenyewe kuondoka. Baada ya kushinda La Decima, nilihisi nahitaji changamoto mpya. Nilihisi muda wa kuondoka umefika,” Alonso aliwaambia waandishi wa habari.
“Sikuamua kuondoka kwa sababu ya ujio wa Toni Kroos. Madrid wamefanya usajili mzuri sana na tungecheza wote kwa muda mwingi. Hivyo sikuondoka kwa sababu yake, nilihitaji tu changamoto mpya.
“Bayern ndio lilikuwa chaguo sahih kwangu mimi.” – Alonso

HATIMA YA TORRES CHELSEA;HIKI NDICHO ALICHOKISEMA

IMG_6865.JPG
Fernando Torres amemaliza kipindi kigumu kabisa cha miaka mitatu na nusu kwenye maisha yake ndani ya klabu ya Chelsea baada ya kukubali kuondoka katika timu hiyo.
Fernando alijiunga na Chelsea mnamo mwaka 2011 January kwa ada ya uhamisho ambayo ilivunja rekodi ya usajili nchini Uingereza – £50m akitokea Liverpool – leo hii imethibitishwa rasmi kwamba mchezaji huyo sasa anajiunga na klabu ya AC Milan ya Italia kwa mkataba wa mkopo wa miaka miwili.
Torres anajiunga na AC Milan kwenda kurithi nafasi ya Mario Balotelli ambaye amejiunga na Liverpool kwa ada ya uhamisho wa £16m.
Torres ameichezea Chelsea mechi 172 na kufanikiwa kuifungia magoli 45 tangu alipotia mguu Stamford Bridge.
Mchezaji huyo anategemewa kutua Milan leo tayari kufanyiwa vipiko vya afya.

Na hii ni nyingine tena! Wasanii walioandamana nusu uchi Nairobi Kenya.

34 
Siku hizi ishu ya kuvua nguo kuonyesha msisitizo au kulipigia kelele jambo flani imekua kawaida, yani wengi wameitumia hii njia kufikisha malalamiko yao na mfano mzuri ni hivi karibuni kwa Wanafunzi wa kike kwenye shule ya sekondari ya Wasichana Tabora Tanzania kubaki nusu uchi kwa nia ya kupigia kelele matatizo ya shule ikiwemo maji.

Nchi jirani ya Kenya matukio kama haya yamekua mengi pia lakini hawa ndio wamechukua headlines kwa kuwa Wanamuziki wa kwanza kuandamana kwa aina hii.
Ripota wa TZA Kenya Julius Kepkoich amesema Wasanii hawa waliandamana nje ya ofisi za Nation Media Nairobi wakiwa nusu uchi kulalamikia nyimbo zao kutochezwa na vyombo vya habari.
Wakiwa na mabango yao Wasanii hawa kutoka maeneo ya Vitongojini walisema wanaumizwa na kitendo cha nyimbo zao kutochezwa, wamekua wakitoa nyimbo mpya kila wakati lakini hazichezwi kwenye Radio wala TV badala yake zinazochezwa ni za wasanii walewale kila siku.
35

