Jumanne, 21 Julai 2015

Mtoto huyu ameweza kuishi kwa miaka 12 na virusi vya Ukimwi bila kutumia dawa yoyote!


HIV
Nimekutana na stori mmoja kutoka Ufaransa inayomhusu mtoto wa miaka 18 aliyeweza kuishi na Ukimwi kwa miaka 12 bila kutumia dawa zozote wala vidonge vyovyote vya ARV.
Kitendo hiki kimeweka headlines nyingi sana nchini Ufaransa na kimeleta matumaini mapya ya kupata tiba ya ugonjwa wa Ukimwi, kwa njia ya kushusha virusi kwa viwango vya chini mwilini bila kutumia tiba ya kupunguza makali.
HIV2
Msichana huyo alikuwa akitumia tiba ya kupunguza makali mpaka alipotimiza miaka 6 na baada ya mwaka mmoja timu ya madaktari iligundua kuwa virusi vya mtoto huyo haviongezeki, havipungui wala kuathiri mwili wake kwa namna yoyote ile.
Na tangu kipindi hicho ameweza kuishi na virusi hivyo bila venyewe kuonekana kwenye damu yake na bila kutumia dawa yoyote hali inayojulikana kama “remission” – virusi kutokuongezeka wala kupungua mwilini, kwa miaka 12.
HIV3
Madaktari wanaamini kutakuwa na kitu cha tofauti kwenye mfumo wake wa damu iliyoiwezesha dawa alizokuwa anazitumia akiwa mtoto kudhibiti ongezeko la virusi, lakini kwa sasa hali nzima juu ya uvumbuzi huu bado ni utata kwa madaktari.
HIV4
Daktari kutoka The Institut Pasteur nchini Ufaransa amesema kwamba hii ni mara ya kwanza ndani ya miaka mingi kwa hali hii kujitokeza kwa watoto ama kijana kwenye ripoti aliyowasilisha kwenye Press Conference ya The 8th IAS Conference on HIV Pathogenisis Treatment and Prevention mjini Vancouver wiki hii.

Ijumaa, 29 Mei 2015

Watoto elfu 250 huenda wakafa kwa njaa Sudan

Watoto elfu 250 huenda wakafa kwa njaa Sudan

Mshirikishi mkuu wa shirika la Umoja wa mataifa nchini Sudan Kusini, Toby Lanzer, amesema kuwa takriban watoto laki mbili u nusu wamo katika hatari ya kufa katika kipindi cha miezi kadhaa ijayo iwapo mashirika ya utoaji misaada, hayatafikisha misaada kwa watu walio na mahitaji.
Wafuasi wa Rais Salva Kiir na mpinzani wake Riek Machar wanaendelea kupigana 

Bwana Lanzer ameiambia BBC kuwa, watu wanateseka kwa sababu ya umaskini.
Vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Sudan Kusini imesambaratisha uchumi wa taifa hilo.
Watoto zaidi ya laki mbili u nusu wamo katika hatari ya kufa kwa njaa

Amesema kwamba mashirika ya utoaji misaada yatafanya yawezavyo kuwasaidia wahitaji, lakini amani itapatikana tu nchini Sudan Kusini iwapo viongozi watakubaliana kukomesha mapigano.
Bwana Lanzer amewasihi viongozi wa pande hasimu kusameheana ilikukomesha maafa.

Ni Diamond Platnumz tena kwenye Headlines time hii kamshirikisha Mr. Flavour


XXXX
Hii ni kolabo nyingine kutoka kwa Mtanzania Diamond Platnumz ambayo hii kamshirikisha mkali kutoka Nigeria Mr.Flavour wimbo unaitwa Nana,video imefanywa na GodFather mtu wangu.

Diamond Platnumz ametumia dakika hizi tatu kumuimbia mrembo aliye mbele ya macho yake,unaweza kumuandikia chochote hapa Diamond kisha baadae atapita na kusoma comment yako mtu wangu.
XX2


Jumamosi, 23 Mei 2015

IRELAND YAFANYA MAAMUZI KUHUSIANA NA NDOA ZA JINSIA MOJA

wapiga kura wajitokeza kwa wingi nchini Ireland ili kuamua kuhusu kuhalalishwa kwa ndoa za watu wa jinsia moja.

