Usiku wa kuamkia leo October 16 2015 majukwaa ya siasa Tanzania
yametawaliwa na ajali ya Helikopta ambayo imeanguka na kulipuka kwenye
mbuga ya Wanyama ya Selous ambapo Waziri wa maliasili na utalii Lazaro
Nyalandu alithibitisha kwamba mmoja wa waliokuwemo ndani ni Mbunge wa
Ludewa Deo Filikunjombe (CCM).
Kupitia ukurasa wake wa Twitter,Nyalandu aliandika;
"Tumetuma vikosi vya maafisa na maaskari katika eneo la Selous
kulikotokea ajali ya helikopta katika harakati za uokozi, ajali ya
helikopta imetokea katika kitalu R3 ndani ya mbuga ya Selous na
mashuhuda wanasema ilianguka na kulipuka ng’ambo ya mto Ruaha
"Mashuhuda wa ajali ya helikopta iliyotokea Selous walikuwa kitalu R2 na
walishuhudia ikianguka na kulipuka ng’ambo ya mto Ruaha Kitalu R3,
Maafisa na Maaskari wanaelekea eneo la tukio kutokea Msolwa na Matambwe
na tumeagiza vikosi vilivyo kwenye doria Selous kushiriki uokoaji
"Mashuhuda wa ajali ya helikopta Selous walikuwa Kitalu R2 wanasema
ilianguka baada ya majira ya saa 12 jioni na kulipuka, serikali kupitia
wizara ya maliasili na utalii inachukua hatua zote kuwafikia wahanga na
majeruhi wa ajali ya helikopta Selous usiku huu
"Nimeagiza section 2 zenye askari 16 kutoka Matambwe na Msolwa (Selous)
kwenda eneo la tukio, RPC Morogoro na mkuu kanda ya Msolwa (Selous)
wanashirikiana, hatujui kitakachokuwa kimewapata wasafiri ndani ya
helikopta iliyoanguka akiwepo Mh, Filikunjombe, tuungane kuwaombea kwa
Mungu"
Katika taarifa nyingine kutoka upande wa CCM iliyotolewa na naibu waziri
wa mawasiliano sayansi na teknolojia January Makamba mida ya saa sita
usiku ilisema: "Tumesikia habari za chopa kuanguka huko Selous. Mungu
aepushe kusiwe na majeruhi. Chopa zote zinazotumiwa na CCM kwenye
kampeni ziko salama"
Baadae aliandika :"Kwakuwa ilisemekana kuwa chopa ya kampeni ya
CCM imeanguka, tulifuatilia/kubaini/kuripoti kuwa tulizokodi kama Chama
hakuna iliyoanguka". Hiyo ndio ilikua tweet ya mwisho kuandikwa na
January Makamba usiku lakini badae aliretweet kilichoandikwa na Waziri
Nyalandu na Zitto Kabwe.
Zitto aliandika: "Naomba utulivu.(1) ajali ya helkopta
imethibitishwa (2) kuwaka hakujathibitishwa (3) ndugu yangu Deo
alikuwamo (4) hakuna uthibitisho wa madhara, naomba utulivu mpaka tupate
taarifa rasmi zilizothibitishwa na mamlaka husika, naomba sana hilo ili
kuepuka sintofahamu"
Ijumaa, 16 Oktoba 2015
Home »
» HABARI KUHUSU HELIKOPTA YA CCM ILIYOANGUKA MBUGANI IKIWA NA MBUNGE DEO FILIKUNJOMBE
HABARI KUHUSU HELIKOPTA YA CCM ILIYOANGUKA MBUGANI IKIWA NA MBUNGE DEO FILIKUNJOMBE
Related Posts:
Na hii ni nyingine tena! Wasanii walioandamana nusu uchi Nairobi Kenya. Siku hizi ishu ya kuvua nguo kuonyesha msisitizo au kulipigia kelele jambo flani imekua kawaida, yani wengi wameitumia hii njia kufikisha malalamiko yao na mfano mzuri ni hivi karibuni kwa Wanafunzi wa kike kwenye … Read More
VIONGOZI WATUMIA MADARAKA YAO KUJINUFAISHA Mstaafu wa Awamu ya Pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi (katikati) akifungua semina ya majadiliano kati ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma na wanahabari waliojadili rasimu ya Sheria Mpya ya Kudhibiti Mgongano wa … Read More
Je Toni Kroos ndio kamkimbiza Alonso Madrid? Xab Alonso ajibu.Kiungo wa kimataifa wa Spain Xabi Alonso amejiunga na klabu ya FC Bayern Munich ya Ujerumani akitokea kwa mabingwa wa ulaya Real Madrid kwa ada ya uhamisho wa paundi millioni 5. Alonso ambaye alijunga na Real Madrid… Read More
HATIMA YA TORRES CHELSEA;HIKI NDICHO ALICHOKISEMA Fernando Torres amemaliza kipindi kigumu kabisa cha miaka mitatu na nusu kwenye maisha yake ndani ya klabu ya Chelsea baada ya kukubali kuondoka katika timu hiyo. Fernando alijiunga na Chelsea mnamo mwaka 2011 January kw… Read More
Baada ya Okwi kutangaza kujiunga na Simba,hiki ndicho walichokifanya Yanga. Ikiwa imepita siku moja toka klabu ya Simba kumtangaza Emmanuel Okwi kama mchezaji wao rasmi wa klabu hiyo,taarifa nyingine iliyotolewa leo na uongozi wa Yanga ni kumshitaki Okwi. Klabu ya Young Africans imemshitaki Emman… Read More
0 comments:
Chapisha Maoni