Alhamisi, 21 Agosti 2014

VIONGOZI WATUMIA MADARAKA YAO KUJINUFAISHA

Mstaafu wa Awamu ya Pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi (katikati) akifungua semina ya majadiliano kati ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma na wanahabari waliojadili rasimu ya Sheria Mpya ya Kudhibiti Mgongano wa Maslahi kwa Viongozi wa umma.
Mstaafu wa Awamu ya Pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi (katikati) akifungua semina ya majadiliano kati ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma na wanahabari waliojadili rasimu ya Sheria Mpya ya Kudhibiti Mgongano wa Maslahi kwa Viongozi wa umma.
Mstaafu wa Awamu ya Pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi akifungua semina ya majadiliano kati ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma na wanahabari waliojadili rasimu ya Sheria Mpya ya Kudhibiti Mgongano wa Maslahi kwa Viongozi wa umma.
Mstaafu wa Awamu ya Pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi akifungua semina ya majadiliano kati ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma na wanahabari waliojadili rasimu ya Sheria Mpya ya Kudhibiti Mgongano wa Maslahi kwa Viongozi wa umma.[/caption] [caption id="attachment_49848" align="aligncenter" width="640"]Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Salome Suzete Kaganda (kwanza kushoto) akizungumza kwenye semina ya majadiliano kati ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma na wanahabari waliojadili rasimu ya Sheria Mpya ya Kudhibiti Mgongano wa Maslahi kwa Viongozi wa umma.
Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Salome Suzete Kaganda (kwanza kushoto) akizungumza kwenye semina ya majadiliano kati ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma na wanahabari waliojadili rasimu ya Sheria Mpya ya Kudhibiti Mgongano wa Maslahi kwa Viongozi wa umma.
Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Salome Suzete Kaganda akizungumza kwenye semina ya majadiliano kati ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma na wanahabari waliojadili rasimu ya Sheria Mpya ya Kudhibiti Mgongano wa Maslahi kwa Viongozi wa umma.
Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Salome Suzete Kaganda akizungumza kwenye semina ya majadiliano kati ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma na wanahabari waliojadili rasimu ya Sheria Mpya ya Kudhibiti Mgongano wa Maslahi kwa Viongozi wa umma
Baadhi ya washiriki katika semina ya majadiliano kati ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma na wanahabari waliojadili rasimu ya Sheria Mpya ya Kudhibiti Mgongano wa Maslahi kwa Viongozi wa umma.
Baadhi ya washiriki katika semina ya majadiliano kati ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma na wanahabari waliojadili rasimu ya Sheria Mpya ya Kudhibiti Mgongano wa Maslahi kwa Viongozi wa umma.(Martha Magessa)
Baadhi ya washiriki katika semina ya majadiliano kati ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma na wanahabari waliojadili rasimu ya Sheria Mpya ya Kudhibiti Mgongano wa Maslahi kwa Viongozi wa umma.
Baadhi ya washiriki katika semina ya majadiliano kati ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma na wanahabari waliojadili rasimu ya Sheria Mpya ya Kudhibiti Mgongano wa Maslahi kwa Viongozi wa umma.
Baadhi ya washiriki katika semina ya majadiliano kati ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma na wanahabari waliojadili rasimu ya Sheria Mpya ya Kudhibiti Mgongano wa Maslahi kwa Viongozi wa umma.
Baadhi ya washiriki katika semina ya majadiliano kati ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Ummana wanahabari waliojadili rasimu ya Sheria Mpya ya Kudhibiti Mgongano wa Maslahi kwa Viongozi wa umma.
Katibu Msaidizi Kanda ya Mashariki, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Getrude Cyriacus (wa kwanza kushoto) akiwasilisha mada juu ya Rasimu ya Sheria Mpya ya Kudhibiti Mgongano wa Maslahi kwa Viongozi wa umma kwa wanasemina.
Katibu Msaidizi Kanda ya Mashariki, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Getrude Cyriacus (wa kwanza kushoto) akiwasilisha mada juu ya Rasimu ya Sheria Mpya ya Kudhibiti Mgongano wa Maslahi kwa Viongozi wa umma kwa wanasemina.