Wapiga kura wengi wameripotiwa kujitokeza kwenye kura ya maoni nchini Ireland ya kuamua iwapo ndoa za watu wa jinsia moja zinaweza kuhalalishwa .
Katika sehemu nyingine ukiwemo mji mkuu Dublin na miji mingine, idadi ya wapiga ilitarajiwa kufikia takriban asilimia 60.

Ndoa za jinsia moja   

Wataalamu wengi wa Ireland walio katika mataifa ya kigeni walirudi nyumbani kupiga kura.
Wale wanaounga mkono ndoa za jinsia moja walitarajia watu wengi kujitokeza.

Wapenzi wa jinsia moja wakitoka katika kituo cha kupiga kura

Ikiwa kura hiyo itafanikiwa Ireland itakuwa nchi ya kwanza kuhalalisha ndoa za jinsia moja kupitia upigaji kura.
Matokeo yanatarajiwa kutangazwa baadaye leo.

 

ZAIDI YA WATU 40 WAUAWA MEXICO

Polisi nchini Mexico

Takriban watu 43 wameuawa wakati wa ufyatulianaji wa risasi katika jimbo la Michoacan nchini mexico kati ya vikosi vya usalama na genge moja lenye silaha.
Mapigano hayo yalianza wakati magari ya polisi yalipofyatuliwa risasi kwenye barabara moja kuu katika kijiji kilicho karibu na mpaka na jimbo la Jalisco.
Moja ya megenge hatari zaidi ya madawa ya kulevya, liko eneo hilo na limekuwa likipigana vita vigumu katika jimbo la Michoacan kwa miaka mingi.
Maafisa kutoka kwa idara za usalama wanaelekelea eneo hilo kufanya uchunguzi.

REAL MADRID YAWASILIANA NA BENITEZ

Rafael Benitez

Mkufunzi wa kilabu ya Napoli Rafael Benitez ameorodheshwa miongoni mwa makocha wataokumrithi Carlo Ancelotti katika kilabu ya Real Madrid.
Ancelotti anatarajiwa na wengi kuachana na kilabu hiyo baada ya mechi ya mwisho na Getafe wikiendi hii.
Mazungumzo kati ya Real Madrid na Benitez yanaendelea huku kandarasi ya Benitez katika kilabu ya Napoli ikitarajiwa kukamilika mwezi ujao,ijapokuwa hakuna makubaliano yalioafikiwa.
Klabu ya West Ham pia iliwasiliana na kocha huyo ambaye aliwahi kuifunza Chelsea na Liverpool.

Carlo Ancelotti

Mkufunzi wa West Ham ambaye anaiandaa West Ham dhidi ya Newcastle anatarajiwa kuanzisha mazungumzo na klabu hiyo kuhusu hatma yake wiki ijayo.
Benitez alianza kazi ya ukufunzi katika kilabu ya Real Madrid B na pia amewahi kuifunza Valladolid,Osasuna,Etramadura,TenerifeValencia na Inter Milan.

DAVID LUIZ:'NIMEWAHI KUSHIRIKI NGONO'

David Luiz kushoto 


Mlinzi wa klabu ya Paris St-Germain David Luiz amevishtumu vyombo vya habari kwa kukosa heshima baada ya kukanusha madai kwamba yeye hajawahi kushiriki katika tendo la ngono.
Ripoti hizo zilianza kusambaa baada ya mchezaji huyo wa zamani wa Chelsea mwenye umri wa miaka 28 kusema katika instagram kwamba yeye na mpenziwe ''wako tayari kungojea''.
Aliiambia BBC focus kwamba.''Dini yangu,ubaatizaji wangu,nafurahia.
Watu wanasema maneno kila mahala kuhusu iwepo mimi sijawahi fanya tendo la ngono.''Ukweli ni kwamba mimi nishawahi kushiriki katika tendo hilo''.
 
    Luiz 
Aliongezea:Watu wengine katika vyombo vya habari hawaheshimu maisha ya watu.
Mimi ninawaheshimu wenzangu kwa hivyo sina bughudha ya aina yoyote.