Kikao cha Bunge leo Novemba 27 kimeanza kwa maswali mawili kuulizwa na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni Freeman Mbowe kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda.
“…Chini ya
 uongozi wako kama Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na 
ukiwa kiongozi wa shughuli za Kiserikali Bungen, tumeiona Serikali 
ikikumbana na matatizo na vikwazo vingi ikiwemo ‘Operesheni Tokomeza’ 
ambayo ilipelekea wananchi wengi kupoteza maisha na wengine kupata 
vilema…“– Mbowe.
Tumeona 
mauaji ya raia yakiendelea Kiteto, kashfa kubwa ambayo iko current sasa 
hivi ikiwa ni pamoja na kauli zako ulizowahi kuzisema kwamba fedha 
zilizopotea za akaunti ya Escrow hazikuwa fedha za umma bali zilikuwa 
fedha za watu binafsi…“– Mbowe.
Baada ya 
Ripoti ya CAG kutolewa hadharani kuhusiana na fedha za Escrow na baada 
ya Ripoti ya PCCB kutolewa na hatimaye jana hapa Bungeni kusomwa taarifa
 ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali, nini msimamo wako kuhusu 
kauli yako ya awali kwamba fedha zile zilikuwa ni za watu binafsi na sio
 fedha za umma?“– Mbowe.
Kwa uzito 
huo ukichanganya na matukio mengine mbalimbali ambayo yamepelekea 
fedheha kubwa kwa taifa letu, huoni kama ingekuwa muafaka kwako binafsi 
na taifa kupumzika kidogo ili kupisha nafasi kwa watu wengine kuweza 
kumalizia ngwe hii ya utawala wenu?”– Mbowe.
Akijibu maswali hayo, Waziri Mkuu Mizengo Pinda amesema; “…Inawezekana
 Mheshimiwa Mbowe una shauku ya kutaka litokee hilo lakini mambo haya 
yanategemea kama ndivyo Mungu kapanga au hapana…“
Ningeweza 
nikajaribu kukujibu lakini sina sababu ya kufanya hivyo, sina sababu ya 
kufanya hivyo kwa sababu suala lenyewe ndiyo subject ya mjadala hapa 
Bungeni ambao unaanza leo.. Tusubiri mjadala utakavyokwenda naamini na 
mimi nitapata nafasi ya kusema mawili matatu, kwa hiyo nadhani mwisho wa
 yote Bunge litakuwa limefikia mahali ambapo tunaweza tukasema kwa 
uhakika ni hatua stahiki namna gani inaweza kuchukuliwa…” Waziri Mkuu Mizengo Pinda.
Baada ya majibu hayo, Mbowe alipata nafasi ya kuuliza swali la nyongeza kwa Waziri Mkuu; “…Pamoja
 na kwamba jambo hili litajitokeza baadaye katika mijadala ya leo, bado 
haiondoi ukweli kwamba una wajibu wa kulijibu swali langu. Naomba kwa 
heshima sana nikuulize tena kwa mara nyingine, taifa limepata fedheha 
kubwa sana kutokana na sakata hili, nchi nzima inasikiliza tatizo hili…“– Mbowe.
“…Una 
heshima kama kiongozi wa Serikali lakini heshima ambayo itakuwa 
imethibitishwa zaidi kama utaamua kujiwajibisha mwenyewe ili kuweka 
heshima yako na heshima ya Serikali, je kwa mara nyingine huoni ingekuwa
 vema kama basi utujibu kama unafikiri bado zile fedha ni za umma kama 
hutaki ku-declare kujiuzulu katika hatua ya sasa?”– Mbowe.
Akijibu swali hilo, Waziri Mkuu amesema; “…Naomba
 nirudie nilichosema, suala la kujiuzulu si jipya lakini maadam jambo 
hili liko hapa Bungeni, unatanguliza hili jambo kwanini? Tungoje 
tujadili tufikie mwisho halafu tutaamua…”– Mizengo Pinda.
Nimekurekodia sauti ya wakati maswali hayo yakiulizwa na kujibiwa Bungeni leo Dodoma, unaweza kusikiliza kwa kubonyeza play.






0 comments:
Chapisha Maoni