Baadhi ya washiriki katika semina ya majadiliano kati ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma na wanahabari waliojadili rasimu ya Sheria Mpya ya Kudhibiti Mgongano wa Maslahi kwa Viongozi wa umma.
Baadhi ya washiriki katika semina ya majadiliano kati ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma na wanahabari waliojadili rasimu ya Sheria Mpya ya Kudhibiti Mgongano wa Maslahi kwa Viongozi wa umma.
 Na Joachim Mushi, Dar
Mstaafu wa Awamu ya Pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi amesema bado viongozi wa umma wanatumia madaraka yao na Ofisi zao kwa kujinufaisha wenyewe na kuwasahau wananchi waliowaweka madarakani hivyo kuna kila sababu ya kuleta sheria ya kuziba mianya hiyo kwa viongozi wanaokwenda kinyume na maadili.
Alhaj Mwinyi ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akifungua semina ya majadiliano kati ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma na wanahabari waliojadili rasimu ya Sheria Mpya ya Kudhibiti Mgongano wa Maslahi kwa Viongozi wa umma.
Alisema licha ya kuwepo kwa Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma ya mwaka 1995 inayotumika sasa bado kumekuwa na wimbi kubwa la mienendo ya matumizi mabaya ya ofisi na madaraka kwa viongozi wa umma kwa kujinufaisha wenyewe kimaslahi.
"...Maana yake ni kwamba umma sasa haupewi kipaumbele unavyo stahiki. Maamuzi ya viongozi yanatolewa kwa maslahi binafsi na hivyo kudhihirisha kuwepo kwa tatizo la mgongano wa maslahi. Viongozi hao waliopewa dhamana na wananchi wanatumia rasilimali za umma ili kujinufaisha binafsi au shughuli zao ambazo wanazo pembeni," alisema Rais huyo mstaafu.
Alisema hata hivyo sheria ya maadili ya viongozi wa umma imekuwa na mapungufu kwa kuwabana baadhi ya viongozi wa umma na kuwaacha wengine pamoja na watumishi wa umma hivyo kujikuta nao wakijihusisha na mgongano wa kimaslahi.
Hata hivyo, ameongeza kuwa tayari Serikali imeona mianya hiyo na hivyo kuanza mchakato wa kuja na sheria maalum itakayo dhibiti hali hiyo. "...Nadhani mmewahi kusikia mara kwa mara namna ambavyo Rais wetu Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akiagiza Serikali kufanya jitihada za dhati ili kuhakikisha kuwa viongozi wa umma wanaacha au wanajiepusha na tabia ya kushiriki zaidi kwenye biashara na kuacha jukumu lao...," alifafanua Mwinyi akiwaeleza washiriki wa semina hiyo.
Aidha aliipongeza Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kwa kuanza mchakato wa kutungwa kwa sheria Mpya ya Kudhibiti Mgongano wa Maslahi kwa Viongozi wa umma, ambapo itakapo kamilika huenda ikawa suluhisho la mgongano wa kimaslahi kwa viongozi na watumishi wa umma.
Rais huyo mstaafu aliwataka wanasemina kuijadili rasimu iliyowasilishwa na Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma na kutoa maoni yao kuiboresha zaidi ili itoke na majibu ya kero ya muda mrefu ya Mgongano wa Maslahi kwa Viongozi wa umma.
Kwa upande wake, Katibu Msaidizi Kanda ya Mashariki, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Getrude Cyriacus akiwasilisha mada juu ya Rasimu ya Sheria Mpya ya Kudhibiti Mgongano wa Maslahi kwa Viongozi wa umma kwa wanasemina kabla ya mjadala alisema wataalam wa Sekretarieti hiyo wamefanya utafiti kwenye mataifa mbalimbali na kutoka na mapendekezo ambayo yataongoza mjadala kuelekea kupata sheria nzuri.
Naye Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Salome Suzete Kaganda akizungumza katika semina hiyo, alisema Rasimu ya Sheria Mpya ya Kudhibiti Mgongano wa Maslahi kwa Viongozi wa umma walioiandaa itajadiliwa na wadau mbalimbali ili kupata maoni kabla ya kuwasilishwa kwenye baraza la makatibu wakuu kuboreshwa zaidi kabla ya mchakato kupanda ngazi za juu.
Aidha aliwataka wananchi na wadau wengine kuendelea kuijadili Rasimu ya Sheria Mpya ya Kudhibiti Mgongano wa Maslahi kwa Viongozi wa umma pindi itakapo wafikia na kutoa maoni kwa lengo la kuiboresha zaidi ili itakapo kamilika iweze kufanya kazi vizuri na kujibu kero zilizopo katika eneo hilo la viongozi wa umma.
"...Mapendekezo ya sheria hii hayalengi kuwafanya viongozi kuwa maskini, bali kasi yao ya ukwasi iendane na hali halisi ya kipato chao. Sheria hii itakapopitishwa itapunguza ubinafsi wa viongozi walioko madarakani kujipendelea wenyewe na maeneo wanayotoka." Alifafanua Jaji Kaganda.

RATIBA LIGI KUU BARA 2014/2015 HII HAPA


DSC_0007-546x291
Kocha mkuu wa Simba sc Patrick Phiri akiongea na wachezaji wake


Kocha mkuu wa Yanga akiongea na msaidizi wake
Baraka Mpenja, Dar es salaam
RATIBA ya ligi kuu soka Tanzania bara msimu wa 2014/2015 utakaoanza kutimua vumbi septemba 20 mwaka huu umeanikwa hadharani na Shirikisho la soka nchini Tanzania TFF.
Afisa habari na mawasiliano wa TFF, Boniface Wambura Mgoyo katika taarifa yake amesema ratiba hiyo imezingatia michuano ya Chalenji itakayochezwa Novemba, usajili wa dirisha dogo Nov 15- Des 15, ushiriki wa klabu za Azam na Yanga kwenye mashindano ya Ligi ya Mabingwa (CL) na Kombe la Shirikisho (CC).(P.T)
Wambura alisema mechi zitachezwa wikiendi ili kuongeza msisimko/kuwapa fursa washabiki wengi zaidi kuhudhuria, na katikati ya wiki imeachwa wazi kwa ajili ya mechi za Kombe la FA (Federation Cup).
Vilevile kutakuwa na mechi Boxing Day na siku ya Mwaka Mpya.
Siku ya ufunguzi zitapigwa mechi saba katika viwanja tofauti nchini ambapo mabingwa watetezi  Azam fc wataanza kutetea ubingwa wao dhidi ya wageni Polisi Morogoro katika uwanja wa Azam Complex, Chamazi, jijini Dar es saalam.
Yanga chini ya kocha Mbrazil, Marcio Maximo wataanza ugenini katika uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro dhidi ya wakata miwa wa Mtibwa Sugar.
Timu mbili zilizopanda ligi kuu msimu huu, Stand United na Ndanda fc zitachuana katika dimba la Kambarage mkoani Shinyanga.
Mgambo JKT watakawakaribisha Kagera Sugar katika dimba la CCM Mkwakwani jinni Tanga.
Ruvu Shooting wataanza kampeni zao katika uwanja wao wa Mabatini uliopo Mlandizi Pwani dhidi ya maafande wa Tanzania Prisons.
Wagonga nyumbo wa Mbeya City fc wataanza nyumbani katika dimba la CCM Sokoine Mkoani Mbeya dhidi ya JKT Ruvu.
Wekundu wa Msimbazi Simba chini ya kocha Mzambia, Patrick Phiri wao wataanza kampeni za kuusaka ubingwa wa ligi kuu bara septemba 21 dhidi ya Coastal Union uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Raundi ya pili  itacheza septemba 27 na 28 mwaka huu ambapo timu zote zitashuka dimbani.
Septemba 27, wekundu wa Msimbazi Simba watacheza mechi yao ya pili nyumbani dhidi ya Polisi Morogoro.
Mechi nyingine siku hiyo zitakuwa baina ya Mtibwa Sugar dhidi ya Ndanda fc katika uwanja wa Manungu Turiani. Azam watawakaribisha Ruvu Shooting Chamazi, Mbeya City watachuana na Coastal Union uwanja wa Sokoine, wakati Mgambo JKT watakuwa Mkwakwani kuchuana na Stand United.
Raundi ya pili itakamilika septemba 28 ambapo JKT Ruvu watavaana na Kagera Sugar katika uwanja wa Azam Complex.
Mechi nyingine itawakutanisha Yanga sc ya Maximo dhidi ya Tanzania Prisons uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Endelea kufuatilia mtandao huu kwasababu utaendelea kukujuza kuhusu ratiba nzima ya ligi kuu soka Tanzania bara.Na mimi mwandishi wako Nickson Luvega.

Israel na Hamas waendelea na mapigano

Ukanda wa Gaza ukishambuliwa na maroketi
Mgogoro kati ya Israel na Palestina unaendelea. Pande zote mbili zimekuwa zikishambuliana kwa maroketi. Wakati huo huo, Misri inataka mazungumzo ya kuleta amani yaanze tena.
Mgogoro kati ya Israel na Palestina unaendelea. Pande zote mbili zimekuwa zikishambuliana kwa maroketi. Wakati huo huo, Misri inataka mazungumzo ya kuleta amani yaanze tena.
Hali ya wasiwasi imerejea tena kwa wakaazi wa Israel na ukanda wa Gaza. Awali Israel na Hamas walikubaliana kuendeleza muda wa kusitisha mapigano. Lakini makubaliano hayo hayakuheshimiwa. Israel inasema kuwa hapo jana Hamas ilianza kurusha maroketi kuelekea Israel na ndipo Israel ilipojibu mashambulizi.
Wizara ya afya ya Palestina inaripoti vifo vya Wapalestina wasiopungua 10. Wengine 68 wamejeruhiwa. Israel kwa upande wake inasema kuwa ilifanya mashambulizi 60 ya angani. Ni mashambulizi yanayolenga nyumba za viongozi wa Hamas. Lakini sehemu kubwa ya watu wanaokufa ni raia wa kawaida. Bwana mmoja aliyeshuhudia mashambulizi kwa macho anaelezea kusikitishwa kwake na mauaji yanayoendelea. "Familia nzima imeuwawa: Baba, mke wake aliyekuwa na mimba pamoja na watoto wao watatu. Waisraeli wamelenga familia nzima bila kutoa taarifa na bila sababu yoyote."
Katika kisa kingine, watu watatu waliuwawa baada ya nyumba yao kubomolewa na roketi katika ukanda wa Gaza. Nyumba hiyo inaaminiwa kuwa ya kiongozi wa kijeshi wa Hamas, Mohammed Deif. Msemaji mmoja wa Hamas amethibitisha kuwa miongoni mwa waliouwawa walikuwepo mke na mtoto wa Deif. Waziri mmoja wa Israel amenukuliwa akisema kuwa Mohammed Deif anastahili kufa kama vile Osama bin Laden alivyokufa. Waziri huyo aliongezea kuwa Deif ni muuaji na kwamba Israel itatumia kila nafasi itakayojitokeza kujaribu kumuua kiongozi huyo wa Hamas.
Kwa sasa hakuna ishara za mgogoro huu kutulia. Israel imewaandaa maaskari 2,000 wa ziada kwa ajili ya kufanya operesheni za ardhini wakati wowote ule.
Hata mazungumzo ya kuleta amani yaliyokuwa yakiendelea Cairo, Misri yamesitishwa. Wawakilishi wa pande zote mbili wamegoma kuendelea na juhudi za kupata suluhu ya mgogoro. Misri imewaasa Hamas na Israel kurejea katika meza ya mazungumzo, ikisema kuwa inajaribu kushawishi pande zote mbili kuheshimu makubaliano ya kusitisha mapigano kwa muda. Kwa mujibu wa viongozi wa Palestina na wawakilishi wa Umoja wa Mataifa, zaidi ya watu 2,000 wameuwawa tangu mgogoro huu ulipoanza mwezi uliopita.
Mwandishi: Nickson M Luvega
Mhariri: Yohana John